Mbinu za kusugua meno ya watoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbinu za kusugua meno ya watoto

Discussion in 'JF Doctor' started by Kimbweka, Jul 19, 2012.

 1. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Watoto wenye meno nzuri hukua kuwa watu wazima wenye meno nzuri. Ukiwafunza watoto wako jinsi ya kusugua meno na kutoa uchafu katikati ya meno kwa kutumia uzi spesheli, isitoshe pia kuwapeleka kwa daktari wa meno mara mbili kwa mwaka watakua na meno nzuri na yenye afya
  Hata kama meno ya watoto wako itangÂ’oka kisha mengine yamee ni muhimu sana kuyaweka yakiwa safi. Meno ya mtoto wako mchanga huwa katika sehemu muhimu ambazo meno mengine yatamea vizuri akiwa mtu mzima.
  Watoto wadogo:
  Watoto wako wanapaswa kujifunza kuhusu utunzi bora wa meno kutoka kwako kwa mfano mwema kwa kusugua meno, kuondoa mabaki ya vyakula kwenye meno kwa kutumia uzi spesheli. Wasaidie kusugua na kuondoa vyakula kwenye meno hadi wafikishe umri wa miaka 7 ama 8 ambapo wanaweza kutekeleza wenyewe. Hapa pana njia zitakazoweza kukusaidia.

  • Tumia mswaki ya mtoto iliyo laini na utie kiasi kidogo cha dawa ya meno iliyo na floraidi
  • Fuata maagizo jinsi ya kusugua meno ya mtoto wako lakini tekeleza haya kwa upole
  • Hakikisha kuwa umesugua meno ya mtoto wako kwa dakika mbili
  • Hakikisha kuwa mtoto wako amesuuzia mdomo wake na kutema dawa ya meno. Usiwache waimeze
  • Usisahau kuondoa vyakula katikati ya meno kwa kutumia uzi spesheli.
  Hakikisha kuwa mtoto wako anatekeleza tabia hizi njema. Usiwaache wanywe vinyaji vingi baridi au vinyaji vya sukari. Hapa kwa wingi tunamaanisha zaidid ya moja kwa siku. Epukana na tabia ya kumpa mtoto wako vinyaji baridi na vyakula. Haya waweza kufanya mara moja tu. Unywaji wa vinyaji baridi ni mbaya kwa meno ya mtoto wako na ukuaji wake.
   
Loading...