Kila kitu ni mtizamo wako juu ya hicho kitu. Kuna watu wanasema TZ ni nchi ya amani, kuna wengine wanabisha sana, kulingana na tafsiri zao za amani.
Ila kikubwa nilichogundua ni kuwa, ukimpata mwenza mnayerandana kimitizamo, afu na myo wako umpende(mioyo can be very stubborn at times, inamkataa the right person na kung'ang'ania alshabab), basi ndoa ni paradiso ya duniani.
Mtu ambaye unaweza mweleza hata zile worry ambazo ulikuwa hujawahi mweleza mtu, mtu ambaye mna-communicate katika 'a heart to heart level', mind you, sila kila uhusiano una aina hii ya mawasiliano. Kuna mahusiano mabayo mnawasiliana kama chiriku tu, mnaongelea mambo meeeengi, mnaishia kwenye vitu personal, no heart to heart.
Aina hii ya mahusiano, hamna siri, hamna mtu anayejengwa kwao kinyemela, hamna anayemwibia mwenzie hela, sababau kama una shida si utasema.
Ukiamka asubuhi na kukutana na tabasamu lake, uwiii, unapiga tu sala ya kuomba maisha marefu ya pamoja.