Mbinu kampuni katika uendeshaji wa shughuli za kisiasa.

Mbinu kampuni katika uendeshaji wa shughuli za kisiasa.

TUNTEMEKE

Platinum Member
Joined
Jun 15, 2009
Posts
4,587
Reaction score
580
Uzima ni jambo la msingi ambalo sote tuliobahatika kuwa nao hatuna budi kumshukuru Mwenyez Mungu kwa kutupatia bure,kwa heshma kabisa pia yatupasa kuwaombea ndugu zetu wote walio hai lakini wanateseka kwa maradhi mbalimbali hapa ulimwenguni.Niwapongeze vijana wote waliopo maeneo mbalimbali wakifanya kazi kwa minajili ya kujiletea maendeleo.Msiokuwa na ajira msikate tamaa,zidisha bidii katika kutafuta mbinu mbadala na stahiki katika kukabiliana na changamoto za maisha na hatimae Mungu atafungua milango siku mojaNikirudi kwa mada kuu,ni budi akafaham maana ya KAMPUNI na CHAMA CHA SIASA na pia utofauti katika uendeshaji baina ya hivi vitu viwili.Ni kianza na maana ya neno kampuni,ni muungano wa watu wawili au zaidi wenye nia na makubaliano ya pamoja ya kutaka kufanya biashara ili waweze kutengeneza na pia kupata faida.Ili kupata wateja,kampuni inalazimika kufanya kila lililo ndani ya uwezo wake ikiwa ni pamoja na kutangaza bidhaa zake.Kampuni makini inayoendana na wakati haina budi kutumia teknolojia ya hali ya juu sana katika uzalishaji wa bidhaa zake.Matokeo hasi yanayotokana na matumizi ya teknolojia ya juu,ni kwamba wanyakazi hupoteza ajira kwa sababu ya matumizi ya vifaa ambavyo hufanya kazi mda mrefu bila kuhitaji nguvu ya binadam,mfano kazi ambayo pengine ingeweza kufanywa na watu zaidi ya kumi,kwa sababu ya tecnolojia ya kisasa,inaweza ikafanywa na mtu mmoja tu,hivyo kampuni inalazimika KUFUKUZA au KUPUNGUZA watendaji wake ili kutengeneza faida zaidi,otoshe tu kusema lengo kuu la KAMPUNI ni kupata faida hasa ya kifedha na si kutoa huduma kwa wananchi ili kuwasaidia kuondokana na dhiki,hii ndio kampuni.Lakini tofauti kabisa na CHAMA CHA SIASA ambacho maana halisi ni kikundi cha watu wenye lengo moja na waliojiunga pamoja kwa lengo la kushika dola na hatimae kuongoza serikali.Ni takribani miongo miwili sasa tangu Tanzania irudie na kuanza kufata mfumo wa vyama vingi.Kuna faida nyingi sana tumezipata kutokana na kuwepo kwa mfumo huu wa vyama vingi ikiwemo kukua kwa demokrasia,uhuru wa kutoa maoni,uwazi na ukweli na hata maendeleo pia japo hayaendani na ongezeko la watu nchini.Pasi na shaka yoyote ni wazi kuwa kuibuliwa kwa hoja mbalimbali na vyama vya upinzani kumechangia kwa kiasi kikubwa hofu ya ufujaji mali za umma na rasirimali za taifa letu kwa watendaji serikalini na baadhi ya wanasiasa,ni ukweli usiofichika kuwa hii imetokana na uwepo wa upinzani makini na wanasiasa wazalendo katika nchi yetu ambao wanastahili sifa na hatuna budi kuwaenzi.Umakini wa chama chochote kile cha siasa unapimwa na utendaji wake wa kila siku pamoja na sera nzuri za chama husika zenye lengo la kumkwamua mwananchi wa kawaida kutoka hali duni ya maisha pamoja na mikakati madhubuti ya matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo.Chama makini cha siasa hupimwa kwa kuwaonesha dira vijana ambao ndio nguzo ya mabadiliko..Tofauti kabisa na KAMPUNI ambayo wamiliki wake hulenga kupata faida na hivyo kulazimika kufukuza wafanyakazi wake ili iweze kuzalisha zaidi kwa kutumia mashine,CHAMA CHA SIASA MAKINI hujikita zaidi katika kutafuta wanachama ili kuungwa mkono na hatimae kuchukua dola kirahisi.Chama chenye viongozi makini hukijenga chama chao kwa uwezo mpana na busara katika kuepusha makundi,migogoro baina ya wanachama na viongozi,viongozi makini pia hupimwa kwa kutokubagua wanachama wake kwa misingi ya ukabila,udini,elimu pamwe na ukanda,chama makini hutatua matatizo yake na migogoro kwa busara na si kufukuza kama ifanyavyo kampuni,chama makini ni kama chuo chenye kutoa elimu na kuwaandaa vijana wake kuja kuwa viongozi makini na shupavu katika taifa lao,chama makini hufanya vijana wake wawe wazalendo na si waasi wa kuja kuingia msituni kwa visingizio vya kutafuta haki iliyopotea,chama makini huzalisha viongozi makini wenye kufata misingi ya haki na usawa,hukemea tabia nyemelezi za UKANDA,huenda mbali zaidi na kujikita kwenye hoja za msingi zenye kugusa maisha ya kila mmoja,ndani ya chama makini binadam wote ni sawa.Mwisho nawapongeza waasisi wote wa vyama vingi nchini kwani uhuru wa mawazo tulionao leo ni kwa sababu yenu,lakini pia nitoe rai kwa viongozi wa vyama vya siasa kutofautisha uendeshaji wa kampuni na vyama vyetu vya siasa..Mmbarikiwe sana!
 
