Mbeya City CFC kulipia karo wanafunzi 100 Jijini Mbeya

Mbeya City CFC kulipia karo wanafunzi 100 Jijini Mbeya

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,356
10419010_526314417514940_7371742682106637412_n.jpg

​

Timu ya Mbeya City Council Fc inayoshiriki Ligi kuu ya soka Tanzania bara imetangaza kuwa italipa karo za shule kwa watoto zaidi ya 100 wanaosoma katika shule mbalimbali zilizopo mkoani Mbeya.

Akizungumza katika tamasha la Mbeya City Family Day Mwenyekiti wa timu hiyo Mussa Mapunda amesema kuwa uongozi umeamua kufanya jambo hilo kama sehemu ya kuunga mkono na kuchangia shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni moja ya mambo ambayo klabu imejiwekea utaratibu huo ikiwa na lengo likiwa la kuusogeza mchezo wa mpira wa miguu katika jamii za watu wote.

“hii ni sehemu ya mipango yetu mingi, Programu hii itatekelezwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta za umma na binafsi katika kuchangia shughuli mbalimbali za kijamii ili kufanya jamii kuwa sehemu nzuri ya kuishi kwa watu wote” alisema Mapunda .

Akiendelea zaidi Mwenyekiti huyo alisema kuwa katika kutekeleza hili klabu italipa karo ya shule kwa watoto 100(wakike 45 na wa kuime 55) wanaosoma katika shule mbalimbali za serikali zilizopo katika mkoa wa Mbeya lengo likiwa ni kuwasaidia waweze kusoma vizuri bila ya wasiwasi jambo ambalo litawaongezea ufanisi darasani.

“Wanafunzi hawa ni wale ambao hawana uwezo na ni wale waliopo kidato cha kwanza, tumefanya hivi ili mchakato wa kupata elimu usikwazwe na kuleta tatizo la mdondoko(drop out) katika matokeo yao” alimaza.

Programu hii itakua endelevu, itafanyika mikoa mingi ya nchi kufuatana na uwezo wa klabu kifedha.

Chanzo: Mbeya City Council FC -
 
Safi sana. Mapinduzi muhimu. Wale makanjanja na wapigaji wa simba na yanga hawawezi kufikiria mambo km haya wao wanafikiria mitumbo yao tu.
 
Back
Top Bottom