Mbatia hatihati Vunjo

Mbatia hatihati Vunjo

Mbatia asubiri tena huruma ya Rais ajaye apate ubunge wa kuteuliwa. Muda wote alikuwa anapiga domo akiwa Dar wakati akina Mnyika, Tundu Lisu na Mbowe wana ngome zao majimboni.

Mbatia amekuwa mtumwa wa lowassa ( Msukule wa lowassa) ili amsaidie kwenye mbio zake za ubunge huku akijua bila msaada wa Lowassa hawezi shinda. Naamini hivyo kwa Sababu:

1. Mwaka 1995 Mbatia aligombea ubunge akashinda, alishikwa mkono na Augustino Mrema na kuwaambia wana vunjo anaenda kugombea urais ila anawaachia kijana mbatia kuwa mbunge wao.

2. Mwaka 2000 Mbatia alimsaliti Mrema na alipogombea ubunge wana Vunjo walimwambia kama unataka ubunge aende kumwomba Mrema msamaha, kitu ambacho hakufanya kwa hiyo akapigwa chini na wana Vunjo. Pia, tukumbuke 1995 Mrema alipomshika mkono mbatia akipata kura 57,000 ambayo ilikuwa asilia 87 Ya kura zote. Alipomsaliti Mrema 2000 akipata kura 3,400 ambayo ni asilimia 2 ya kura zote.

3. Mwaka 2010 aligombea jimbo la Kawe akapata kura kiduchu akishika mkia kuwa mtu wa tatu, nyuma ya Mdee wa CHADEMA na mgombea wa CCM. Palikuwa hakuna mtu wa kumshika mkono.

4. Sasa 2015 anasubiria huruma ya Lowassa ndio maana habanduki ubavuni kwake na amekuwa msemaji wa CHADEMA huku chama chake cha NCCR kikiwa kinalegalega. Kweli lowassa amemhurimia ndio maana alikwenda Vunjo na kufanya mikutano mitatu Kahe, Kirua Vunjo na Himo. Hakuna jimbo jingine ambapo lowassa amefanya Mkutano zaidi ya mmoja. Lowassa hakufanya Mkutano Moshi mjini, Moshi vijijini waka Rombo.
Alipomaliza mikutano hiyo aliondoka.

Kila mgombea ubunge ameenda kujichimbia kwenye jimbo lake kusaka kura lakini yeye yupo ubavuni kwa Lowassa tu. Mfano Tundu Lissu yupo jimboni kwake anapambana ulitegemea ndio awe msemaji wa Lowassa lakini anapigana kiume jimboni kwake.
 
Namuombea Mbatia Apite .Wananchi wa Vunjo Mchagueni Anauwezo Mkubwa wa Kutumikia Wananchi compare na Hao Wengine

Tatizo Mbatia kajisahau sana.
Hata ndani ya Chama upambe wa Lowassa umempotezea mwelekeo.
Yale malalamiko kuwa hata hajawnda kupiga kampeni na wagombea wa chama chake mwenyewe ni serious sana.
Kama leo Mbatia na Kafulila hawajasimama jukwaa moja ni hatari sana.
 
MTU asijewadanganya, Vunjo ni jimbo la Mbatia ije mvua - lije jua ushindi ni lazima kama siyo Razima!!

James mbatia hata pata kura Vunjo kwa sababu haonekani Vunjo yeye yupo ubavuni Mwa lowassa. Wanavunjo wanauliza kama Kwenye kampeni haonekani akipata ubunge itakuaje? Mbatia hana makazi Vunjo Nyumba anayofikia ni Ya wazazi wake, kiasi cha watu Vunjo kumwita "yahaya". Mbatia hana mke wala Mtoto wana Vunjo wanauliza ataongozaje jimbo la Vunjo na ubachela wake ataenda kustarehe Dar Es salaam. Pia, historia ya baba Yake aliyekuwa akiwatumikisha watu wa Vunjo Kwenye mashamba Yake bila kuwalipa malipo stahiki. Madiwani wa Chadema kumtosa mbatia na kuahidi kumpigia kura Mrema kwa kuwa mbatia anaua Chadema Vunjo kwa kung'ang'ania kuweka madiwani wa Nccr kata zote 16 na kuwanyima Chadema kata 8 kama walivyokibaliana Kwenye ukawa. Wana Vunjo wanajua mbatia anatumika Na Aloyce Kimaro wa Ccm ( mbunge wa Vunjo 2005- 2010) Land Rover hardtop wanazotumia Nccr Kwenye kampeni ni zake. Tunajua Mrema kafunga Kiwanda cha kimaro cha vinywaji na Zile eka 11 alipora ajenge kituo cha radio zimethibitiwa kwa hiyo huu msaada kwa mbatia ni kwa ajili gani, hii ndoa ya ukawa na Ccm Vipi? Wana Vunjo sio wajinga. Wanaona Na wanajiuliza
 
