MBINU ZA KUKUZA UDADISI KWA WANAFUNZI

MMASSY

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
290
193
Mara nyingi tumesikia watu wakilaumu mtalaa wetu kwamba unafunga fahamu za wanafunzi wetu. Wenye madai haya wanafikiri bila mtalaa kufanyiwa marekebisho makubwa, haiwezekani elimu yetu ikamnufaisha mwanafunzi. Hata hivyo, tulisema wiki iliyopita, kazi ya mtalaa ni kutoa dira ya jumla ya aina ya raia wanaotarajiwa kufundwa kupitia mtalaa husika.
Mwalimu ndiye mwenye kazi kubwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaelewa kile kinachokusudiwa kufikiwa na mtalaa. Katika makala haya ninalenga kuonesha namna gani mwalimu aliyefuzu anaweza kutumia mtalaa huu unaolalamikiwa kujenga tabia ya udadisi kwa wanafunzi wake.
Ningependa nitumie mfano wa Shirika letu liitwalo Holy Hands Book Project. Shirika hili linaendesha huduma ya kushauri wanafunzi na walimu(Student Cousling Service) ambapo kimsingi unajaribu kuwasaidia wanafunzi na walimu pia mbinu kadhaa za kufaulu mitihani.Mwalimu anafundishwa mbinu kadha wa kadha za kumfundisha mwanafunzi na mwanafunzianafundishwa mbinu kadha wa kadha za kusoma na kujibu mitihani yake ili mwisho aweze kufaulu vyema mitihani yake.
Mradi huu unatumia kanuni kuu tano ambazo naamini mwalimu yeyote anaweza kuzitumia.
Kwanza, kuhakikisha kuwa mwanafunzi anaelewa kwa nini anahitaji kujifunza kile anachojifunza. Hili kwa hakika limekuwa changamoto ya ufundishaji wa kimazoea.
Tumekuwa tukifundishwa maudhui ambayo kwa kweli hatuelewi tutayatumia wapi. Nakumbuka kwa mfano, nikiwa kidato cha 3 kwenye somo la Fizikia tulifundishwa hesabu ndefu za namna ya kutafuta muda utakaotumiwa na tone la mwisho kudondoka kwenye bomba la maji linalofungwa.
Hatukuelewa kwa nini ilikuwa ni lazima kusumbua akili kufanya hesabu hizi ngumu zisizotatua tatizo lolote kwenye maisha yetu. Ufundishaji wa namna hii, kwa hakika, unamkatisha tamaa mwanafunzi. Mwanafunzi asiyeelewa kwa nini anasoma kitu hawezi kuwa na udadisi
Kupitia mfumo wetu wa ujifunzaji, HHBP tunajaribu kufikiri namna gani kile kinachofundishwa kinagusa maisha ya kawaida ya mwanafunzi. Kujua uhusiano wa maudhui na maisha yake kunamwongezea mwanafunzi ari ya kujifunza kwa sababu anaelewa thamani ya kile anachotarajiwa kujifunza.
Mwalimu anapata somo muhimu hapa. Kwamba ni muhimu atafute namna ya kuhusianisha somo lake na maisha ya mwanafunzi. Kwa mfano, mwalimu wa Kemia anapofundisha somo la Mada (matter) anahitaji kufanya kazi ya ziada kumsisimua mwanafunzi kuona namna maarifa ya mada yanavyoweza kumsaidia katika maisha yake ya kila siku. Kazi hii haifanywi na mtalaa bali mwalimu.

