MAFILILI
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 2,377
- 1,200
Katika hali inayoashiria kupimana ubavu katika jimbo la Mbeya Mjini ambalo mbunge wake ni Joseph Mbilinyi a.k.a. "SUGU" kupitia CHADEMA na Naibu Waziri wa Elimu, Philip Mulugo imezidi kupamba moto baada ya vijana zaidi ya 300 waendesha boda boda kuhama kambi ya Sugu na kujiunga rasmi kambi ya Mulugo. Vijana hao ambao walikuwa ni nguvu na tegemeo la SUGU na CHADEMA kwa ujumla katika harakati za kisiasa jijini Mbeya, wamempa Mulugo fursa ya kuwa mlezi wao kwa vile SUGU amedhihirisha kuwa ni mbabaishaji na hayuko karibu na wananchi. Hizi ni dalili tosha kuwa zama za SUGU na CHADEMA jijini Mbeya zinafikia ukingoni. Mulugo ameonyesha mfano kwa kuwawesha vijana kuanzisha SACCO na kuchangia shilingi milioni 1 na laki 4 kwa nia ya kuomgeza wigo wa kuendesha shughuli za kujiletea vipato, jambo ambalo SUGU alishindwa kulifanya tangia achaguliwe kuwa mbunge, pia vijana husika wamechukia kitendo cha SUGU kutoenda kuwajulia hali walipokuwa wameshikwa kwa kosa la kuleta mtafaruko kwa lengo la kuieneza CHADEMA.
Chanzo; Gazeti la Majira, Januari 15, 2013
Chanzo; Gazeti la Majira, Januari 15, 2013