Thanks bro..Mkuu nakushauri ni vema ukatembelea duka la pembejeo za kilimo hasa maduka makubwa katika eneo au mkoa unaoishi, naamini ukiwauliza hao wahusika kwa udadisi watakupatia ushauri mzuri sana kuhusiana na mbegu bora ya mahindi kulingana na uhitaji wako.
Naamini ukizingatia hilo utafanikiwa...kumbuka ushauri atakaokupa mkulima wa morogoro ni tofauti na yule wa katavi au songea au mtwara...mtu atakupa ushauri kulingana na hali ya mvua ya eneo husika.
Kila lakheri mkuu.
Kwa mkuranga na huku pwani kwa kuwa misimu ya mvua ni mifupi sana mbegu nzuri ni MTV1,shoka hizo ni miezi miwili. Au panda staha... Miezi 3 . hizo mbegu nzuri sana kwa ukame magonjwa na zinaweka vizuri zipo sana maduka ya pembejeo karibia mkuranga nzima
Asante kiongozi, ntaenda hapo mkuranga mjini nikaulizie hizo mbegu kwa ajili ya kulima vuli zikianza..Kwa mkuranga na huku pwani kwa kuwa misimu ya mvua ni mifupi sana mbegu nzuri ni MTV1,shoka hizo ni miezi miwili. Au panda staha... Miezi 3 . hizo mbegu nzuri sana kwa ukame magonjwa na zinaweka vizuri zipo sana maduka ya pembejeo karibia mkuranga nzima