MAZURI ya Kikwete ambayo hayajawahi kufanywa na marais waliomtangulia HAYA HAPA

Namkubali sana JK lakini lazima penye dosari tuseme.

Tunajenga daraja kigamboni kwa zaidi ya bilioni 100, barabara ujenzi mabilioni ya kutosha kila mwaka lakini tunashindwa ku dedicate hata bilioni 10 tununue vitanda wagonjwa wanalala chini kwenye hospitali za serikali !!! na vitanda vilivyopo vina kutu na vimechoka mbaya. Mgonjwa analazwa Muhimbili lakini vipimo regency na Agha Khan. Wagonjwa wanagombania vyakula na mapaka Shume Muhimbili. Kama mgonjwa wako amelepelekwa hospitali huna daktari unayemjua ujue imekula kwenu.

Shame shame Mr President!!
 
Ifikie kipindi wabongo tuanze kudai vitu Nchi yetu Ina deserve na sio kuridhika na trivials zinazofanywa na viongozi,ndio maana hatuendelei,Nchi inahitaji Elimu bora na sio majengo mengi ya shule,mradi huu wa DRT umefanywa kwa kuangalia matatizo ya sasa ila sio challenges za mbele,ndio maana sitashangaa miaka mitano au kumi ijayo Rais mwingine ataivunja na kuanzisha project mpya,kwa hiyo ukitaka tu kuangalia vitu alivyofanya waweza kumsifia usiku Mzima,ila swala la kujiuliza ni JE?,hivi vitu ndio tunavyo deserve na ndio tulitegemea Mkuu wetu atufanyie?

una hoja lakini umeshindwa kuitetea na kuijenga sawasawa ili great thinkers wakuelewe. kwani tuna deserve nn zaidi hivi alivyofanya. ( kwa mtazamo wako). kumbuka pia kwamba maendeleo ni vipaumbele. kulikuwa na kipaumbele cha shule za sekondari ambazo ndio hizo zimejengwa kila kata mapungufu yatatatuliwa over time, miundombinu bora ndio daraja ktk kuelekea maisha bora
 
1-+muonnekano+wa+daraja+la+kigamboni.JPG


IMG_9921.jpg
ujenzi wa daraja la kigamboni mwezi july ulikuwa umefikia asilimia 47 kama inavyoonekana kwenye picha
 
Ningefurahi mambo mawili yafuatayo ameyakamilisha kabla ya 2015.
1.Train inachukuwa mzigo wote wa bandari ya Dar na kuhamishia Chalinze,msururu wa malori usionekane tena mjini.
2.DSM tunapata maji ya uhakika
 
Kwa uungwana na ukweli,tukiacha siasa za ki-HARAKATI NA HUSUDA lazma ufike wakati tukiri kwa sauti bila HOFU kwamba kwa kipindi chake JK amefanya mengi MAZURI kwa watanzania.Nimesema tuache UNAFIKI na HUSDA.!Ndiyo banaa..! Mnyonge Mnyongeni Haki Yake Mpeni !
 
Mwenye macho haambiwi tazama,ni kweli JK amefanya mambo mengi sana mazuri,nampongeza sana.Ninachoomba ni aongeze nguvu katika kuvipa nguvu vyama vya upinzani,na kuwapunguzia nguvu polisi,kwani wanatia doa kwa mauji ya kiholela dhidi ya raia wakiwa kwenye mikutano au maandamano!Badala ya kupanmbana na majangili wanaomaliza manyama pori na mafisadi.
 
Ngoja waje wenye degree za matusi wakiongozwa na akina mwita maranya uone mvua ya matusi


Kizuri chajiuza, CCM hatuhitaji vurugu kutekeleza sera zetu

Huna mchango wowote zaidi ya kuumia kwasababu wengine wanamawazo tofautiana nawe. We rofa!!!!
 
Ni ukweli usiopingika, ni miongoni mwa marais wachache Afrika ambao ni wasikivu na wavumilivu. Mapungufu anayo ambayo binadamu wote tunayo. Amefanya mazuri na mabaya, tujivunie mazuri aliyoyafanya, sitegemei kama kuna rais yeyote atakae kuja kuiongoza nchi hii atafanya mazuri tu 100%. Bravo JK
 
Haki za raia na usalama wao vip? tutawawezesha vijana kupata ajira vip hapo?Maisha bora kwa kila mtz vip? mauaji ya tembo na usafirishaji wa twiga ( rasilimali zetu)? katika maraisi kibisa na legelege waliotokea TZ M.Kikwete anaongoza...namchukia kuliko njaa.
 
una hoja lakini umeshindwa kuitetea na kuijenga sawasawa ili great thinkers wakuelewe. kwani tuna deserve nn zaidi hivi alivyofanya. ( kwa mtazamo wako). kumbuka pia kwamba maendeleo ni vipaumbele. kulikuwa na kipaumbele cha shule za sekondari ambazo ndio hizo zimejengwa kila kata mapungufu yatatatuliwa over time, miundombinu bora ndio daraja ktk kuelekea maisha bora

kwa hio kipaumbele kujenga.....mwanza kumejengwa mtambo wa umeme mpya lakini kila siku umeme unakatika sio usiku wa manane au mchana
 
Back
Top Bottom