Michael Chairman
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 922
- 588
Mazungumzo magumu si jambo rahisi , moja ya jambo linalowatatiza wengi sana kwenye maisha ya kila siku na kama hauna mbinu dhidi ya mazungumzo magumu yanaweza yasikuache salama kihisia na kiakili, nchini kwetu kwa sasa tunaye Rais ambaye utashi wake mkubwa ni kuona mambo yanakwenda na kama kuna namna wewe unasababisha mambo yasiende , kwenye mkutano wake na wazee wa Dar es saalam alisema watu hao atawabomoa, sasa huenda ikawa kesho kwako maana Rais Magufuli ni mtu wa kazi anaweza kutua kwako kwenye eneo la kazi ama kwenye Gemba zake (maeneo ya ofisi za serikali).
jaribu kupitia mbinu hizi rahisi zikusaidie kuzungumza naye Mhe Rais
Mosi, Kuwa na maandalizi muda wote.
Kuwa na maandalizi kwenye uga wa maeneo yako ya kazi juu ya masuala nyeti yatayaoulizwa ni rahisi sana kuwa na mazungumzo mazuri na Mh, Rais na unaweza kutoka salama kabisa ukiwa mwenye furaha , muhimu kukumbuka maandalizi hayo yatie ndani kuwa na taarifa sahihi na z kweli maana huyu mzee amekuwepo site kwa kipindi kirefu sana kwahivyo anafahamu vyema sana kinachoweza kuendelea eneo lako la kazi na moja ya mbinu anayoitumia na kutokana na watu unaofanya nao kazi, kuwa na maandalizi kutakufanya uwe na nafasi nzuri.
Pili, Baini mambo yanayo kupatia hamasa kwenye mazungumzo.
Kufahamu hamasa zako zinazo kusukuma wewe kuzungumza kwa uzuri kwenye mazungumzo yako na Mh Rais kutakusaidia kuwa mwenye kujiamini lakini hakikisha kuwa pia unalinda hamasa ya Mh Rais kuzungumza nawe, mara nyingi yeye ni muumini wa ukweli na anapenda sana ukweli unazpozungmzwa na hiyo ni hamasa yake jaribu kuilinda na usitoke nje ya hapo na hata kama unatoka toka lakini endelea kuhifadhi hamasa yake, usije ukamuondoa kwenye hamasa yake ya kutaka ukweli.
Tatu, uwe na hoja (fact).
moja ya jambo linalompatia burudani Rais Magufuli akiwa anakusikiliza ni kuwa na hoja (fact), eneo hili unawajibika uwe mzuri kwenye kuwa na hoja na takwimu zinazo hitajiwa na yeye ,kuwa na takwimu za kifedha, idadi ya vitu , idadi ya watu ,majengo ,tarehe, baada ya kuwa na hoja basi hakikisha kuwa unakuwa na mifano inayokusaidia kumfanya amini na ziwe zenye mashiko na hakikisha upo tayari kuzitetea hoja zako badala ya kujibu hapana na ndiyo tu , ukifanya hivyo hapo ndiyo utakuwa umeupata moyo na furaha ya Rais.
Nne , usimkosoe , kumlalamikia , kumhukumu bali msifie.
mwandishi wa kitabu muhimu sana cha kuwa na mahusiano bora na watu ndugu Dale Carnigie anasema kwenye kitabu chake hicho kliitwacho how to win friends and influence people , mambo hayo juu ni ya kutiliwa mkazo sana unapokuwa kwenye mazungumzo ya aina yoyote huenda na si na Rais Magufuli imeonekana hata marekani kwa Rais Trump ambaye hivi majuzi amewambia wanaomkosoa waende makwao , hakuna anayependa kukosolewa na hata kama unataka kukosoa kwa njia bora ya kuanza kueleza makosa ya kwanza.