Mbio za mwenge kitaifa

Charles Gerald

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2016
Posts
1,405
Reaction score
1,848
Jamani nipo hapa maeneo ya kwimba kwenye mapokezi ya mbio za mwenge kitaifa. Mwenge unakuja unapita sekondari moja ya kata. Sasa shida ni kwamba wanafunzi wote wa primary kutoka shule zote za kata wameletwa hapa, shule zingine ziko mbali. Naona sio sawa ukizingatia huu mwenge unakaa muda mfupi sana then vitoto hivi vigeuze kwa miguu tena kurudi majumbani. Hawa watoto wanapaswa kuachwa kuwasumbua kwa mambo ambayo hayana maana kwao.
 
Je, bila hao wanafunzi ni nani ataujaza uwanja...?

Kwanza weka picha, acha porojo.
 
Mwenge umepoteza uhalisia na dhamira
Wanasiasa wanautumia kujipatia umaarufu.
 
Hapo watoto wa Feza Boys huwezi kuwakuta.
Ulipita shinyanga mjini pia, ilikuwa jmosi. Watoto wote wa shule za serikali sekondari na msingi walienda kuusubiri na kuupokea ila wale wa private hakuwepo ht mmoja.
 
Ulipita shinyanga mjini pia, ilikuwa jmosi. Watoto wote wa shule za serikali sekondari na msingi walienda kuusubiri na kuupokea ila wale wa private hakuwepo ht mmoja.
Watoto wa wapiga kura ndiyo wanahusishwa na shughuli hizi si watoto wa wapigiwa kura
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…