Mbona haeleweki nifanyeje?

Mbona haeleweki nifanyeje?

Cleofa

Member
Joined
Apr 27, 2015
Posts
9
Reaction score
0
Habari wana Jf,

Nlimkosea mpenzi wangu ni muda sisi umepita nilikiri kosa na kuomba msamaha nikimshirikisha mpaka dadayake wiifi angu badae alikubali msamaha wangu mambo yakaisha.

Mwaka mmoja baadae ghafla alibadilika nikimtmia sms hajibu nukimpigia hapokei, nikamtumia sms vipi mbona kimya hata ukikuta missed call hunitafuti?

Alichojibu ni yale yale ya mwaka juzi ndio mana ipo ivo, je ana mapenzi tena na mimi? Kuna sababu ya mimi kuendelea kuomba msamaha.

Naombeni ushauri wenu

Cleofa
Kuna makosa mengine huacha makovu moyoni kwa mfano mpenzi wako kuchepuka hii sio rahisi kuisahau hata kama utasamehe.

Kwa ufupi kama ulisamehewa, kwa sasa inawezekana umeanza kuonyesha tabia zinazofanana na lile kosa ulilomtendea, au pengine una vioja ambavyo jamaa amevichoka na ametafuta mtu mpya kimya kimya.

Sitaki kusema kwamba jamaa hakupendi, ila nasema mapenzi yake kwako yamepungua.

ushauri wangu

Endelea kupima upepo kwanza, ukiona hali ni hiyo hiyo omba meza ya mazungumzo na jamaa ikishindikana jaribu kupitia rafiki yake wa karibu au ndugu yake, mueleze ukweli amshauri jamaa.

Ukikwama katika hatua zote hizo basi sidhani kama kuna option tena, let it go.
 
Last edited by a moderator:
na ametafuta mtu mpya kimya kimya.

Cha kufanya na wewe mkuu Cleofa nitafute mimi kimya kimya. Ukishanipata utamsahau hautamsumbua which means baada ya muda ni lazima ataku-Miss atakutafuta tu. Ukiendelea kumfuatilia hawezi kuku-Miss.

Mkuu Cleofa, karibu PM tafadhali.
 
Last edited by a moderator:
achana nae huyo..sio mtu wa kusamehe..atakuwa anatumia hilo kosa kama fimbo ya kukuchapia...kila mara atakuwa analikumbushia..na uenda ameshakuchoka au amepata kipozeo nje ndo mana anakulitea masinema..toka nduki
 
Kama alikwambia amekusamehe halafu miaka miwili baadae anarudisha kesi ile ile..means hajakusamehe na hutakaa kwa amani coz atakuwa anaifanya ndio sababu mara kwa mara, Mie ningebwaga manyanga, watu wa vinyongo ni stress tupu.
 
Shosti ningekua wewe ningetulia,kama kujishusha umejishusha vyakutosha,kama yeye mwanamme na wewe pia una hadhi yako ya kike,tulia usimtafute shughulika na mambo yako mengine kama anajua thamani yako atarejea ...
 
inaonesha ulifanya kosa kubwa. kosa kubwa la kumfanya mwenzi wako asisahau linajulikana. tafuta maraya mwenzio. umeandika unafupishafupisha thrd yako haina mvuto
 
achana nae...hajakusamehe na without tht kusonga mbele kwenu kutakuwa shida,mnapotezeana mda..ila kama vpi ongeeni tena na dada mtu (mediator wenu)..ila mh,ulifanya kosa gani mtu hajakusamehe mwaka mzima??!!..ila inaonekana kama kakuchoka vileeee
 
Habari wana Jf,

Nlimkosea mpenzi wangu ni muda sisi umepita nilikiri kosa na kuomba msamaha nikimshirikisha mpaka dadayake wiifi angu badae alikubali msamaha wangu mambo yakaisha.

Mwaka mmoja baadae ghafla alibadilika nikimtmia sms hajibu nukimpigia hapokei, nikamtumia sms vipi mbona kimya hata ukikuta missed call hunitafuti?

Alichojibu ni yale yale ya mwaka juzi ndio mana ipo ivo, je ana mapenzi tena na mimi? Kuna sababu ya mimi kuendelea kuomba msamaha.

Naombeni ushauri wenu

Mkuu hapo penye red nadhani tatizo lilianzia hapo, maana nilichokiona hapo ni kwamba ulimuomba msamaha hakusamehe ndipo ulipoamua kumshirikisha huyo mtu, ndio akakubali, hilo ni tatizo, hakuwa tayali yeye binafsi kusamehe, ila alisamehe kwa shinikizo na pengine kwa kuwaheshimu hao watu tu ili labda asiwauzi.

Jaribu kumtafuta na mkae chini nyinyi wawili tu, muulize kwanini ameamua kufanya hivyo na uombe msamaha tena, ila ukiona dalili ni mbaya piga moyo konde na uendelee na maisha yako, maana kama ameshampata mzuri zaidi yako sijui. Inauma ila pole.
 
Ulifanya kosa gani? Kama ulicheat halafu ukakiri hapo umeliwa mama.hawezi kuisamehe hiyo.
 
hicho ni kibuti cha kimya kimya.....anza tu maisha mapya.....
 
Habari wana Jf,

Nlimkosea mpenzi wangu ni muda sisi umepita nilikiri kosa na kuomba msamaha nikimshirikisha mpaka dadayake wiifi angu badae alikubali msamaha wangu mambo yakaisha.

Mwaka mmoja baadae ghafla alibadilika nikimtmia sms hajibu nukimpigia hapokei, nikamtumia sms vipi mbona kimya hata ukikuta missed call hunitafuti?

Alichojibu ni yale yale ya mwaka juzi ndio mana ipo ivo, je ana mapenzi tena na mimi? Kuna sababu ya mimi kuendelea kuomba msamaha.

Naombeni ushauri wenu

Close the chapter mydear ashakuacha kidhungu! sikuhizi hatuongeagi matendo ukisoma mchezo unajiongeza na wewe unachukua hatua.
 
Back
Top Bottom