Mbaroni kwa kutishia kumuua mamaake

Mbaroni kwa kutishia kumuua mamaake

cocobanana

Member
Joined
Nov 2, 2016
Posts
8
Reaction score
6
Juma Janmohammed lakini ye upenda kujiita Fuad Jamal a.k.a Mzee Baba amenaswa uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akisubiri Ku kwea pipa la kuelekea uingereza Huku akijua fika kuwa Ana kesi ya kutishia kumuua mama yake mzazi, ina maana alipoona Huku inakaribia machale yakamcheza Akaona bora akimbie

Ndipo kabla hajafanikiwa kutoroka Maafisa wa jeshi la Polisi nchini wakafanikiwa kumpiga pingu mbele Ya Abiria wenzake
.
Inasemekana eti Mzee baba akaanza Kutokwa na Machozi Kama Mtoto mdogo,
.
Mpaka wakati huu Inasemekana Mzee Baba yupo Polisi Kwa ajili ya mahojiano na alipojaribu kuomba dhamana ilishindikana kutokana na Mtuhumiwa huyo kumiliki Passport mbili Za kusafiria moja ikimtambulisha Kama raia wa uingereza na nyingine ikimtambulisha Kama Raia wa Tanzania
.
Inadaiwa kuwa chanzo cha mgogoro Kati ya mtu na mamaake ni masuala ya Nyumba Nyumba ambapo Bi Mkubwa aliingia mkataba Na mwekezaji flan jina kapuni, kwamba Nyumba aliyokuwa anaimiliki ivunjwe Na kujengwa Ghorofa ambalo chini kuna frames halafu juu kuna makazi ya watu, mchongo ukafanyika Mama akapewa baadhi ya Vyumba kwa makubaliano kwamba baada ya Miaka kadhaa Atamiliki Ghorofa lake lote mwenyewe, basi mama akaamua kuwakabidhi wanae Funguo moja moja, sasa inasemekana Farid akaingiwa na tamaa na kutaka apendelewe zaidi Kwa kupewa Nyumba Zaidi ya moja ndani ya Ghorofa Hilo, hivyo akawa anamlazimisha mama yake Kwa kutishia kumuua kitu ambacho mama yake alikipinga,

Ndipo Jamaa huyo akawa anamtishia kumuua na hii si Mara ya kwanza Siku ya Siku Farid alimvamia mama yake akiwa na kundi la wahuni inasemekana kuwa Walitishia kumuua Mama Kama akikataa kwenda sawa na amri yao, Bahati Nzuri majirani na baadhi ya Ndugu waliskia vishindo na makelele ikabidi wakaingilie Kati na kwenda kumuokoa mama yao, mtuhumiwa na wenzake wakachoropoka ikabidi mama akatoe ripoti Polisi ikafunguliwa kesi na kuanza kuunguruma Ndipo Farid alipoona maji yanamfika shingoni Akaona bora atoroke nchi, Polisi walipopata taarifa ndo wakamnasa airport na kumtia ndani.
.
Nmekutana nayo Whatsap
14607106_568191000048941_88689721747701760_n(1).jpg
 
Ndo madhara ya kuzeekea nyumbani ......mtu miaka 27+ uko kwa baba na mama
 
Ndio tatizo la kutegemea vya home! Jitu zee linashindwa kutafuta vya kwake! Mpaka unamkosesha amani mzazi aliepaswa kukutegemea! Pambaff kabisa!
 
Duh!! Huyu kama ameweza kumfwata mama yake Na kundi la wahuni Na kumtishia kumuua mama yake bas angeweza hata kumuua kweli. Inauma kuona mtoto wako mwenyewe anakufanyia vitendo viovu kama hivo

Bora kawahiwa Sasa kinachomliza n nini Na mambo kayataka mwenyewe

Mungu amtie nguvu huyo mama
 
Ila kwa nature ya wazazi wetu wa kike,ameshaanza kujuta kwanini alitoa taarifa polisi
 
Huyo jamaa zee la miaka kadhaa huko uk hali mbaya anakuja kukaba hom maisha yasonge ni aibu kubwa
 
Shame on him!
(Kama hiyo ndiyo picha yake ,machoni ANAONEKANA kama Teja- mtumia madawa wa kulevya, kwanza kwa umri huo yeye ndiye angekuwa anategemewa na mzazi wake)hivi upo magahribi UK , anafanya nini hadi kuja kugombea nyumba bongo!?AU ni shoga!?
 
Wabeba box wanatia aibu,Rudini tu kama Le mutuz sasa hiv anakula tu bataz na le super mitindiz
 
jianaume kubwa nyambaffuu utakuta anaingilishi nyingiii mademu wanashoboka kumbe pesa hana nyau kabisa na akafie sero
 
Akina MAMA tuna shida jamani! unajitesa kufanya matusi (labda siku hiyo hata hukuwa mwenye mood), unalea mimba, kichanga na hatimaye akiwa mtu mzima anataka kukufanya BUCHA aiseee! huyu kijana sheria mtie nguvuni kama akiwa na hatia
 
Akina MAMA tuna shida jamani! unajitesa kufanya matusi (labda siku hiyo hata hukuwa mwenye mood), unalea mimba, kichanga na hatimaye akiwa mtu mzima anataka kukufanya BUCHA aiseee! huyu kijana sheria mtie nguvuni kama akiwa na hatia
tena wasimuachie
 
Back
Top Bottom