Mbatia hatihati Vunjo

Mbatia hatihati Vunjo

hapa vunjo tumepanga kuchagua mbatia -ila kukomalia madiwani wote alichemsha .segerea ni full chadema ila madiwani kulikua na mgawanyo muafaka -amekosea sana hyu mbatia ila CDM tUMPE KURA TU MAANA WALA CDM HAITAYUMBA
 
Hata lingekuwa gazeti lolote lile nazidi kusisitiza wanavunjo wasifanye makosa wakamwacha Mbatia kwa ushabiki wowote ule. Mbatia ni jembe la uhakika na ni mtu mwenye msimamo na uwezo mkubwa sana wa kuelewa, kutetea na kutenda mbali ya usomi wa hali ya juu alio nao. Huyu mzee Mrema ni ndumakuwili pandikizi na hajawahi kuwa mpinzani wa kweli na zaidi amezeeka na kuchoka. Asubiri nafasi aliyoahidiwa na Magufuli. Huyu wa ccm bado sana yeye aachwe ale kwanza ujana kwenye ma-night clubs ila silaha anayotishia nayo raia wema anyanganywe hadi atakapojitambua. Moshi mjini ikiwa kuna alieweza kuwaroga na mkalogeka mkiacha kumchagua Jaffary wa chadema maendeleo yote yaliyoletwa na mzee Ndesamburo akishirikiana na Jaffary yatayeyushwa kwa mwaka mmoja tu. Moshi vijijini nanyi nawaasa kuna jembe la chadema mmekabidhiwa hapo nae ni nd.Komu msije kudanganyika mkamwacha kwa ulaghai wa kapero,fulana na upande wa kanga mtajutia uamuzi wenu kwa miaka mitano. Huo ndio wosia wangu kama mzee ninae wafahamu wagombea hao na uwezo walio nao wa kuwatumikia. MABADILIKO UKAWA. UKAWA LOWASSA.

Hata Mbatia ni pandikizi la Ccm, tumuulize mdee wa Kawe anajua Siri

Mbatia anadai kuwa katika mikutano ya kampeni Mdee alimwita kuwa ni Fataki anayefanya mapenzi na watoto wa shule, kibaraka wa CCM na kila wiki analipwa sh milioni 80 na CCM hivyo kuwataka wapiga kura wa jimbo la Kawe wasimchague Mbatia.
 
Hata Mbatia ni pandikizi la Ccm, tumuulize mdee wa Kawe anajua Siri

Mbatia anadai kuwa katika mikutano ya kampeni Mdee alimwita kuwa ni Fataki anayefanya mapenzi na watoto wa shule, kibaraka wa CCM na kila wiki analipwa sh milioni 80 na CCM hivyo kuwataka wapiga kura wa jimbo la Kawe wasimchague Mbatia.

Zile zilikuwa ni mbinu tu za kujitafutia kura kwa Mdee na kisiasa hilo hufanyika sana. Hata wakati Mdee anatumia mbinu hizo kwa Mbatia wote walikuwa upinzani tofauti na Mrema anayafanya hayo kwa mwana ccm huku yeye akijidai kuwa upinzani. Hizo sio mbinu zinazokubalika katika siasa bali ni usaliti, unafiki na njaa kali.Ni vile sina uwezo wa kukuwekea hapa jamvini clip inayowaonyesha baadhi ya wanachama wa ukawa wamemzingira Mrema wakimuuliza ni nini lilikuwa lengo lake kufanya vile na anakotaka kuelekea. Walimchachamalia kweli kweli wakimwambia wazi kura zao zote sasa watampa Mbatia na akaondoka kimya kimya katokomea. Itafute kwenye youtube utaiona.
 
Mbatia asubiri tena huruma ya Rais ajaye apate ubunge wa kuteuliwa. Muda wote alikuwa anapiga domo akiwa Dar wakati akina Mnyika, Tundu Lisu na Mbowe wana ngome zao majimboni.


Mbatia amekuwa mtumwa wa lowassa ( Msukule wa lowassa) ili amsaidie kwenye mbio zake za ubunge huku akijua bila msaada wa Lowassa hawezi shinda. Naamini hivyo kwa Sababu:

1. Mwaka 1995 Mbatia aligombea ubunge akashinda, alishikwa mkono na Augustino Mrema na kuwaambia wana vunjo anaenda kugombea urais ila anawaachia kijana mbatia kuwa mbunge wao.

2. Mwaka 2000 Mbatia alimsaliti Mrema na alipogombea ubunge wana Vunjo walimwambia kama unataka ubunge aende kumwomba Mrema msamaha, kitu ambacho hakufanya kwa hiyo akapigwa chini na wana Vunjo. Pia, tukumbuke 1995 Mrema alipomshika mkono mbatia akipata kura 57,000 ambayo ilikuwa asilia 87 Ya kura zote. Alipomsaliti Mrema 2000 akipata kura 3,400 ambayo ni asilimia 2 ya kura zote.

3. Mwaka 2010 aligombea jimbo la Kawe akapata kura kiduchu akishika mkia kuwa mtu wa tatu, nyuma ya Mdee wa CHADEMA na mgombea wa CCM. Palikuwa hakuna mtu wa kumshika mkono.

4. Sasa 2015 anasubiria huruma ya Lowassa ndio maana habanduki ubavuni kwake na amekuwa msemaji wa CHADEMA huku chama chake cha NCCR kikiwa kinalegalega. Kweli lowassa amemhurimia ndio maana alikwenda Vunjo na kufanya mikutano mitatu Kahe, Kirua Vunjo na Himo. Hakuna jimbo jingine ambapo lowassa amefanya Mkutano zaidi ya mmoja. Lowassa hakufanya Mkutano Moshi mjini, Moshi vijijini waka Rombo.
Alipomaliza mikutano hiyo aliondoka.

Kila mgombea ubunge ameenda kujichimbia kwenye jimbo lake kusaka kura lakini yeye yupo ubavuni kwa Lowassa tu. Mfano Tundu Lissu yupo jimboni kwake anapambana ulitegemea ndio awe msemaji wa Lowassa lakini anapigana kiume jimboni kwake.

Mbatia siku zote anategemea huruma za wanasiasa wengine. Safari hii hilo halitawezekana. NCCR-Mageuzi imefia mikononi mwake.
 
Back
Top Bottom