Mbona sioni kosa la Nyalandu ?

Mbona sioni kosa la Nyalandu ?

nakuona

Member
Joined
May 4, 2012
Posts
19
Reaction score
9
NIMEKUWA mfuatiliaji mzuri sana wa mambo yanayoendelea huko nyumbani, hasa sakata la Tanapa na Lazaro Nyalandu- pamoja na mambo mengi yaliyosemwa ukisoma gazeti hili la Rai,ambalo limetuwekea barua Nyalandu aliyoiandika kwenda Tanapa. Unaona kuwa Nyalandu hajafanya kosa lolote bali ameonyesha uelewa mkubwa katika uongozi na utatuzi wa Migogoro. Binafsi sioni kosa lake hebu wadau someni wenyewe:

Siri yafichuka Maliasili na Utalii
Naibu Waziri chabainika
*Kampuni ya utalii iliyofungiwa yafunguliwa
WAKATI mgogoro unaolihusisha Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kampuni ya utalii yaAhsante Tours ukielekea ukingoni, hatua aliyochukua Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, imewekwa bayana.

Uhalisia wa hatua hiyo ambayo ililalamikiwa kwamba iliingilia utendaji kazi wa TANAPA, umefahamika baada ya RAI kufanikiwa kuiona nakala ya barua ambayo iliandikwa na Naibu Waziri huyo, Novemba 23, mwaka huu kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi.

Miongoni mwa madai yaliyoibuka baada ya hatua hiyo ya Nyalandu, ni pamoja na madai kuwa maelekezo yake kwa TANAPA yalikuwa na sura ya kuibeba kampuni ya Ahsante, jambo ambalo alilipinga.

Barua hiyo yenye kumbukumbu namba AB 315/484/01 inasomeka; “YAH: KUFUNGIWA KWA KAMPUNI YA “AHSANTE TOURS” KUINGIZA WATALII HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA.

“Tafadhali rejea kichwa cha barua hapo juu, na barua yako Kumb. TNP/HQ/L.10/29 iliyoandikwa kwa Mkurugenzi Mtendaji, “Ahsante Tours” ya Mjini Moshi.

“Leo, tarehe 23/11/2012 nimefanya kikao hapa wizarani na wakurugenzi wa Kampuni ya “Ahsante Tours”, Bi Stella Swai na Bwana Cuthbert Swai, ambao waliomba wizara iangalie upya athari ambazo zitatokana na “Ahsante Tours” kufungiwa kuingiza wageni katika Hifadhi za Taifa (TANAPA).

“Wizara inasisitiza kwamba ni muhimu “Tour Operators” wote walipe viingilio vya Hifadhi za Taifa kabla wageni wao hawajaingia hifadhini, ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kwa wageni na kwa mapato ya TANAPA.

“Aidha, kwa kuzingatia maelezo ambayo wizara imeyapata kutoka kwa wakurugenzi wa “Ahsante Tours”, na kutoka kwako, ni dhahiri kwamba maamuzi ya Mkurugenzi Mkuu ya kuwaruhusu walipe baadaye (post payment) yalilenga kuiwezesha kampuni kumudu “cash flow” zao kwa kipindi ambacho walikuwa wamekopa US$ 1,300,000 kutoka Benki ya TIB kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa Weruweru River Lodge; lodge ambayo imegharimu US$3m.

“Kwa taarifa ambazo wizara imezipata, kampuni hii ya wazawa inailipa TANAPA dola milioni 2 kila mwaka kama “entry fees” hifadhini, na kwa taarifa kutoka KINAPA, Ahsante Tours ni kampuni ya pili kwa kuingiza watalii wengi zaidi Mlima Kilimanjaro.

“Kwa kuwa sera za Serikali ya CCM ni kuwawezesha wananchi kiuchumi, wizara inafurahishwa na taarifa kuwa Ahsante Tours wameajiri wafanyakazi (temporary staff) 650, ambao ni porters na guides, pamoja na wafanyakazi wengine 41 ofisi kuu, na wengine 38 kwenye Weruweru River Lodge.

