Mbaroni kwa kumbaka mtoto wa miaka 16

Mbaroni kwa kumbaka mtoto wa miaka 16

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,426
changes_to_family_law_ontario-696x465.jpg

DAR ES SALAAM: MKAZI wa Tegeta Machinjioni, Dar es Salaam, Shadrack Myaule (24), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa shtaka la ubakaji.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Joyce Mushi, karani wa mahakama hiyo, Matarasa Hamisi, alidai Desemba 16 na 23 mwaka jana, mshtakiwa alimbaka mtoto mwenye miaka 16 katika eneo la Tegeta Machinjioni, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na Hakimu Mushi alisema kuwa dhamana yake iko wazi na atatakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaotoa bondi ya Sh.milioni 1.

Mshtakiwa alirudishwa rumande kwa kushindwa kukidhi masharti ya dhamana hadi kesi yake itakaposomwa tena Februari 18, mwaka huu.

Wakati huo huo, watu watatu wamepandishwa kizimbani kwa shtaka la kupiga na kujeruhi.

Waliopandishwa kizimbani ni Nicksoni Miti (34), Flora James (39) na Salome Sangali (16) wote wakazi wa Mabibo.

Wakisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Hanifa Mwingira, Mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Credo Rugaju alidai kuwa Julai 7 mwaka jana katika eneo la Mabibo washtakiwa walimpiga Mary Laus kwa kutumia ndoo ya plastiki na kumsababishia majeraha mbalimbali katika mwili wake.

Washtakiwa walikana kutenda kosa hilo na Hakimu Mwingira alisema kuwa dhamana yao iko wazi na kila mshtakiwa atatakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaotoa bondi ya Sh milioni 1.

Washtakiwa walirudishwa rumande kwa kushindwa kukidhi masharti ya dhamana hadi kesi yao itakaposomwa Februari 18, mwaka huu.

Chanzo: Mtanzania
 
Mtoto wa miaka 16??
insane,sheria sometimes hazipo fair kabisa,huyo dogo ukute hako ni kademu kake,pesa ndio zimemtia hatiani,na si sheria wallah,miaka 16 kwa mtoto wa kike Dar is a big mama,pole sana kwa kijana huyu..
 
Kwa nini bond inawekwa kubwa hivyo. Vijana wataozea magerezani/rumande.
 
Huyo anayetuhumiwa kubaka, jumba bovu limemwamgukia yeye...

Siku hizi watoto wa miaka 16 wanafanya mambo ya ajabu kushinda hata watu wazima...

Cc: mahondaw
 
Mtotoo wa miaka 16, huyo mtu mzima kabisa
 
Mtoto wa miaka 16??
insane,sheria sometimes hazipo fair kabisa,huyo dogo ukute hako ni kademu kake,pesa ndio zimemtia hatiani,na si sheria wallah,miaka 16 kwa mtoto wa kike Dar is a big mama,pole sana kwa kijana huyu..

Rape Apologist Alert!
 
Back
Top Bottom