Mbona wanatetemeka, upepo haujavuma?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929
Mbona hawa watetema, wakubwa wanatetema,
Wapo wanahema hema, midomo imeachama,
Na meno yanawauma, mwili ukiwatetema,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!

Wamejipanga mamia, makumi ya mia na mia,
Kwa zamu wahutubia, ahadi wakimwagia,
Huku wakitukania, mioyo ikiwakimbia,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!

Mbuyu ukitikisika, ni mwanzo wa kuanguka,
Mizizi itachomoka, chini "puu" kusikika,
Si punje itaokoka, majani yatapukutika,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!

Nimeshika togwa miye, nakunywa naangalia,
Nasubiri nisikie, walotetema wanalia,
Ujumbe uwafikie, imebadilika Tanzania,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
THINGS HAVE CHANGED ALOT MKUU,

NO LONGER AT EASY.

Moto uliowaka Igunga na sasa Arumeru ni ushahidi tosha siku zinahesabika lazima wateteme.
 
Mbona hawa watetema, wakubwa wanatetema,
Wapo wanahema hema, midomo imeachama,
Na meno yanawauma, mwili ukiwatetema,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!

Wamejipanga mamia, makumi ya mia na mia,
Kwa zamu wahutubia, ahadi wakimwagia,
Huku wakitukania, mioyo ikiwakimbia,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!

Mbuyu ukitikisika, ni mwanzo wa kuanguka,
Mizizi itachomoka, chini "puu" kusikika,
Si punje itaokoka, majani yatapukutika,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!

Nimeshika togwa miye, nakunywa naangalia,
Nasubiri nisikie, walotetema wanalia,
Ujumbe uwafikie, imebadilika Tanzania,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

Ni shairi zuri kwa both sides of the story, yaani iwapo CDM itashinda ama haitashinda. Kama haitashinda ina maana itakuwa imefanikisha kuwatetemesha CCM. Its well worked!
 
Elimu ya uraia kwetu,imegeuka sumu kwao,
Hotuba za nyerere tamu,wao zimegeuka nyongo,
Hata wazee vidole viwili juu, Kijani hazivaliki hata kiteto,


Hahahahahaha! nimejaribu!
 
Elimu ya uraia kwetu,imegeuka sumu kwao,
Hotuba za nyerere tamu,wao zimegeuka nyongo,
Hata wazee vidole viwili juu, Kijani hazivaliki hata kiteto,


Hahahahahaha! nimejaribu!
Walidhani hakuchwi, sasa kumbe kumepambazuka.

na mimi nimejaribu.
 
Mbona hawa watetema, wakubwa wanatetema,
Wapo wanahema hema, midomo imeachama,
Na meno yanawauma, mwili ukiwatetema,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!

Wamejipanga mamia, makumi ya mia na mia,
Kwa zamu wahutubia, ahadi wakimwagia,
Huku wakitukania, mioyo ikiwakimbia,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!

Mbuyu ukitikisika, ni mwanzo wa kuanguka,
Mizizi itachomoka, chini "puu" kusikika,
Si punje itaokoka, majani yatapukutika,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!

Nimeshika togwa miye, nakunywa naangalia,
Nasubiri nisikie, walotetema wanalia,
Ujumbe uwafikie, imebadilika Tanzania,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

tena wanawaya waya, nguo zinao uzani,
bora wangesoma aya, singewindwa ka kunguni,
wajapoimbiwa kwaya, pepo lipo kiunoni,
na upepo haujavuma, ukivuma ni anguko.

ukivuma ni anguko, kutowesha vichokoo,
kama wa kisulisuli, ole ni kwa zao koo,
ghiliba zimewakatili, sasa wanaona soo,
chama kongwe mapinduzi, kimejipindua pindu.
 
tena wanawaya waya, nguo zinao uzani,
bora wangesoma aya, singewindwa ka kunguni,
wajapoimbiwa kwaya, pepo lipo kiunoni,
na upepo haujavuma, ukivuma ni anguko.

ukivuma ni anguko, kutowesha vichokoo,
kama wa kisulisuli, ole ni kwa zao koo,
ghiliba zimewakatili, sasa wanaona soo,
chama kongwe mapinduzi, kimejipindua pindu.

Kumbe nawe "mayu" mkali kweli kweli"
 
Uuuuuuuuuwi! maarufu,Arumeru Mashariki,
Yanogesha maradufu,CHADEMA haishikiki,
CCM yawa mfu,lakini haishtuki,
Na bado!

Na ule wa Segerea,unaojongea,
Napo watajionea,CHADEMA kidedea,
Matusi watatupia,makamanda puuzia,
Na bado!
 
Magamba wapapatika,Nguo pia kuchanika,
Hawakioni cha kushika,Wananchi wamefunguka,
Hata raia wanateka,Mwisho wao umefika,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom