Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Wanaume wanaoishi na virusi vya Ukimwi sasa huenda wakapata suluhisho la kupata watoto na wenza wao ambao hawana virusi hivyo, baada ya kuwapo tiba ya kusafisha mbegu za kiume zenye VVU hapa nchini.
Tiba hiyo sasa inapatikana hapa nchini katika hospitali moja iliyo jijini Dar es Salaam, ambayo inatoa huduma za uzazi na upandikizaji wa mimba katika mirija ya uzazi kitaalamu inayojulikana, In Vitro Fertilization,(IVF). Kwa sasa, njia ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (MTCPT) ndiyo inayotumika duniani kote kwa mjamzito kupewa dawa za ARV wakati wa ujauzito zinazokinga maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na baada ya mtoto kuzaliwa.
Jinsi mbegu zinavyooshwa
Kisayansi, damu pekee si kipimo cha kuonyesha kuwapo kwa maambukizo ya VVU katika mwili bali hata katika majimaji ya mwilini.
Ogani zinazozalisha majimaji ya mbegu za kiume, huathiriwa kwa namna ya pekee na VVU.
Daktari Bingwa wa Uchunguzi wa magonjwa, Henry Mwakyoma alisema kwa kawaida virusi vya Ukimwi hupenda kukaa katika chembehai nyeupe(CD4).
"Kwa kawaida VVU haviishi katika mbegu za kiume. Lakini hupendelea zaidi kukaa katika CD4 au chembehai nyeupe za damu ambazo zipo katika damu na katika majimaji ya mbegu za kiume au semen," alisema.
Alisema ndiyo maana inawezekana mwanamume mwenye VVU, asimwambukize mwenza wake.
"Kama hana michubuko mwanamke anaweza asipate maambukizo, kwa kuwa majimaji ya mbegu za kiume yanakosa mahali pa kuingia," anasema.
Daktari wa Kitengo cha Uchunguzi wa magonjwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Innocent Mosha anaungana na Dk Mwakyoma na kusema, kwa kawaida mbegu za kiume hazina VVU kwa sababu ni seli inayojitegemea, lakini majimaji yanayobeba mbegu hizo ndiyo huwa na VVU.
Wanasayansi wanasema mwanamume anaweza asionyeshe VVU katika damu, lakini majimaji ya mbegu za kiume yakaonyesha uwapo wa virusi. Wanaeleza kuwa kwa mwanamume anayetumia dawa za kufubaza makali ya VVU, majimaji hayo yakipimwa hayaonyeshi uwapo wa VVU, bali virusi huonekana katika damu tu.
Hii ni kwa sababu ARV hupunguza wingi wa virusi na hivyo kushuka na kufikia kiwango cha kutoonekana.
Jarida la Science Daily la nchini Uingereza linaonyesha robo tatu ya wanaume wanaoishi na VVU na wanaotumia ARV, walipopimwa majimaji yanayobeba mbegu za kiume hayakuwa na VVU.
Katika kusafisha huko kwa mbegu za kiume,wanasayansi husafisha maji yanayobeba mbegu hizo kwani kiuhalisia mbegu haziathiriki na UKIMWI ila ni maji yanayozibeba.
Mwananchi.