Mbatia na Cheyo hamueleweki kabisa

Mbatia na Cheyo hamueleweki kabisa

jnuswe

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
1,270
Reaction score
549
WanaJF.

Mimi si kusikitishwa tu bali nim,eshangazwa sana na nashindwa kuamini kama kweli nchi hii kuna vyama imara vya upinzani

Juzi tu Mh. Mbatia kalaumiwa kwa kukiuka yale waliokubaliana kama vyama vya upinzani kuwa kongamano la amani atafutwe mwezeshaji atakaye liendesha badala ya serikali (CCM) yeye akaamua kufungamana na ccm (serikali ) ili wao ndo waratibu kongamano hilo hili akijua wazi chanzo cha kuanza kutoweka kwa amani nchi hii kinasababishwa na ccm.

Mh. Cheyo naye anailaaumu CHADEMA, kwa kuja na mpango wa kufundisha vijana juu ya kujilinda dhidi ya uonevu wa polisi na ccm kwa kutumia vikosi vyao vya uharifu vya Green Guard. Anasema hakubaliani na suala hilo, mimi nimeshindwa kuwaelewa hawa kama kweli ni wapinzani ? ama wanaitumikia CCM na serikali yake

Wote tunakumbuka aliyoyasema Mh. Mrema alipoenda kumtembelea Mh. Nassari pale Mhimbili alikokuwa amelazwa baada ya kuumizwa vibaya na watu waliokuwa wametumwa na ccm kumdhuru mbunge huyo; Mh. Mrema alisema "ccm ni mbaya haya yanayowapata yalinipata na mimi lakini nina uhakika hawataweza"

Kweli nchi hii kuna vyama vya upinzani ama vipo kwa ajili ya kuganga njaa tu ? ili bora liende
 
Mbatia mwenyewe kawezeshwa na CCM hadi ubunge na sio bahati mbaya,kuna mapishi yanapikwa jikoni kwa kuitumia NCCR MAGEUZI na kiongozi mmoja wa upinzani na kupeleka watu maarufu toka ccm kwa minajili ya kuidhoofisha CHADEMA na kugawa kura,maneno ya ZZK( Zana Zaio) kuhusishwa na kuhama Chama sio maneno tu ya kukoteza kwani Ccm wanajuana agombee uchaguzi ili iwe kama Lipumba 2010 au ahame wamfadhili,inshort jamaa ni mradi wao.

Tujikumbushe ya Cheyo,kamati anapewaga na ccm,tujikumbushe na Mrema halafu utitiri wa vyama then historia ya Kigoma,waweza pata picha
 
Unajichanganya. Kama bado huwajui wapinzani wa kweli dhidi ya CCM, nawe pia unastahili watu wakushangae.
 
Unajichanganya. Kama bado huwajui wapinzani wa kweli dhidi ya CCM, nawe pia unastahili watu wakushangae.

Hii itakuwa ajabu ya karne Mbatia na Cheyo kuwa wapinzani wa kweli , unasababisha na wewe watu sasa wakushangae ! waliwahi sikia wapi mpinzani wa kweli anapewa fadhila za viti maalum kama ilivyo kwa Mbatia, ujanishawishi lete hoja nyingine hii sio hoja
 
Ooh ! Makene nafikiri hujanielewa wapinzani wa kweli dhidi ya CCM mimi najua ni CHADEMA na NCCR kwa maana ya taasis lakini sio Mbatia kama mwenyekiti wa NCCR Mageuzi
 
Unajichanganya. Kama bado huwajui wapinzani wa kweli dhidi ya CCM, nawe pia unastahili watu wakushangae.
Mkianzisha maandamo mnakosa watu mnaanza kutangaza vyama vyote vya upinzani vijitokeze huwa nacheka sana, hapa unajifanya Chadema ndiyo wapinzani pekee wa CCM.
 
ndo analipa fadhila ya uteuzi wake kwa JK,hana jipya SIGARA KALI(ndumila kuwili) huyo
 
James Mbatia a big hypocrite!Kama ana balls kwa nini asigombee ubunge ?Ni ajabu kubwa eti kateuliwa na Raisi (CCM) na yeye ni NCCR?Njaa kitu kibaya sana,CCM wamejitahidi kumhonga huyu mtu,kumbukeni alipokuwa UDSM .na kukatishwa masomo yake.

John Cheyo ni opportunist.Anaongoza chama cha kinyantuzu(UDP).Hawezi kuwa mpinzani kamili kwa sababu yeye na kaka yake wana vitenda na serikali.
 
Mbatia ni Mbunge Mteule wa CCM, unategemea aende kinyume na Bossi wake. NCCR ndo wameliwa kwa kuwa na Kiongozi pandikizi la CCM. Kwa maana hiyo nccr Mageuzi ni haki kuitwa ccm B+C
 
mbatia na cheyo wote ni mapandikizi ya ccm ndani ya vyama vya upinzani
 
unapotaka kulinganisha wapinzani wa kisiasa na maadui wa taifa unatushangaza.
mbatia(NCCR), Cheyo(UDP), ni wapinzani wa kisiasa na wadau katika mustakabali wa taifa.
ILA CHADEMA NI ADUI MKUBWA WA USTAWI NA MUSTAKABALI WA TAIFA LETU
 
Huyu Cheyo toka afilisiwe viwanda vyake vya nguo kule Swaziland hajawahi kutulia kiakili!!??
 
