Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,535
Mwandishi Kagure Mugo wa Kenya aliwahi kuandika- “Nyumba ndogo, wanawake wa pembeni na ndoa za wake wengi huwasukuma wanawake kufikiria mbinu za kuongeza ubora katika via vyao vya uzazi ili kuwatuliza wanaume”.
Duniani kote wanawake wanapambana kujiweka vizuri, wengine wamefikia hatua ya kufanya upasuaji ili kuyafanya maumbile hayo yasiwe legelege.
Ingawa njia za kurudisha maumbile zimekuwapo kwa miaka mingi, hivi sasa imekuwa biashara nzuri inayowaingizia kipato walioamua kuwekeza huko kutokana na kushamiri kwa matumizi yake nchini.
Hivi sasa nchini ili kuzipata dawa hizo unaweza kubonyeza namba katika simu yako na ndani ya dakika 15 unachokihitaji kikawa nje ya mlango wako.
Mitaani ipo misemo kuwa adui wa mwanamke ni mwanamke. Katika hili wanawake wameungana na kuhamasishana kutumia dawa hizo, huku kila mmoja akitoa ushuhuda wake namna ilivyomsaidia kudumisha ndoa.
Mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika kwa kiasi kikubwa kunadi viungo hivyo na wauzaji wamekuwa wakiwaaminisha wanawake kuwa vinaongeza ladha kwenye mapenzi.
“Nani asiyejua habari ya kistic hapa mjini? Kistic ndiyo habari ya mjini na mkombozi wa akina dada...mbali ya kutibu magonjwa kadhaa pia kinapangilia siku zako za hedhi kama zilikuwa zinajichanganya pia kukausha maji ukeni na kuongeza joto la hatari.
Pia hiki kistic kinakuletea heshima kwa mpenzi wako kwani hutaki kutolewa ‘out’ Dubai, kujengewa nyumba au kumwagiwa madola? Halima Yusuph (siyo jina halisi) ni miongoni mwa wanawake waliotumia kiungo hiki akisema: “Baada ya kutumia mpenzi wangu huwa anaweweseka kuliko kawaida mpaka anataka nihamie nyumbani kwake.”
Mwandishi aliwasiliana na mmoja wa wauzaji wa viungo hivyo hasa biashara yake ikiwa ni kifaa kiitwacho madura stick chenye umbo linalofanana na soseji ambacho huingizwa ukeni muda mfupi kabla ya kufanya tendo la ndoa.
Mwandishi: Haloo habari yako
Muuzaji: Nzuri tu nani mwenzangu
Mwandishi: Mimi mteja nimepitia ukurasa wako Instagram nimeona mambo mazuri nikaona niwasiliane na wewe hebu niambie nakupata wapi nataka hiyo madura stick.Muuzaji: Wewe sema unapatikana wapi utaletewa ulipo.
Mwandishi: Nipo Kinyerezi
Muuzaji:Tuwasiliane kesho maana leo muda umeshaenda.
Mwandishi: Hebu shosti nitoe ushamba hiyo madura stick naitumiaje na inadumu kwa muda gani.
Kwa mujibu wa muuzaji huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kiungo hicho kina uwezo wa kudumu kwa miezi mitatu hadi minne.
Muuzaji: Kipo kama chaki unavyokiingiza kinayeyuka kidogokidogo unaweka kwa muda mfupi, unatoa na kukifuta kwa pamba kisha unakihifadhi kwa matumizi ya baadaye. Kuisha kwake kunategemea na kadri kitakavyoyeyuka kikiwa ukeni.
Katikati ya Jiji la Dar es Salaam yupo mwanamume maarufu ‘Babu wa Kisomali’ ambaye huuza bidhaa mbalimbali ikiwamo vilivyopo pichani.
Mwanamume huyu huuza vifaa mbalimbali vyenye majina ya kuvutia ambayo kwa sababu za kimaadili hayawezi kuandikwa.
Baadhi ya bidhaa hizi huzinadi kuwa zinapunguza majimaji, kuleta joto na kuongeza hamu ya tendo la ndoa.
