Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
Rejea mada yangu juu ya vitu sita ambavyo havikuumbwa na MUNGU.
Vitu sita ambavyo si viumbe vya Mungu
Wakati wakichangia mada yangu juu vitu sita ambavyo Mungu hakuviumba, watu kadha wa kadha Jamii Forum, whatsapp na facebook walisema kuwa hoja zangu zilijielekeza kama vile kabla ya Mungu kuumba Dunia hakuumba vitu vingine.
Wamejenga hoja kwa kusema kuwa mwanzo sura ya kwanza yote ilikuwa makhususi kwaajili ya kuelezea jinsi Dunia ilivyo umbwa na si ulimwengu. Kabla ya kuumbwa Dunia, tayari ulimwengu ulikuwa ushaaumbwa, na kwasababu hiyo wanahitimisha kwa kusema KIZA ni sehemu ya ulimwengu na kiliumbwa kabla ya Dunia, na Kabla ya Nuru.
Awali ya yote, naelewa kuna galaxy zisizo pungua bilion 100, na kuna matirioni ya nyota. Najua fikra zao kuwa Mwanzo Sura ya kwanza inazungumzia uumbaji wa dunia na si uumbaji wa ulimwengu, kwa hivyo wanasema Kiza kiliumbwa siku nyingi kabla ya matukio yalihotajwa na mwanzo sura ya kwanza.
Kabla sijawajibu hoja zao, naomba tujiulize, kwa mujibu wa mwanzo 1:1 na kwa kuzingatia maandiko mengine ya biblia, Mbingu ni nini? na mbinguni wapi? Kisha tujiulize nch ni nini?
Mbingu ni neno la kiroho zaidi lenye maana ya anga.(space). Wana sayansi wanatumia neno "anga" wakati Mungu anatumia neno "mbingu". Kwa hivyo tukijua maana ya anga kwa vyovyote vile pia tutajua maana ya mbingu.
Anga ni eneo kubwa sana(three dimensional region) ambalo huanzia pale atmosphere inapoishia. Naomba mfahamu kuwa atmosphere ni moja kati ya matabaka ya dunia. Hii ina maanisha pale dunia inapoishia ndipo anga huanza. Kwasababu hiyo, ndio maana wanasayansi wanasema Dunia iko angani.
Anga ndio ulimwengu wenyewe, sababu vitu ambavyo vipo angani galaxy, nyota, sayari, vimondo, setelaiti, na nk ndio hufanya ulimwengu. Anga, ambayo kimsingi ndio ulimwengu umeundwa na vitu vifuatavyo.
1. Normal Matter
Ambayo ni asilimia tano ya ulimwengu wote. Galaxy, nyota, sayari, vimondo, na hata viumbe hai vimetokana na NORMAL MATTER.
2. Dark Energy
Ambayo yenyewe ni asilimia 25
3 Dark Matter
Ambayo yenyewe ni asilimia 70 ya ulimwengu wote.
Kwa hivyo nyota zote ziko angani, na nimesema hapo juu kuwa anga ndio mbingu. Kama wanasayansi wanasema nyota ziko angani, tujiulize Mungu anasema nyota ziko wapi?
"Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze"
Isaya 13:10
"Umeongeza wafanya biashara wako kuwa wengi kuliko nyota za mbinguni;...."
Nahumu 3:16
"katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni,..."
Mwanzo 22:17
"Ametukuka aliye zijaalia nyota mbinguni, na akajaalia humo taa na mwezi unao ng'ara."
Quran 25:61
"Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota."
Quran 37:6
Quran na biblia zote zinasema nyota ziko mbinguni, kama nyota ziko mbinguni kwa mujibu wa Mungu, na kama nyota pia ziko angani kwa mujibu wa sayansi, je nikisema kuwa MBINGU na ANGA ni kitu kimoja nitakosea? Kwa vyovyote vile sitakosea.
Kwahivyo naomba muelewe, mwanzo 1:1 iliposema Mungu aliziumba mbingu ilimaanisha Mungu aliuumba ULIMWENGU. Sababu tumeona mbingu ni mkusanyiko wa matirioni ya nyota na mifumo yake ambayo kwa pamoja hufanya ulimwengu.
Ukisoma astronomy jinsi inavyo zielezea nyota, hasa vile zilivyo undwa, utagundua hazikuanza tu kuwa na Nuru(Mwanga) na Joto kali, bali kuna mambo na michakato ilikuwa inafanyika, na matokeo ya mambo hayo ndio yakapelekea nyota kuwa na mwanga. Kwa hivyo Mungu aliposema iwe Nuru ndio aliruhusu michakato hiyo kuanza kufanya kazi na hatimaye tukapata jua. Lakini kabla ya NURU kuja kulikuwa na nini? jibu KIZA.
"Nchi" maana yake Dunia, lakini lazima tujue na kukubali kuwa kila nyota ina mfumo wake, na katika kila mfumo wa nyota una sayari zake, na kila sayari ina usiku na machana. Kwa hivyo Mungu aliposema iwe NURU, basi hapo hapo nyota zote ulimwenguni zikatoa Nuru au zikawa na uwezo wa kuwa na mwanga.
Kuna baadhi ya mambo yalifanyika maalum kwaajili ya sayari moja moja, lakini kuna baadhi ya mambo yalifanyika kwa sayari zote kwa ujumla. Kwa hivyo siku iliyoumbwa "mchana" katika sayari ya dunia, ndio siku iliyo umbwa mchana katika sayari zote za ulimwengu. Ninasema hili kutokana na sababu kubwa ifuatayo.
Mfumo wa Nyota Jua una jumla ya sayari nane, na dunia ni moja katia ya sayari hizo nane. Kwa hivyo kipindi Jua lilipopewa NURU, ile Nuru yake ilifika katika sayari zote nane. Pale Mungu aliposema Nuru ijitenge na giza, na giza liwe usiku na Nuru iwe mchana, tukio hilo lilitokea kwa Sayari zote. Kwasababu hiyo si kweli hata kidogo kuwa NURU na MCHANA uliotajwa katika mwanzo 1:3-5 ulikuwa makhususi kwaajili ya Sayari Dunia pekee.
Ili useme ile NURU ni makhususi kwaajili ya dunia tu, ni lazima utuambie Nuru hiyo imetoka katika Nyota gani tafauti na nyota jua. Sababu Nyota Jua ndio huangazia sayari zote katika mfumo wa Jua. Hivyo ni dhahiri kuwa wakati Jua lilipoanza kuangazia dunia ndio wakati huohuo lilipoangazia sayari zingine pia.
Mambo mkhususi ya Dunia katika mwanzo sura ya kwanza ni uumbaji wa mito, bahari, miti, wanyama, nk. Haya ndio yalikuwa makhususi kwaajili ya Dunia, na kila sayari ilikuwa na mambo yake makhususi kadiri ya Mungu mwenyewe alivyoona vema, ndio maana tabia na sifa za dunia ziko tafauti na sayari Zuhura, lakini zote zinategemea NURU ya Jua na zote zina usiku na mchana.
Kwa hivyo bado niko katika hoja yangu, kuwa Mungu aliposema kaumba mbingu alimaanisha kaumba ulimwengu. Akaumba Nuru kwa kulifanya jua litoe mwanga, lakini Mungu hakuumba Kiza, bali aliumba Nuru ili kukipiga KIZA, na kwasababu hiyo hakuna ushahidi Mungu akisema ameumba Kiza, hivyo basi KIZA KILIZUKA siku nyingi sana kabla ya kuumbwa kwa ilimwengu.
Njano5
Call/whatspp 0622845394