Kanuni ya pili inayotumiwa na HHBP, ni kuhakikisha mwanafunzi anajenga uwezo wa kujiuliza maswali ya msingi kuhusu hicho anachojifunza badala ya kutegemea majibu yaliyopikwa na mwalimu anayeonekana kuwa mjuzi na mmiliki wa maarifa.
Kwa hakika madarasa yetu yanafanya kinyume. Kazi ya walimu imekuwa ni ‘kuhubiri’ maarifa kwa mwanafunzi. Mwanafunzi anachukuliwa kama mtu anayesubiri kupikiwa kila kitu na kazi yake ni ‘kumeza’ kile anachoambiwa. Hana fursa ya kuuliza wala kuhoji.
Shule zetu ‘zinazofaulisha sana’ kimsingi zinajitahidi kuhakikisha mwanafunzi anafahamu kwa hakika nini cha kukariri. Walimu wa shule hizi wanafanya bidii kubwa kuwaimbisha wanafunzi kile wanachojua kitaulizwa kwenye mtihani.
Somo tunalopewa na Holy Hands Book Project ni kwamba mwanafunzi anayewekewa mazingira ya kujiuliza maswali na kushiriki moja kwa moja katika kutafuta majibu, anakuwa na uwezo wa kudadisi kuliko mwenzake anayeshiriki ‘kumeza’ maarifa.
Mwalimu lazima afanye kazi kubwa ya kuibua maswali yanayohusiana na kile anachokifundisha ili wanafunzi waweze kujifunza kwa mfumo wa kutafuta majibu wao wenyewe. Mradi wa HHBP unatuthibitishia kuwa mwalimu akiwezeshwa anaweza kutafsiri mtalaa huu unaodaiwa kuwa haufai kuibua kiu ya kutafuta majibu.
Kanuni ya tatu ni kumtarajia mwanafunzi kutumia maarifa yake kutengeneza ujuzi. Mwanafunzi wa HHBP si tu anahitajika kujibu maswali ya kufikirisha, bali kuonesha ujuzi mahususi. Mathalani, baada ya mwanafunzi kujifunza namna mimea inavyotengeneza sukari kwa kutumia mwanga wa jua, lazima aoneshe anavyoweza kutumia maarifa hayo kutatua matatizo katika mazingira yake………..Endelea kutufuatilia kupitia facebook page yetu ya Holy Hands Book Project like na uendelee kujisomea zaidi mbinu kadha wa kadha.Pia tupigie au tuandikie sms tukupatie nakala ya kitabu chetu cha Mbinu na mikakati ya kusoma na kuelewa unachokisoma,mbinu za kukumbuka kile ulichokisona,namna ya kujiandaa na mtihani na mikakat ya kujibu mtihani utoke na matokeo mazuri.
Tunatoa huduma za kuhamaisha wanafunzi njia bora za kusoma na kuelewa masomo yao na mbinu za ufaulu wa mitihani kwa wanafunzi wa ngazi zote.Tupigie kupitia namba zetu za simu 0758673441 tukuhudumie

JEROME MMASSY
Mkurugenzi mtendaji
Holy Hands Book Project
 
Hongereni sana mpo vizuri na nimependa jinsi mnavyotumia njia ya kurithisha maarifa/ elimu kutoka kwa Mwalimu kwenda kwa mwanafunzi. Kwa hakika mmelenga wahusika wote.

Vipi, mna namna nyengine yoyote ya kujitangaza zaidi kama kwenye radio, tv n.k ili jamii ifahamu kwamba kuna kitu kama hiki hapa nchini mwetu? Nakumbuka jamaa wa kitabu cha Visa na Mikasa ya Kesi Maarufu Duniani na Hukumu zake, alipojitangaza kwenye radio kubwa hizi soko lake likawa kubwa na akafahamika.

Vipi kuhusu ninyi?
 
Hongereni sana mpo vizuri na nimependa jinsi mnavyotumia njia ya kurithisha maarifa/ elimu kutoka kwa Mwalimu kwenda kwa mwanafunzi. Kwa hakika mmelenga wahusika wote.

Vipi, mna namna nyengine yoyote ya kujitangaza zaidi kama kwenye radio, tv n.k ili jamii ifahamu kwamba kuna kitu kama hiki hapa nchini mwetu? Nakumbuka jamaa wa kitabu cha Visa na Mikasa ya Kesi Maarufu Duniani na Hukumu zake, alipojitangaza kwenye radio kubwa hizi soko lake likawa kubwa na akafahamika.

Vipi kuhusu ninyi?
Ahsante sana kwa ushauri,kwa sasa hatujawa na accesss na radio za mbali bali tumetumia local radio stations zilizoko Arusha.Tutaendelea kuwafikia wengi zaidi kwa kujitangaza via Tv stations na radio nyingi kama ulivyoshauri mkuu.Unaweza kutupta pia katika mtandao wa face book kwa jina la Holy Hands Book Project, Instagram kwa jina la holyhands_bookproject.
 
Ahsante sana kwa ushauri,kwa sasa hatujawa na accesss na radio za mbali bali tumetumia local radio stations zilizoko Arusha.Tutaendelea kuwafikia wengi zaidi kwa kujitangaza via Tv stations na radio nyingi kama ulivyoshauri mkuu.Unaweza kutupta pia katika mtandao wa face book kwa jina la Holy Hands Book Project, Instagram kwa jina la holyhands_bookproject.
Ahsante sana, natumai dhamira yenu itazaa matunda chanya na inaweza ikawa ni chachu vilevile kwenye gurudumu la elimu kwa hapa Tanzania.
 
Back
Top Bottom