Mbinu gani inaweza kutumika kumbadilisha mtoto anayeanza kuandika kutumia mkono wa kushoto?

Huwa mnanikeraaaaa shida iko wapi na ndo maumbile yake au ni venye dunia imetuamulia basi na wewe unaelekea t humo humo aisee siku mwanangu kaenda shue kashika kalamu na shoto wameanza kumbadilisha niliwazukia na kishindo cha wakoma bado kidogo nipige mtu nikawaambia muacheni na kula analia shoto tena mi mwenyewe kuna mda namuangalia natamani ningekua shoto
 
Wakuu ambao mshakutana na scenario kama hii kwa watoto kuna uwezekano wa kumbadilisha mapema
Mkuu,

Mimi ni left handed. Kipindi ninakua wazazi walikuwa wakinichapa nikitumia shoto kuandika.

Alikuja padri mmoja rafiki yake na baba akawakataza baba na mama waniache niendelee kutumia mkono wa kushoto.

Kwanini unataka kumkataza mtoto kutumia shoto?
 
Nilianza kugundua my third born kuwa ni left handed toka mapema sanaa. His left hand was energetic kuliko right one..hata kalikua kakikupiga na mkono wa kushoto ni tofaut na wa kulia. Akirusha mawe kwa left ni tofaut na kulia nikamwambia yf hapa tumezaa left handed, mama yake alipambana sana kutaka awe anatumia right hand alipoanza shule nikamkataza kuwa muache. Uzuri mimi ni left footed kwenye masuala ya kucheza mpira enz hizo so sikuona ajabu sana..

Kitu pekee nilichopambana nae sana ni kwenye ulaji wa chakula. Hapa ndio ilikua changamoto .alikua anajishau sana kula kwa kushoto hapa ndio nilipokua nagombana nae mpaka sasa amezoea. Anaandika kwa kushoto anacheza mpira kwa mguu wa kusho.

HAKUNA SHIDA YOYOTE MKUU hata usijali
 
Acha usijaribu kumbadirisha kitu ambacho yawezekana hufahamu watu wengi wanaoandikia shoto wanao uwezo wa kujifunza mkono wa kulia na wakaweza kuandika in short left handed huwa wana zaidi ya kuwa both handed lakini right hand huwa ni right hand forever hiyo kulia Wala usimfundisha nakuhakikishia utamwona baadae anaweza kunitumia yeye mwenyew japo sio kama kama ilivyo kushoto mm nna rafiki zangu wanaotumia mikono yote left&right japo left iko smart Sana.
 
Back
Top Bottom