Mbeya Kunani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbeya Kunani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Nov 26, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,470
  Trophy Points: 280
  Mbeya yaendelea kuwa gizani
  Merali Chawe, Mbeya
  Daily News; Tuesday,November 25, 2008 @21:15

  Mkoa wa Mbeya jana uliendelea kuwa katika giza totoro kwa siku ya tatu mfululizo, baada ya transfoma linalopokea umeme kutoka katika Gridi ya Taifa na kuusambaza mkoani hapa, kupata hitilafu Jumapili iliyopita.

  Kutokana na hitilafu hiyo ya umeme, shughuli za kiuchumi katika Mkoa wa Mbeya vikiwamo viwanda vidogo, mafundi mchundo, vinyozi, sehemu za mitandao zimekwama kuendelea na shughuli za kila siku na kusababisha wananchi wanaotegemea shughuli hizo kuwa katika hali ngumu kiuchumi.

  Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mbeya, Mhandisi Stella Hiza alisema katika kukabiliana na tatizo hilo, mafundi sita kutoka Dar es Salaam wamewasili hapa kuungana na mafundi wengine ili kukabiliana na tatizo hilo.

  Hata hivyo, alisema hawezi kusema ni lini tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi na kwamba wanajitahidi usiku na mchana katika kuhakikisha transfoma hiyo inatengenezwa na kuendelea kupokea umeme kutoka Gridi ya Taifa na kuwawezesha wananchi kuendelea kupata huduma kama kawaida. Baadhi ya wananchi walisema kukatika huko kwa umeme kusikokuwa na kikomo kumesababisha kukwama kwa shughuli za kiuchumi, na Tanesco wanatakiwa kuhahakikisha wanarejesha haraka huduma ya umeme.

  Katika taarifa yake juzi, Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud, alisema transfoma kubwa inayosambaza umeme kwa mkoa huo iliyopo katika kituo cha umeme cha Mwakibete, imeharibika ghafla Jumapili iliyopita. Alisema jitihada za kutengeneza transfoma hiyo zinafanywa kati ya Tanesco Makao Makuu na Mbeya, na kuwaomba radhi wananchi wote wa Mbeya kutokana na usumbufu unaojitokeza kutokana na tatizo hilo.
   
 2. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  JK analipiza kisasi :).
   
 3. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  yaani hakuna back-up ya aina yeyote? mhmm!!
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,470
  Trophy Points: 280
  Umeme wazidi kuleta kizaazaa Mbeya

  na Christopher Nyenyembe, Mbeya
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  KUKOSEKANA kwa umeme kwa siku nne mfululizo kumeufanya Mkoa wa Mbeya kuendelea kuwa gizani na kuwaongezea makali ya maisha wakazi wa mkoa huo, hususan ndani ya jiji hilo huku shughuli muhimu zikiwa zimesimama.

  Hali ikiwa hivyo, mmoja wa mainjinia wa TANESCO kutoka makao makuu, inadaiwa kuwa alirushwa na umeme kutoka kwenye transfoma iliyoharibika na kupopoteza fahamu. Alikimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mbeya ambako alipatiwa matibabu.

  Tukio hilo la kuanguka kwa mtaalamu huyo wa umeme aliyejulikana kwa jina moja la Mkweche, limekuwa gumzo jijini humo huku wananchi wa maeneo ya Mwanjelwa kwenye kitongoji maarufu, wamekuwa wakiyazomea magari ya TANESCO yanayopita hapo, kwa madai kuwa zote hizo ni hujuma na matunda ya mkataba mbovu wa umeme wa IPTL.

  Tanzania Daima imekuwa ikifuatilia kwa karibu malalamiko yanayotolewa na wananchi tangu mkoa huo kuwa giza totoro nyakati za usiku kukosekana kwa umeme kulifanya shughuli mbalimbali zisimame, huku wale wachache wanaotumia majenereta wamepandisha gharama za utoaji wa huduma zikiwamo mashine za kusaga nafaka, kuchaji simu na masaluni.

  Kukatika kwa umeme huo tangu Jumapili iliyopita, kumekuwa kinyume kabisa na tangazo la TANESCO lililoelezea kuwa umeme huo utakatwa kutoka tangu saa 3.00 siku hiyo hadi saa 10.00, lakini hali imeonekana kuwa tofauti kabisa na hivyo kusababisha mkoa huo utawaliwe na miungurumo ya majenereta.