Hata waongezeke na act. Mbatia lazima ashinde wananchi wa wavunjo wanamsimamo hawapelekwi pelekwi wewe
 
Mbatia kaua nccr yetu.kaiua vibaya mnoo huko vunjo nako ccm tutawakata tu hamna shida
 
uchambuz wa mwandish huyu unachekesha sana yaani ccm iporwe jimbo kama la same mashariki afu waje wapate mosh mjini ambako hawajawah hata kuelekea kupata kura zao zimekuwa za chin sana mara zote kwa mosh mjini
 
ccm ina vichekesho yaani wanyanganywe same majimbo waje wapate moshi vijijini?haiwezekani hata mjini wanaongea tu hawatapata zaidi ya majimbo mawili-lowassa hajaenda moshi vijijini

Lowassa tulikuwa nae Moshi vijijini kata ya Kibosho!
 
James mbatia hata pata kura Vunjo kwa sababu haonekani Vunjo yeye yupo ubavuni Mwa lowassa. Wanavunjo wanauliza kama Kwenye kampeni haonekani akipata ubunge itakuaje? Mbatia hana makazi Vunjo Nyumba anayofikia ni Ya wazazi wake, kiasi cha watu Vunjo kumwita "yahaya". Mbatia hana mke wala Mtoto wana Vunjo wanauliza ataongozaje jimbo la Vunjo na ubachela wake ataenda kustarehe Dar Es salaam. Pia, historia ya baba Yake aliyekuwa akiwatumikisha watu wa Vunjo Kwenye mashamba Yake bila kuwalipa malipo stahiki. Madiwani wa Chadema kumtosa mbatia na kuahidi kumpigia kura Mrema kwa kuwa mbatia anaua Chadema Vunjo kwa kung'ang'ania kuweka madiwani wa Nccr kata zote 16 na kuwanyima Chadema kata 8 kama walivyokibaliana Kwenye ukawa. Wana Vunjo wanajua mbatia anatumika Na Aloyce Kimaro wa Ccm ( mbunge wa Vunjo 2005- 2010) Land Rover hardtop wanazotumia Nccr Kwenye kampeni ni zake. Tunajua Mrema kafunga Kiwanda cha kimaro cha vinywaji na Zile eka 11 alipora ajenge kituo cha radio zimethibitiwa kwa hiyo huu msaada kwa mbatia ni kwa ajili gani, hii ndoa ya ukawa na Ccm Vipi? Wana Vunjo sio wajinga. Wanaona Na wanajiuliza
Aliachana na yule mke wake?!
 
Asirudi,mwehu sana yule!na ubunge wa sketi haoati pia
 
kumbe source gazeti raia mwema? nime elewa

Hata lingekuwa gazeti lolote lile nazidi kusisitiza wanavunjo wasifanye makosa wakamwacha Mbatia kwa ushabiki wowote ule. Mbatia ni jembe la uhakika na ni mtu mwenye msimamo na uwezo mkubwa sana wa kuelewa, kutetea na kutenda mbali ya usomi wa hali ya juu alio nao. Huyu mzee Mrema ni ndumakuwili pandikizi na hajawahi kuwa mpinzani wa kweli na zaidi amezeeka na kuchoka. Asubiri nafasi aliyoahidiwa na Magufuli. Huyu wa ccm bado sana yeye aachwe ale kwanza ujana kwenye ma-night clubs ila silaha anayotishia nayo raia wema anyanganywe hadi atakapojitambua. Moshi mjini ikiwa kuna alieweza kuwaroga na mkalogeka mkiacha kumchagua Jaffary wa chadema maendeleo yote yaliyoletwa na mzee Ndesamburo akishirikiana na Jaffary yatayeyushwa kwa mwaka mmoja tu. Moshi vijijini nanyi nawaasa kuna jembe la chadema mmekabidhiwa hapo nae ni nd.Komu msije kudanganyika mkamwacha kwa ulaghai wa kapero,fulana na upande wa kanga mtajutia uamuzi wenu kwa miaka mitano. Huo ndio wosia wangu kama mzee ninae wafahamu wagombea hao na uwezo walio nao wa kuwatumikia. MABADILIKO UKAWA. UKAWA LOWASSA.
 
Back
Top Bottom