Mbao wadai mwamuzi aliwanyonga

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,569
9,429

BAADA ya kupoteza mchezo wa fainali ya Kombe la FA mbele ya Simba kwa mabao 2-1, wachezaji wa Mbao FC wamemtupia lawama za waziwazi mwamuzi aliyechezesha mechi hiyo, Ahmed Kikumbo kutoka Tanga.

Juzi Jumamosi, Mbao FC ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Simba katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Kilio cha Mbao kwa mwamuzi huyo wa kati ni namna alivyowazawadia penalti Simba dakika ya 118 ambayo Shiza Kichuya alifunga na kufanya matokeo kuwa 2-1 mpaka mwisho, wakidai kwamba hakukuwa na madhambi yaliyofanyika kwenye eneo la hatari.

Beki wa kulia wa timu hiyo, Boniface Maganga, amesema mwamuzi hakuwa makini kwenye uamuzi wake, kwani hakuna mchezaji aliyefanya madhambi kwa kushika mpira kwenye eneo lao la hatari kama alivyodai mwamuzi, jambo ambalo liliwatoa mchezoni.

“Ukiangalia vizuri utagundua kwamba hakuna mchezaji wetu aliyeshika, bali ulimgonga sehemu nyingine katika harakati za kuokoa hatari, lakini tukashangaa mwamuzi anaweka penalti,” alisema Maganga.

Naye kocha wa kikosi hicho, Etienne Ndayiragije, raia wa Burundi, amesema wamekubali matokeo hayo na amewapongeza wachezaji wake kwa kazi kubwa waliyoifanya tangu mwanzo hadi mwisho wa michuano hiyo.

Ikumbukwe kuwa, wakati mwamuzi huyo anaamuru iwe penalti, wachezaji wa Mbao walimvaa na kutaka kumpiga mpaka askari walipoingia uwanjani na kumuokoa hali ambayo ilimfanya hadi Ndayiragije na benchi lake la ufundi kufanya kazi ya ziada ya kuwatuliza ambapo mchezo ulisimama kwa takriban dakika tatu.
 
Mbona Azam Tv walionesha tukio mubashara na wote tulishuhudia mpira ukigonga mkono wa beki wa Mbao bila ubishi kabisa, wanataka kutuambia nini sasa! Ahsante Azam Tv maana kama sio wao hakika ubishi huu usingeisha kamwe kwa jinsi sisi wabongo tulivyo!
 
Hivi Azam walikuwa wanaonyesha mipira miwili kwenye mechi moja.
Penati ilitoka wapi? Muamala wa mpesa ndiyo ulitoa penati isiyokuwepo
 
Yaani inashangaza kweli! zamani nilisikia watu wanabishana na radio mpka inazima lakini sasa kuna watu wanabishana na TV. yaani kitu kiko wazi kabisa lakini mtu anabisha. kama kusoma hujui basi hata kuangalia picha unashindwa. huu si ushabiki bali ni ubishi.
 
Kwa hiyo ni nani amewasema Mbao ikiwa wamenyongwa..? Au hawajafa baada ya kunyongwa..?
 
Angalieni mpira wa ulaya hakuna refa anae toa penalt bado dk 3au NNE mpira kwisha,
 
Ile penalty wangepewa Mbao, Muda huu Simba wangekuwa UN.
Bahati mbaya Simba walikuwa hawashambuliwi. Hadi unafanya madhambi kwenye eneo lako la hatari, ina maana kuna presha kubwa inaelekezwa langoni mwako
 
penati.png
 
Back
Top Bottom