“Kutokana na maelezo hayo, kiasi cha deni ambacho TANAPA ilikuwa inaidai kampuni hii kuanzia Septemba 2011 ni US$ 70,000, na hadi sasa kiasi cha deni lililobaki ni US$ 39,000; kiasi ambacho pamoja na kuendelea kulipa deni la TIB, bado kampuni hii ni dhahiri inao uwezo wa kulilipa bila kuathiri biashara ya utalii.

“Kwa kuzingatia kufungiwa kwa Ahsante Tours kutaathiri idadi kubwa ya watalii ambao wanatarajiwa kutembelea nchi yetu, kutahatarisha zaidi ya wananchi 700 kupoteza kazi zao, na kutapoteza mapato kwa TANAPA yapatayo US$2m kwa mwaka, ikiwa ni pamoja na kuifanya kampuni yenyewe kufilisiwa kwa kuwa haitakuwa na uwezo wa kuilipa TIB, na hivyo kufungwa kwa Weruweru River Lodge, na hivyo kupoteza idadi ya vitanda 68 vya kulaza watalii Kilimanjaro.

“Naagiza yafuatayo yafanyike:-

(1)TANAPA na Ahsante Tours wafanye kikao cha pamoja, Jumatatu, tarehe 26, Novemba 2012, ili kupanga upya mpango wa jinsi deni hilo litakavyolipwa bila kuathiri uendeshaji wa shughuli za maelfu ya watalii wanaopitia Ahsante Tours (payment plan).

“(2) Mpango huo uonyeshe ni kiasi gani Ahsante Tours itailipa TANAPA kila mwezi kuanzia sasa hadi deni la US$ 39,000 kuisha na izingatiwe kwamba makubaliano hayo ni sharti yaheshimiwe na pande zote mbili ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza kwa shirika kupoteza mapato au kampuni kuchukuliwa hatua zaidi.

“(3) Watalii wote waliofanyiwa “booking” na Ahsante Tours kwa safari zinazoanzia sasa sharti walipiwe “entry fees’ kabla ya kuingia hifadhini kama sera na kanuni za TANAPA zinavyoelekeza, na kwa vyovyote vile kusiwepo ongezeko la deni jipya, ili kuweza kulimaliza kabisa tatizo hili kwa mpango wa (win-win situation). Mwisho, nakutakia utekelezaji mwema.”

Hatua ya kuifungia kampuni ya Ahsante Tours ilichukuliwa na uongozi wa TANAPA, baada ya kampuni hiyo kushindwa kulipa dola za Marekani 31,000 zilizokuwa zimesalia kati ya dola 70,000 ilizokopeshwa ili iweze kuhudumia watalii, baada ya muda wa makubaliano kumalizika.

Mmoja wa watoa habari wetu wizarani hapo, alisema kuwa si sahihi kusema Naibu Waziri, alikuwa na maslahi kwenye sakata hilo, kutokana na ukweli kujidhihirisha kwenye barua yake kwenda TANAPA, ndio sababu alihimiza kuwa watalii wote walipe “entry fees”, na usiwepo upendeleo wowote, badala yake iwepo “win-win situation.”

Kuifungulia Ahsante Tours

Taarifa zilizoifikia RAI kabla ya kwenda mitamboni jana, zilisema kuwa kampuni hiyo ilifunguliwa juzi Jumanne na sasa inaendelea na shughuli zake.

Taarifa hizo pia zilithibitishwa na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi, ambaye alisema wameifungulia kampuni hiyo baada ya kulipa deni lililokuwa limesalia.

“Tumewafungulia baada ya kulipa deni na kuandika apology kutokana na usumbufu wote uliojitokeza, kwa sasa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida,” alisema Kijazi
 
Back
Top Bottom