Mbeya City Sasa Kimataifa Zaidi

Mbeya City Sasa Kimataifa Zaidi

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,154
Reaction score
13,267
Update 25/5/2014

WAWAKILISHI wa Tanzania Bara katika michuano mipya ya klabu ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) iitwayo Nile Basin, Mbeya City wameanza vizuri leo baada ya kuifunga mabao 3-2 Academie Tchite ya Burundi mjini Khartoum, Sudan.
Mabao ya Mbeya City katika mchezo huo wa Kundi B yamefungwa na Paul Nonga dakika ya 15, mshambuliaji mpya Themi Felix kutoka Kagera Sugar dakika ya 27 na Mwagane Yeya dakika ya 37. Mabao ya timu ya Burundi yamefungwa na Rashid Patient dakika ya 10 na Munirakiza Cedric dakika ya 68.[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Wachezaji wa Mbeya City wakishangilia moja ya mabao yao leo[/TD]
[/TR]
[/TABLE]







Kila la heri Mbeya City Cecafa Nile Basin

mbeya.png

Kocha wa Mbeya City.


MEI 22, mwaka huu Mbeya City itaanza harakati zake za kuwania Kombe la Nile Basin linaloandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kwa kushirikiana na Serikali ya Misri.

Jina kamili la michuano hii ni ‘Cecafa Nile Basin Cup' yaani Kombe la Cecafa la Bonde la Mto Nile. Bendera ya Tanzania itapeperushwa na Mbeya City, timu ngeni kabisa katika soka la ushindani Tanzania lakini imeonyesha ukomavu mkubwa.

Wakati Ligi Kuu Bara inaanza Septemba mwaka jana, hakuna aliyewaza kama Mbeya City ingeweza kuwa moja kati ya timu kali na tishio katika soka la Tanzania. Labda viongozi wa timu hiyo na benchi la ufundi ndio waliowaza makali ya timu yao.

Timu hii imeonyesha kwamba, katika soka lolote linawezekana inapokuwepo nia na malengo ya kutaka kufanikiwa, kinyume cha hapo hakuna litakalotendeka na hakuna njia ya mkato.

Kutokana na uhodari wake, Mbeya City almanusura ishike nafasi ya pili katika ligi lakini ikaishia nafasi ya tatu huku ikipata matokeo mazuri katika mechi 26 za ligi ilizocheza.

Nidhamu ya wachezaji, kocha, viongozi hata mashabiki ndicho kitu pekee kilichoifanya Mbeya City leo hii ipate heshima kokote inakopita nchini. Heshima ya timu hii, imeziongezea thamani jezi zake ambazo zimetapakaa kote nchini.

Sasa Mbeya City imepata nafasi ya kuiwakilisha nchi ndani ya msimu mmoja tu, hizi ni hatua za haraka sana katika ukuaji lakini lazima tukubali kuwa timu hii inapata inachostahili.

Tunaiamini Mbeya City kwamba itafanya vizuri katika michuano hiyo ndio maana hakuna minong'ono yoyote pindi Cecafa ilipoipa nafasi ya kuiwakilisha nchi baada ya Azam FC kutokuwa na nafasi ya kucheza michuano hiyo.

Wote tupo nyuma ya Mbeya City katika kuhakikisha Bendera ya Tanzania inapepea vizuri katika michuano hiyo kwani ushindi wa timu hiyo ni wetu sote, wala siyo wa watu wa Mbeya na vitongoji vyake.

Jukumu la kuiunga mkono timu hii ni letu sote na kamwe hatuwezi kuiacha Mbeya City ikiwa mpweke katika michuano hiyo ukizingatia uchanga wake katika soka la ushindani, tena ngazi ya kimataifa.

Pia, hiki ni kipimo tosha kwa wachezaji wa Mbeya City ambao wanacheza mechi za kwanza za michuano nje ya ardhi ya Tanzania na watambue hiyo ni nafasi yao ya kipekee kujitangaza na kuuza vipaji vyao kimataifa.

Misri ni miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo ligi yake imepiga hatua ikiwa na ufadhili mkubwa unaowezesha wachezaji wake kulipwa mamilioni ya fedha.
​

 
wasibweteke kqma Tukuyu starz
 
shukran sana kwa udadavuzi.mbeya city wakaze

Sure wakaze buti, wasiltuletee yale mauzauza ya Mapinduzi Cup kule Zanzibar mwanzoni mwa mwaka huu ambapo waliondolewa mapema tena kwa aibu! Kila la Heri MCC.
 
Wamekuwa na msimu mzuri,naamini watatuwakilisha vyema kwenye mashindano.
 
Unaweza kuwa sahihi, ila ingekuwa sahihi zaidi kama ingeelezwa bayana kwamba washiriki wa mashindano hayo ni washindi wa pili wa Ligi Kuu za nchi wanachama.
 
Unaweza kuwa sahihi, ila ingekuwa sahihi zaidi kama ingeelezwa bayana kwamba washiriki wa mashindano hayo ni washindi wa pili wa Ligi Kuu za nchi wanachama.

Jamal Malinzi ni wmenzetu humu
 
Walisema eti nguvu ya soda hahaha pambafu sana ngoja tukawashangaze na wenzenu huko nile basin
 
Hongera mbeya city, ushindi wenu ni ushindi wa taifa
 
Back
Top Bottom