Mbatia: Mjadala wa Katiba usitishwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbatia: Mjadala wa Katiba usitishwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 11, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  na Datus Boniface

  MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ametaka kusikitishwa mara moja kuendelea na zoezi la kuratibu pamoja na kuwasilishwa katika kikao cha Bunge mjini Dodoma kwa Muswada wa Marejeo ya Katiba kutokana na muswada huo kuvunja Katiba ya nchi.

  Mbatia alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akitoa msimamo wa chama hicho kuhusu mjadala wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mbele ya waandishi wa habari.

  "Serikali inazungumzia Marejeo ya Katiba wakati sisi tunazungumzia Katiba Mpya, tangu kuanzishwa kwa chama chetu hatujawahi kuomba marejeo bali tulikuwa tukipigania kupatikana kwa Katiba Mpya iliyotungwa na wananchi wenyewe.

  "NCCR-Mageuzi tunatoa msimamo wa kupigwa ‘stop' haraka iwezekanavyo kuendelea na mchakato huu kwa maslahi ya taifa, kama wananchi wa Tanzania Visiwani (Zanzibar), wamepinga juu ya mchakato wenyewe, kuna maana gani ya kuuwasilisha katika kikao cha Bunge Dodoma?" alihoji Mbatia.

  Katika maelezo yake Mbatia alisema taratibu zinazofanyika katika kuratibu maoni ya muswada ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri inayotakiwa kurekebishwa.

  Mbatia alisema endapo marekebisho ya ibara hiyo yakishafanyika kama wanavyopendekeza, ni wazi kwamba katiba iliyopo itakuwa ndiyo mhimili wa msingi wa harakati zote za kupata katiba mpya, kutokana na kwamba yote yatakayofanyika yatakuwa na ridhaa ya Katiba. Ingawa Mbatia hakueleza sababu wanazotarajia kuchukua endapo serikali na mamlaka husika zitashindwa kusitisha zoezi hilo, alisema msimamo wao ni wa nia njema, wenye kuzingatia masilahi ya taifa na wananchi kwa ujumla.
   
 2. Butho Mtenzi

  Butho Mtenzi JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 328
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kaona mapungufu yake ni mengi mno mwenyee nimeshiriki Mdahalo Dodoma kama kweli ikipita Tz tutaona karaha kuu kuu nyingi na bora ata Katiba iliyopo cha kuomba ni Katiba Mpya na sio marekebisho ya Katiba iliyopo.
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Yaani inachotufanyia serikali ni heri hata michezo ya kitoto ninayo mfanyia mwanangu wa mwaka mmoja una manufaa kwake maana anacheka na kucheka ni afya
   
 4. only83

  only83 JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Jamaa naona kaamka....your welcome Kaka Mbatia,wewe unaanza mapambano leo? sisi tulianza miaka mingi iliyopita....But not too late,welcome!!!
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Apr 11, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hivi watu wengi wanachotaka ni katiba mpya kabisa na manailoni yake au marekebisho ya viraka kwa hii iliyopo sasa?

  I'm sensing people falling for the okie doke on this one and CCM is about to pull a fast one on all of us.
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  And they are about to do it sababu za kufanya mchakato wa mapendekezo ya Katiba uharakishwe haraka hilo ni jambo moja wapo, Wananchi na wao wapewe muda kuchangia na kutoa mawazo sababu katiba ni ya Wananchi siyo Chama ikumbukwe kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alitamka kuwa Katiba hii inahitaji marekebisho ya Viraka kwasababu CCM wanaona ni bora kwao kufanya hivyo kuliko kufanya overhaul ya Katiba nzima ambayo baadhi ya vipengele vilivyoko kwenye Katiba ya sasa vitaondoka kitu ambacho CCM hawataki
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Apr 11, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Poor us! Ni kama vile hatujui hata tunachokitaka. Watu wanahemukia mijadala kumbe mijadala yenyewe ni ya ku-amend the current constitution na sio kuandika a brand spankin' new one. Apples can't be oranges.
   
 8. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  You can imagine even the current constitution ni asilimia chache sana ya Wananchi wanayoijua wengi hawaijui, sasa watu wanakimbilia kutaka Katiba mpya wakati hata hii tuliyonayo Wananchi hawaijui like you said ni kama vile hatujui tunachokitaka leo hii ukienda kumuuliza mkulima wa kule Makambako kama Katiba iliyopo sasa hivi anaijua sidhani kama anajua chochote
   
 9. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mheshima Mbatia, point hiyo tena nzito sana!!!!!!!!!!
   
 11. N

  NewOrder JF-Expert Member

  #11
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 489
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Kama serikali hii italazimisha mabadiliko ya Katiba hii, ni wazi hali tete itaanza kujitokeza na wananchi watakuwa na sababu ya msingi ya kutumia nguvu yao!!

  CCM will have their back on the wall if they try to pull strings in this unprecedented way!! Wananchi will have to pull a rabbit out of a bag. I am afraid if thing whole thing is not halted by the same governments, the bad days are just around the corner!
   
Loading...