Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ameibuka hadharani na kutoa lawama nzito dhidi ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, akidai kuwa ilihusika moja kwa moja katika mchakato ‘usio halali’ uliomng'oa chamani yeye pamoja na viongozi wengine wa juu wa chama hicho kupitia kikao kilichofanyika mnamo Mei, 2022.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mbatia ameeleza kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kushirikiana na Msajili Msaidizi waliendesha kile alichokiita ni "uvunjaji wa kikatiba wa uongozi wa chama" kwa kuingilia moja kwa moja taratibu za ndani bila mamlaka ya kisheria.
Kwa mujibu wa Mbatia, kikao hicho kilifanyika bila kuwahusisha viongozi wakuu waliokuwa hai na waliokuwepo jijini Dar es Salaam siku ya tukio. Amesema kuwa yeye kama Mwenyekiti halali wa chama hakupewa taarifa ya kikao hicho, wala Makamu Mwenyekiti, wala aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa chama wakati huo.
Mbatia ametumia fursa hiyo kueleza kuwa hatua hiyo sio tu ilivunja taratibu za ndani za NCCR-Mageuzi bali pia ni mfano hatari wa kudhoofika kwa mfumo wa kidemokrasia nchini, ambapo vyombo vya kiserikali vinachukua nafasi ya kufanya maamuzi ya ndani ya vyama.