Mbinu ya kutafuta mke sahihi.

Mbinu ya kutafuta mke sahihi.

b wence

Senior Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
154
Reaction score
108
Habari wakuu poleni kwa majukumu ya kutwa nzima,natumai mko poa..

Twende kwenye mada.nimekaa na kufikiri na nikagundua kitu na nikaona si vby nikashea na wandugu ili nililolipata..

Hapa nazungumzia mbinu niliyoiona kuwa iko sahihi kwenye mchakato wa kupata "mke sahihi" namaanisha mke na simaanishi "demu sahihi"....

Ni kuwa hupaswi kumpenda yule uliyemkusudia kumfanya awe mke wako..yaani mapenzi yasikuchagulie mke..KWANN?...Kwa sabb nimegundua wengi walikuja kulalamika baadae au kuja kuona kuwa walikosea kuchagua,kwa sabb walitangulia kupenda kwanza.kwa kawaida mapenzi hukufanya kuwa kipofu,huwezi kuona kasoro za unayemchunguza..na kwa sabb umependa basi kila utakachokiona kwake utakiona ni sahihi tuu..

Fanya ivi,nenda km wale wazee wa zamani,ambao kwanza walioa kisha wakaja kupenda baada ya kuoa.yaani yale matokeo baada ya kuoa ndiyo yatakayokufanya umpende.na ndio mana ndoa zilidumu...siku hz tunaanza kupendana kwanza,hatuoni kasoro,baadae ndio tunagundua kumbe hayuko vile tuliovyoona au kudhania mwanzoni,kwa sabb mapenzi ni upofu mkubwa..

Hivo nahasa usiruhusu upendo ukuchagulie mke..

Ukichunguza kwa umakini mtu anaweza kuwa na mademu wazuri sn kwa nje lkn kwenye kuoa akaja kuoa mwanamke wa kawaida kimuonekano wa nje..vipo vya kuangalia ndani.wife material aangaliwi km ana wowowo kiasi gn,au ni mrembo kiasi gn,basi zile tabia za mke anazo? Je ana umama ndani? Je ana uwezo wa kubeba majukumu km mama?..

Asanteni ndugu zangu..
 
Back
Top Bottom