Mkuu nakushauri ni vema ukatembelea duka la pembejeo za kilimo hasa maduka makubwa katika eneo au mkoa unaoishi, naamini ukiwauliza hao wahusika kwa udadisi watakupatia ushauri mzuri sana kuhusiana na mbegu bora ya mahindi kulingana na uhitaji wako.
Naamini ukizingatia hilo utafanikiwa...kumbuka ushauri atakaokupa mkulima wa morogoro ni tofauti na yule wa katavi au songea au mtwara...mtu atakupa ushauri kulingana na hali ya mvua ya eneo husika.
Kila lakheri mkuu.