Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Ndege ya Kampuni ya Fast Jet imeshindwa kutua kwenye Uwanja wa Kimataifa Songwe nje kidogo ya jiji la Mbeya baada ya kuzidiwa na ukungu mzito ulioambatana na mvua.
Ndege hiyo ilitarajiwa kutua leo saa 2. 00 asubuhi, lakini ilipofika anga la jiji la Mbeya ilikumbana na ukungu ulioambatana na mvua kubwa ikinyesha
Kaimu meneja wa uwanja huo, Hamisi Amiri amesema Marubani wa ndege hiyo waliamua kurudi Dar es salaam na abiria ili kuepuka kufanya majaribio ya kutua jambo ambalo ni hatari
"Kwanza kulikuwa na mvua kubwa, halafu ukungu pamoja na mawingu yalitanda eneo la uwanja jambo ambalo lilisababisha Marubani washindwe kuona vizuri njia ya ndege licha ya kuwapo taa", alisema Amiri.
Chanzo: Mwananchi