Kungwi
Mwandishi alizungumza na kungwi maarufu jijini Dar es Salaam alikiri kuwa na wateja wengi wanaonunua bidhaa hiyo kwa sasa.
Alisema wateja wake wakubwa ni wasichana wasio na ndoa ambao hufika katika maskani yake kwa ajili ya kufundwa na baadaye hununua bidhaa hiyo.
Akielezea zaidi kuhusu viungo hivyo, kungwi huyo alisema hutengeneza kwa kuchanganya asali, majani ya mbaazi na binzari nyembamba.
Alipoulizwa iwapo vina madhara yoyote kwa mtumiaji, kungwi huyo alisema hakuna madhara kwa mtumiaji: “Havina madhara yoyote kwa sababu vitu vyote ninavyochanganya ni vya asili, kwa hiyo havina madhara yoyote.” “Lakini unapokiweka lazima uvae pedi ya kawaida kwa sababu kinakuwa kinavuta ule ute mweupe na majimaji kwa hiyo unakuwa na vitu vitakavyokulazimu ujikinge. Mtu anapotumia bidhaa hii viungo vyake vinakuwa vizuri na akikutana na mtu anapata ladha tofauti,” anasema kungwi huyo.
Alipoulizwa kuhusu viungo hivyo kudaiwa kuambukiza magonjwa kama saratani, kungwi huyo anasema hatumii shabu kwani hiyo ndiyo yenye madhara, kwake anaogopa kuwadhuru wateja wake, huku akitoa ushuhuda kwamba aliwahi kuugua saratani ya matiti hivyo anajua chungu ya ugonjwa huo.
“Haviwezi kukuharibu kwa sababu mimi sitii shabu, mimi naogopa mwenyewe nina saratani kwa hiyo sitaki kumuumiza mtu mwingine.”
Alipoulizwa kuhusu gharama yake kungwi anasema: “Nauza kwa gharama ya Sh5,000 kwa kimoja kwa hiyo mtu akitaka kununua ni Sh25,000 lazima achukue vitano na unaweza kuvitumia hata miezi sita haviharibiki.”
Kungwi mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Aunty Sophy anasema amekuwa na wateja wengi kwa kutengeneza viungo ambavyo vinaungwa kwa vitu mbalimbali ikiwamo shabu.
Alipoulizwa iwapo shabu ina madhara anasema wengi waliowahi kutumia hawajawahi kurudi kwake kudai kudhurika.
“Unajua shabu ina kazi yake, mabinti wengi wananunua viungo hivi kwa kuwa wanataka kuonekana wapya kwa wapenzi wao na ndiyo maana wanatumia shabu ambayo imechanganywa na viungo vingine, pia kama anakuja mteja ambaye hataki shabu pia anauziwa,” anasema Sophy.
Nini madhara yake kiafya
Mtaalamu wa magonjwa ya wanawake Dk Elias Kweyamba anasema matumizi ya dawa hizo yanaweza kuleta athari mtumiaji kutokana na kemikali zinazotumika kutengeneza kiungo husika kinachowekwa ukeni.
“Ukeni kuna bakteria ambao hufanya kazi ya kulinda uke dhidi ya maambukizi unapotumbukiza vitu vyenye kemikali unawaua na endapo watakufa basi unajiweka kwenye hatari ya kushambuliwa na kutokwa na uchafu usiokoma,” alisema.
Dk Kweyamba aliongeza kuwa uwepo wa bakteria hao walinzi husababisha uke kuwa na majimaji hivyo matumizi ya kemikali hizo husababisha kuondoka au kuongezeka kwa maji hayo.
“Maji yakipungua ni rahisi kwa mwanamke kupata michubuko wakati wa tendo na endapo yataongezeka basi unakuwa katika hatari ya kupata maambukizi.
Kwa ujumla kuweka viungo au kemikali ukeni kunaweza kubadilisha kinga halisi ya eneo hilo na kurahisisha kupata magonjwa kwenye mfumo wa uzazi na ugumba,” alisema Dk Kweyamba.
Chanzo: Mwananchi