Mbatia: Wabunge wa CCM ni waoga!

Mbatia: Wabunge wa CCM ni waoga!

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,640
Reaction score
164,788
MWENYEKITI wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), James Mbatia, amesema baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wana nidhamu ya woga na wamekuwa wakiweka maslahi ya chama mbele badala ya kuweka maslahi ya Taifa.

Akizungumza Dar es Salaam jana kuhusu maazimio ya kikao maalumu cha viongozi wakuu wa vyama vya siasa vyenye wabunge na Chama cha UPDP kinachowakilisha vyama visivyo na wabunge, alisema hali hiyo inasababisha hoja nyingi zenye maslahi ya wananchi kutoungwa mkono.

Aidha, amevitaka vyama vitoe mafunzo kwa wabunge wake na hatimaye kila mbunge aelewe wajibu wake na kuweka itikadi ya chama pembeni pindi awapo bungeni.

Aliwataka wabunge wote wakae pamoja kukumbushana wajibu kabla ya kuanza kikao cha Bunge kitakachoanza Aprili 9, mwaka huu.

Alisema nidhamu hiyo ya woga ambayo ipo miongoni mwa wabunge wa chama tawala, inafanya hoja nyingi kuzimwa kwa kuwa haziungwi mkono pale inapoonekana wabunge wengi wameonekana kutoikubali, huku wachache wa vyama pinzani wakiunga mkono.

"Hoja nyingi za msingi haziungwi mkono na wabunge wa CCM, kama vile hoja ya tatizo la maji iliyotolewa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, haikuungwa mkono na wabunge wa CCM, licha ya kuwa katika majimbo yao kuna shida ya maji.

"Hata ukiangalia hoja yangu kuhusu suala zima la elimu, hoja ya Hamis Kigwangala kuhusu suala la ajira kwa vijana hoja hizi zote zipo kwa maslahi ya Taifa, lakini bado haziungwi mkono na kwa kuwa wengi wape basi hata kama wachache wataunga spika atasema wengi wameshinda," alisema Mbatia.

Alisema katika kikao hicho waliazimia mambo mbalimbali, ikiwamo wajibu wa kwanza kwa mbunge lazima uwe kwa Taifa akiwa mahali popote, lakini pia mbunge huyo lazima awe na wajibu katika eneo lake la uchaguzi, awe na wajibu katika chama chake kilichompeleka bungeni na mwisho lazima awe na wajibu kwa dhamira binafsi.

"Umefika wakati sasa mchakato wa mabadiliko ya Katiba ijayo uwezeshe kikamilifu kuwa na Katiba mpya yenye mgawanyo bora wa madaraka, kwa kuwa sasa hivi inaonekana mhimili mmoja ambao ni Serikali unaonekana kuwa na nguvu kuliko mihimili mingine, huku mahakama ikionekana kukosa nguvu na kuwa kama sehemu ndogo," alisema Mbatia.

Source: Mtanzania la tarehe 08/03/2013.
 
Angesema wazi tu mbunge Said Bagaile ana nidhamu ya uoga!

In another development, the chairman of the opposition NCCR-Mageuzi, Mr James Mbatia, waded into the controversy by claiming that the CCM candidate had forged his certificates.

Mr Mbatia said the Dr Kingwangala used the Standard Seven results of the NCCR-Mageuzi candidate for the Nzega seat, Mr Hamis Andrew Kigwangala, to further his education after failing primary school leaving examinations. He said the CCM candidate was then known as Said Nassor Bagaile.

Efforts to reach the Nzega District Commissioner, who chairs the local security and defence committee, to comment on the matter failed.
 
Walichonacho Wabunge wa CCM sio nidhamu ya woga; hawana nidhamu kabisa, ni wachumia matumbo; kunyonga hoja za wapinzani ni mkakati wao wa makusudi wa kuficha maovu lukuki yaliyoasisiwa na kutekelezwa na chama chao CCM
 
Tatizo ni mitandao ndani ya CCM. Upinzani utakomaa pale CCM itakapogawanyika.
 