Gwakisa, Mpiganaji jana nilikushauli kaa chini usome shule, umalize. Kijana uliyeonekana tegemeo la Chama leo umegeuka na kuona kila kitu kibaya.

Wewe hapo nyuma ulikuwa unasema wazi wazi kuwa tatizo la chama kuna mamluki wengi toka CCM na ukipendekeza uongozi uchukue hatua, na baazi ya hao mamluki ulio wasema leo ndio marafiki zako wakubwa, unataka kutuambia na wewe umekuwa maaluki? Najua wale viongozi ulio wasema mamluki Katibu Mkuu, baadhi aliwatoa katika Uongozi, sasa wewe ulitaka upewe zile post nini mdogo wangu.

Nakuomba tena tulia soma shule yako, pia angalia siyo kila uliye naye mnaongea pamoja mpo pamoja. uwe makini, walio makini hawakai katika kundi la kifo wanakaa katika kundi la ushindi.

Naomba uwaze kama mimi, hivi wangekupa uongozi wa BAVICHA ambao mpaka leo unajua wewe ulimshinda yule dada, leo ungeweza kusoma na kuwaongoza vijana wenzako.

Leo unasifika kwa kuiponda CHADEMA popote ulipo, jua jamii inakusoma kesho hauta aminika na yeyeote kuwa makini.

Uchambuzi wako hapo juu naona kama hauna mashiko kwa sababu unaongea kitu ambacho naamini hukiamini.


JUA UKOMBOZI WA HII NCHI UTAPATIKANA NA WENYE MOYO. Mimi ni mwananchi wa kawaida hata katibu mkuu na viongozi wengine hawanijui, nikupe taarifa kabisaa hata msemeje mabadiliko ni lazima
 
Bwana mdogo kama bado unafikiria kuendelea na siasa tulia. Makala yako najua imeilenga CDM, lakini ujue tu kuwa CDM na M4C yake ni mafuriko, hayazuiliki, na ole wake atakayejaribu kuyazuia kama unavyofanya wewe, utakwenda na maji.
 
Back
Top Bottom