voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,553
- 11,885
Nianze kwa kumpa Hongera Mheshimiwa Dotto Biteko (Mb).kwa uteuzi wa Nyadhifa mbili mpya kwa wakati mmoja.
Lakini tujiulize hili jambo la kiutendaji ukizingatia kwamba wizara ya Nishati sio lele mama!
Ni wizara nyeti inayotakiwa usimamizi wa kiuongozi kwa karibu sana.
Ni wizara inayobeba kiini cha maendeleo ya nchi katika kila safu .
Uchumi wa Viwanda.
Ujasiriamali mkubwa na mdogo.
Uendelezaji wa shughuli za Migodi.
Uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kiserikali maofisini.
Lakini pia na maisha ya kawaida ya kila siku nchini.
Hii ni kutokana na umuhimu wa Nishati ya Umeme kiutendaji kama Nyenzo wezeshi.
Lakini pia kuna changamoto nyingi zaidi kwenye hii wizara ikiwamo ukamilishaji wa Bwawa la umeme la JNHP.
Na tukubali kwamba mpaka sasa nchi yetu inapitia kipindi kigumu cha upatikanaji wa nishati hiyo kwa kiwango cha chini kutokidhi mahitaji ya matumizi nchini.
Tulitarajia kupata waziri mpya ambaye angekuja kukaa na kutafuta muarobaini wa tatizo hili.
Sasa tunapopewa Naibu waziri mkuu na hapohapo akawa amepewa mikoba ya Ugonjwa wa Tanesco nchini.
Itakuwaje endapo Naibu waziri mkuu akashindwa jinsi ya kujigawa mtu mmoja ofisi mbili?
Je!
Ni lini anakuwa waziri wa Nishati na ni lini anakuwa Naibu waziri mkuu?
Je!
Linapoketi Baraza la Mawaziri,yeye anakuwa upande upi kwa mfano.Yaani anaketi katika kiti kipi?
Je?
Atakapokuwa ofisini Wizarani,ataandamana na huo msafara wa Naibu waziri mkuu?
Nisaidieni kutudadavulia hili enyi wajuvi.
Cc.
Pascal Mayalla
GENTAMYCINE
Na wengineo.