MWENYEKITI wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), James Mbatia, amesema baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wana nidhamu ya woga na wamekuwa wakiweka maslahi ya chama mbele badala ya kuweka maslahi ya Taifa.

Akizungumza Dar es Salaam jana kuhusu maazimio ya kikao maalumu cha viongozi wakuu wa vyama vya siasa vyenye wabunge na Chama cha UPDP kinachowakilisha vyama visivyo na wabunge, alisema hali hiyo inasababisha hoja nyingi zenye maslahi ya wananchi kutoungwa mkono.

Aidha, amevitaka vyama vitoe mafunzo kwa wabunge wake na hatimaye kila mbunge aelewe wajibu wake na kuweka itikadi ya chama pembeni pindi awapo bungeni.

Aliwataka wabunge wote wakae pamoja kukumbushana wajibu kabla ya kuanza kikao cha Bunge kitakachoanza Aprili 9, mwaka huu.

Alisema nidhamu hiyo ya woga ambayo ipo miongoni mwa wabunge wa chama tawala, inafanya hoja nyingi kuzimwa kwa kuwa haziungwi mkono pale inapoonekana wabunge wengi wameonekana kutoikubali, huku wachache wa vyama pinzani wakiunga mkono.

"Hoja nyingi za msingi haziungwi mkono na wabunge wa CCM, kama vile hoja ya tatizo la maji iliyotolewa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, haikuungwa mkono na wabunge wa CCM, licha ya kuwa katika majimbo yao kuna shida ya maji.

"Hata ukiangalia hoja yangu kuhusu suala zima la elimu, hoja ya Hamis Kigwangala kuhusu suala la ajira kwa vijana hoja hizi zote zipo kwa maslahi ya Taifa, lakini bado haziungwi mkono na kwa kuwa wengi wape basi hata kama wachache wataunga spika atasema wengi wameshinda," alisema Mbatia.

Alisema katika kikao hicho waliazimia mambo mbalimbali, ikiwamo wajibu wa kwanza kwa mbunge lazima uwe kwa Taifa akiwa mahali popote, lakini pia mbunge huyo lazima awe na wajibu katika eneo lake la uchaguzi, awe na wajibu katika chama chake kilichompeleka bungeni na mwisho lazima awe na wajibu kwa dhamira binafsi.

"Umefika wakati sasa mchakato wa mabadiliko ya Katiba ijayo uwezeshe kikamilifu kuwa na Katiba mpya yenye mgawanyo bora wa madaraka, kwa kuwa sasa hivi inaonekana mhimili mmoja ambao ni Serikali unaonekana kuwa na nguvu kuliko mihimili mingine, huku mahakama ikionekana kukosa nguvu na kuwa kama sehemu ndogo," alisema Mbatia.

Source: Mtanzania la tarehe 08/03/2013.
wal hawana uthubutu
 
Sio waoga ila hawajui kilicho wapeleka bungeni. Waliambiwa wao ni kulala na kusema ndiooooo kwa maslahi ya matumbo yao.
 
Chama kiwafundishe wabunge wake kukipinga Bungeni? Hii ni ajabu Mh Mbatia kaisema
 
kama mbunge wangu ndo balaaa, sijawahi msikia akisema matatizo ya jimbo lake. na pia wanajali sana biashara zao kuliko wananchi.
 
Kuendelea na ccm baada ya 2015 ni kujitumbukiza kwenye dimbwi la UMASKINI ambamo hatuwezi kujiokoa hata kama chama cha UPINZANI kikishika nchi baada ya miaka mingine kumi. Kama KIKWETE ametuacha HOI TAABANI KIMAISHA hii miaka nane, itakuaje baada ya miaka mingine miwili, na kisha tuwaongezee miaka mingine kumi? Hali itakuwa mbaya zaidi, KUENDELEA NA RAIS WA CCM BAADA YA 2015, HAKIKA TUTAKUJA KUMSIFU JK PAMOJA NA MADUDU ALIYOYAFANYA!!!
 
Back
Top Bottom