  Kuhusu tukio lililomkumba juzi mtaalamu wa umeme kutoka makao makuu akiwa kwenye timu iliyoungana na mafundi wengine wa mkoani humo, kuwa alidondoka kutoka juu ya transfoma kwa madai kuwa alirushwa na umeme, lakini taarifa za ndani kutoka kwenye shirika hilo zimekuwa zikificha tukio hilo.

  Mkurugenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Dk Eliuter Samky, alipohojiwa jana alikiri kutokea kwa tukio hilo akidai kuwa walimpokea hospitalini hapo mfanyakazi wa TANESCO aliyeletwa, baada ya kupata maumivu makali lakini hakuweza kumtaja jina lake.

  "Unajua huyu ni mgonjwa na hatuwezi kutoa siri za mgonjwa, ila ninachofahamu ni kuwa mfanyakazi wa TANESCO ameletwa hapa na sijui kama ameanguka huko kwenye transfoma au sehemu nyingine, tumemtibu alikuwa ameumia," alisema Dk Samky.

  Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima, mbali ya watendaji wengine wa TANESCO kusita kutaja jina lake uliweza kufanikiwa kulipata jna moja la Mkweche kuwa ndiye aliyeanguka katika pilikapilika za kurejesha umeme ambao bado umezua kitendawili mkoani humo.

  Mbali ya tukio hilo, wakazi kadhaa wa Mwanjelwa walionekana wakiyazomea magari ya TANESCO kila yalipokuwa yakipita kuwa huo wote ni ufisadi uliosababishwa na mkataba mbovu wa umeme wa IPTL ambao umeliingizia hasara taifa na kusababisha fedha za kutengeneza muindombinu mingine kwa umeme wa dharura kutokuwepo.

  Baadhi ya wananchi walisikika walipokuwa wakiyazomea magari hayo kuwa wanamtaka, Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja, afike mkoani humo ili aweze kuwaeleza kwa kina tatizo hilo na kwa nini hakuna transifoma za dharura.

  Wakati hali ikiwa hivyo kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa hospitali ya Rufaa, Dk Samky, alisema kuwa huduma muhimu katika hospitali hiyo zimesimama na wanachokifanya ni kutoa huduma za dharura kwa wagonjwa mahututi ili kuokoa maisha yao na huduma nyingine ambazo hawatumii umeme.

  Katika chumba cha X-Ray hakukuwa na huduma zozote zinazotolewa na hivyo kuwafanya wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo kuikosa, na kwamba huduma inayoweza kutolewa hapo ni ile ya ultra-sound, huku mawodini wauguzi wamekuwa wakitumia mishumaa kuendelea na huduma mbalimbali.

  Mazingira hayo yote yamesababisha pia bei za vyakula zipande kama mchele, baada ya watu kukosa umeme wa kusagia nafaka na kujikuta wakinunua mchele kwenye masoko kupanda bei.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,470
  Trophy Points: 280
  Mwandishi Wetu
  Daily News; Tuesday,December 02, 2008 @21:15

  Mkoa wa Mbeya umekumbwa tena na ukosefu wa umeme baada ya transfoma iliyotengenezwa wiki iliyopita kuharibika tena jana. Taarifa ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) iliyotolewa jana Dar es Salaam, imesema hitilafu iliyojitokeza sasa ni kubwa kuliko ile ya mwanzoni, iliyosababisha mkoa huo kuwa gizani kwa takribani wiki moja.

  Imesema jitihada za dharura zinafanyika kupunguza makali ya ukosefu wa umeme kwa kuhamisha transfoma iliyopo Mufindi, mkoani Iringa na kuipeleka Mbeya. Hata hivyo, taarifa imesema transfoma hiyo ya Mufindi siyo kubwa kama hiyo iliyoharibika, hivyo wakazi wa Mbeya watalazimika kupata umeme utakaotosha kwa matumizi ya taa pekee wakati suluhisho la kudumu la tatizo hilo likitafutwa.

