Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Mbona hawa watetema, wakubwa wanatetema,
Wapo wanahema hema, midomo imeachama,
Na meno yanawauma, mwili ukiwatetema,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!
Wamejipanga mamia, makumi ya mia na mia,
Kwa zamu wahutubia, ahadi wakimwagia,
Huku wakitukania, mioyo ikiwakimbia,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!
Mbuyu ukitikisika, ni mwanzo wa kuanguka,
Mizizi itachomoka, chini "puu" kusikika,
Si punje itaokoka, majani yatapukutika,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!
Nimeshika togwa miye, nakunywa naangalia,
Nasubiri nisikie, walotetema wanalia,
Ujumbe uwafikie, imebadilika Tanzania,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Wapo wanahema hema, midomo imeachama,
Na meno yanawauma, mwili ukiwatetema,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!
Wamejipanga mamia, makumi ya mia na mia,
Kwa zamu wahutubia, ahadi wakimwagia,
Huku wakitukania, mioyo ikiwakimbia,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!
Mbuyu ukitikisika, ni mwanzo wa kuanguka,
Mizizi itachomoka, chini "puu" kusikika,
Si punje itaokoka, majani yatapukutika,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!
Nimeshika togwa miye, nakunywa naangalia,
Nasubiri nisikie, walotetema wanalia,
Ujumbe uwafikie, imebadilika Tanzania,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)