Mbona mabasi yaendayo kasi hayapo njiani?

Mbona mabasi yaendayo kasi hayapo njiani?

Mtoa mada umenishtua maana jana nilikua na rafiki yangu katoka Zanzibar anaenda Moro akaniuliza swali hilihili kuwa yale mabasi yaendayo kasi yako wapi?
Nikamuambia ni usanii wa kisiasa tu ule watu walikuwa wanatafuta kick maana hata barabara zenyewe hazijakamilika.
 
Mabasi yaendayo kasi yapo mengi sema yanapita spidi kali sana. Ukitaka kuliona au kupanda usisubirie kimara mwisho nenda mbezi au usikae kivukoni we kasubirie kigamboni ndo huwa angalau yanapunguza speed
 
Hukunipa taarifa ili niwaruhusu vijana wangu wayalete barabarani, jipange upya alafu ukiw atayari utanijulisha kwamaana hapa Wizarani tuna kazi nyingi.
 
Nimefunga safari toka Moro leo asubuhi kuja DSM ili nishangae mabasi yaendayo kasi.

Cha kusikitisha sijabahatika kuyaona! na ni hivi majuzi mradi ulizinduliwa!

Kulikoni mabasi hayo hayapo njiani tena?.


Leo nimelipanda
 
Back
Top Bottom