  Transfoma kutoka Mufindi ilitarajiwa kufungwa Mbeya usiku wa kuamkia leo. Wiki iliyopita mkoa wa Mbeya ulikosa umeme kwa wiki nzima kutokana na transfoma hiyo kupata hitilafu na kuathiri huduma za hospitali na nyinginezo.

  [​IMG]
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,470
  Trophy Points: 280
  Tatizo la umeme Mbeya utata mtupu

  na Christopher Nyenyembe, Mbeya
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  HALI ya umeme katika Mkoa wa Mbeya, imeendelea kuwa tete huku kukiwa na usiri wa kiini cha tatizo na kuibua maswali mengi kutoka kwa wananchi wa mkoa huo wanaokabiliwa na wakati mgumu kutokana na tatizo hilo.

  Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima kutoka vyanzo mbalimbali vya habari mkoani hapa, umebaini kuwa matengenezo ya transfoma mbili za TANESCO zilizoharibika kwa nyakati tofauti mkoani hapa, ndizo zilizosababisha mkoa huo kukosa umeme kwa muda usiojulikana. Inadaiwa kuwa transfoma hizo zilizofungwa miaka ya 1984 zikiwa na umri wa miaka 24, zimechakaa na haziwezi kufanya kazi ipasavyo kutokana na hitilafu iliyotokea mara ya kwanza.

  Habari zaidi zinadai kuwa uwezekano wa kuzifufua na kuzirudisha kwenye hali yake ya kawaida ni mdogo huku kazi hiyo ikiwa inafanywa kwa uangalifu mkubwa na wataalamu wa TANESCO usiku na mchana bila mafanikiwa.

  Wakati wataalamu hao wakihaha kutengeneza, habari za ndani na za uhakika zinadai kuwa TANESCO inafanya mpango wa kuleta transfoma nyingine kutoka Mafinga Mkoa wa Iringa iliyokuwa ikipeleka umeme kwenye Kiwanda cha karatasi cha Mgololo.

  Hata hivyo imeelezwa kuwa kuna ugumu katika kuisafirisha na kuifunga transfoma hiyo mahala panapotakiwa.

  Ugumu zaidi umeelekezwa kwenye kazi ya ufunguaji kwamba ili iweze kufunguliwa mahali ilipo, inaweza kuchukua muda wa wiki kabla ya kusafirishwa kuja Mbeya.

  Mbali ya mazingira hayo yanayoonyesha tatizo hilo lililotokea kwa muda mrefu na TANESCO wenyewe bila kutafuta njia mbadala mara baada ya hitilafu ya kwanza kwani walichukua muda kuagiza nyingine mpya ambayo haijulikani lini itatua nchini.

  Licha ya kuwepo kwa utata huo na usiri wa shirika hilo kushindwa kuwaeleza wananchi ukweli kwa kila hatua inayoendelea, inadaiwa kuwa watendaji wa TANESCO wamekuwa wakivutana katika utoaji wa taarifa ambazo wamebaini kuwa nyingi zimekuwa zikiwachanganya watu.

  Hivi sasa, vyombo vya habari haviruhusiwi kufika kwenye eneo hilo kupata taarifa kwa madai kuwa hadi wapate kibali maalumu.

  Wakati hali ikiendelea kuwa hivyo, hali ya maisha ya wakazi wa mkoa huo yamekuwa ghali huku bidhaa mbalimbali zikiwa zimepanda bei mara mbili, huku huduma nyingi za kijamii, zikiwa zimesimama.

  Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wananchi wameleza kukatishwa tamaa na mazingira hayo, huku wakiwataka baadhi ya watendaji wa TANESCO waliohusika na uzembe huo, wawajibike.

  Baadhi ya wananchi waliozungumza na Tanzania Daima, wamefika hatua ya kumtaka hata Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipelile kuachia ngazi kwa madai kuwa ameshindwa kutoa taarifa za mara kwa mara juu ya tatizo hilo mkoani hapa.
   
 7. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Alafu hawa wambeya wameamka kweli kweli. ndio wamegomea shule kuitea jina la mkuu wa Mkoa wao.Dah kweli wanalipiziwa kisasi
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  Dec 9, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Muungwana anawafix kwani walijifanya watemi. Watakaa gizani mpaka 2009!!!
   
 9. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #9
  Dec 9, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hivi wakuu SLA za huduma hii zinasemaje?(if at all zipo)
   
Loading...