laskaboza
Senior Member
- Jun 8, 2020
- 144
- 1,601
1. Kama unahitaji mchango (donations) wa jambo lolote, EPUKA kuuliza watu kama wangependa kukuchangia au lah na BADALA YAKE waulize kama wangependa kuchangia elfu 5 au elfu 10 (hicho kiasi ni mfano tu, unaweza ukaweka kiasi kulingana na uzito wa mchango wako) . Kwa mbinu hii itawafanya watu wengi sana wakuchangie!
2. Kama unataka mtu akusaidie kufanya kazi za nyumbani (chores) EPUKA kuwauliza kama wanaweza kufanya hizo kazi na BADALA YAKE waulize kama wataosha vyombo au kupika au kudeki. Kwa mbinu hii ni ngumu sana mtu kukwepa kukusaidia kufanya kazi za nyumbani.
3. Kama unataka kumshawishi mgonjwa ale mboga za majani au matunda EPUKA kumuuliza kama anajiskia vizuri kula na BADALA YAKE muulize umuwekee vijiko vingapi vya mboga au matunda. Kwa mbinu hii ni ngumu sana mgonjwa kugoma kula.
4. Kama unaongea na mtu ambaye ni mgumu kutoa maelezo mengi yanayojitosheleza, ukimuuliza swali na akawa hajatoa maelezo yote EPUKA kurukia kwenye swali lingine na BADALA YAKE kaa kimya kidogo baada ya sekunde kadhaa lazima huyo mtu atalazimika kuendelea kuongea kwa sababu atahisi maelezo yake hayajakamilika.
Je, wewe huwa unatumia mbinu gani kushawishi watu kufanya jambo fulani?