Heshima wanajamvi,

Ni kweli tunaweza kuwalaumu Mbatia,Cheyo na Mrema kwamba wako kinyume na matarajio ya CDM,kwamba wamekubali ufadhili wa kongamano la amani atafutwe mwezeshaji mwingine badala ya CCM.

Sawa kabisa NCCR Mageuzi,TLP,CUF na UDP si wapinzani hawa ni makuwadi wa upinzani chama makini cha upinzani ni CDM tu vingine vyote ni vyama mauza uza ni vibaraka wa CCM.

Chama makini cha upinzani hakipaswi kuchukua mkondo wa kudharau vyama vingine vya upinzani,hata kama vyama hivyo vina kasoro ambazo CDM inahisi si vyema kuvitupa,kuvidharau,kuvikanyaga.

CDM ilifanya kosa kuvitosa vyama vyote vya upinzani na kuunda kambi ya upinzani pekee yake.Ilitoa angalizo kwamba isingeweza kuishirikisha CUF kwasababu imeungana na CCM Zanzibar labda hii inaweza kuwa sababu ya kukubaliana na CDM,vipi NCCR na UDP navyo vimeungana na CCM ?.Pamoja na ugoi goi wa vyama tajwa halikuwa jambo la busara kuviacha pekee bila ulezi wa namna fulani.Matokeo ya kuvisusa CCM imevinyakua na kuviweka chani ya himaya yake.Kulikuwa na shida gani kumpatia Mzee Mapesa wizara ya mifugo ? Vipi CDM ingewaingiza wabunge vijana wa NCCR katika serekali yake kivuli ?.

Mwanzo nilijaribu kuwashauri CDM wasijione wao ndiyo wapinzani pekee wajitahidi kushirikiana na wapinzania wengine huo ndiyo ukubwa.Ukiwaachaa bila uangalizii wataangukia sehemu nyingine ambayo utashindwa kuidhibiti.
 
Wewe unataka mbatia na cheyo wakubali ugaidi wa chadema au nao wafanye upumbavu wa kuuwa watu kama unaofanywa na chadema hakuna hiyo.
 
Halafu chadema hakuna kiongozi hata mmoja mwenye akili alikuwepo zito wakamweka pembeni sasa yamebaki yote mikondoo yakiamua ujinga yote yanaelekea huko.
 
Halafu huwezi kulinganisha vyama vya siasa na kundi la wanaharakati,chadema ni kundi la wanaharakati siyo rahisi kukaa na vyama vya siasa.
 
arusha-leo.jpg
4.jpg
Mkianzisha maandamo mnakosa watu mnaanza kutangaza vyama vyote vya upinzani vijitokeze huwa nacheka sana, hapa unajifanya Chadema ndiyo wapinzani pekee wa CCM.
hii kitu itawatesa sana CCM.
 
Huu Wimbo wa fulani sio mpinzani mmeuimba kwa muda mrefu sasa. Kadhalika tangia Mbatia ateuliwe kuwa mbunge mnarudia maneno yale yale kila siku kuhusu yeye. Ni dhahiri sasa kwamba huu nao kwenu ni mkakati wa kisiasa na hamkusudii kuuacha hivi karibuni. Pengine tutarajie threads nyingine zaidi za namna hii. Mtakapozileta tutawakumbusha haya.
 
WanaJF.

Mimi si kusikitishwa tu bali nim,eshangazwa sana na nashindwa kuamini kama kweli nchi hii kuna vyama imara vya upinzani

Juzi tu Mh. Mbatia kalaumiwa kwa kukiuka yale waliokubaliana kama vyama vya upinzani kuwa kongamano la amani atafutwe mwezeshaji atakaye liendesha badala ya serikali (CCM) yeye akaamua kufungamana na ccm (serikali ) ili wao ndo waratibu kongamano hilo hili akijua wazi chanzo cha kuanza kutoweka kwa amani nchi hii kinasababishwa na ccm.

Mh. Cheyo naye anailaaumu CHADEMA, kwa kuja na mpango wa kufundisha vijana juu ya kujilinda dhidi ya uonevu wa polisi na ccm kwa kutumia vikosi vyao vya uharifu vya Green Guard. Anasema hakubaliani na suala hilo, mimi nimeshindwa kuwaelewa hawa kama kweli ni wapinzani ? ama wanaitumikia CCM na serikali yake

Wote tunakumbuka aliyoyasema Mh. Mrema alipoenda kumtembelea Mh. Nassari pale Mhimbili alikokuwa amelazwa baada ya kuumizwa vibaya na watu waliokuwa wametumwa na ccm kumdhuru mbunge huyo; Mh. Mrema alisema "ccm ni mbaya haya yanayowapata yalinipata na mimi lakini nina uhakika hawataweza"

Kweli nchi hii kuna vyama vya upinzani ama vipo kwa ajili ya kuganga njaa tu ? ili bora liende

Sina kumbukumbu yeyote ya KONGAMANO la AMANI wakati wa utawala wa JK NYERERE! Cheyo na Mbatia huenda wana kumbukumbu hiyo. For God sake...amani haijengwi kwa makongamano ya kujitafutia umaarufu kwenye runinga na radio. AMANI inajengwa kwa kutenda haki tu...hata usali vipi...hata uongee ukitoa machozi ya damu...KAMA HUTENDI YALIYO HAKI HUTAKAA UPATE AMANI...tendeni yaliyo ya haki nanyi mtapata AMANI ya kweli. Mungu atutie nguvu tuache UNAFIKI tuseme yaliyo KWELI kwa faida ya vizazi vijavyo! Kwangu mimi, ukiona watu wanajilinda wenyewe basi serikali ipo likizo...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom