mazoezi..

sky_haf

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2012
Messages
222
Points
0

sky_haf

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2012
222 0
doctors wetu hutwambia tufanye mazoezi ili tuwe na afya njema. Kwani kufanya mazoezi pia kunapunguza uwezekano wa kupata baadh ya maradh...kama kisukari, moyo na mengneyo..
JF Doctors...kivipi mazoez yanamfanya mtu kuwa na afya njema (what physiological processes occur in the body so as to make it health??)
 

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
16,360
Points
2,000

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
16,360 2,000
Mazoezi husaidia kwanza ku burn calories ambazo mrundikano wake mwilini ni hatari iafya lakini pili husaidia katika kutoa sumu mwilini (in form of jasho) ambazo nyingi ni chumvi, chemicals na oxidants. Lakini kizuri zaidi ni kutanua mfumo wa upumuaji, kutanua mfumo wa mzunguko wa damu na kujenga misuli.
 

Chum Chang

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
1,001
Points
0

Chum Chang

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
1,001 0
Mazoezi ni dawa mbadala wa mwili wa binadamu hata wanyama wengine
Mazoezi ukusaidia kukabiriana na msongo wa mawazo kwenye shida za kibinadamu
Mazoezi husaidia kutatua baadhi ya shida na kuna utofauti mkubwa wa kutatua shida kati anaefanya mazoezi na asiefanya
Faida ni nyingi sana anazopata mtu anaefanya mazoezi na hasara ni nyingi za mtu asie fanya mazoezi
Wacha wengine waje kutupa faida zaidi na mchanganua wao bila kuwasahau wale wazee wa 6 kwa 6
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,281
Points
2,000

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,281 2,000
Ujuwe umuhimu wa kufanya mazoezi

Mwili wako uliumbwa kwa ajili ya kufanya kazi (manual labour) kama vile kusukuma, kuvuta, kubeba, kutembea, kuruka, kuimba, kucheza, kusakata rhumba, kuinama, kuinuka, kukimbia, kukusanya, kupanda (climb) kuwinda nk.
Tunapofanya kazi yoyote kimwili ubongo huweza kutoa aina za kemikali (endocrines) ambazo hutuwezesha kuji-balance na kutupa hisia za kuwa well being.

Unajua kuna watu wabishi inawezekana na wewe msomaji ni mmoja wao, hivi ni lini umefanya zoezi? na kwa nini hufanyi mazoezi?


Huku unajiuliza mbona mwili unanilemea, mbona sijisikii vizuri, mbona stress kila siku? wakati mwingine tunawasumbua madaktari bure kumbe dawa zipo ni wewe kufanya mazoezi.


Ni kweli kufanya mazoezi kutakufanya ujisikia vizuri na lazima ufanye hivyo kwa faida yako, hata hivyo wengi wetu hutumia muda mwingi kufanya kazi ambazo tunakuwa tumekaa tu kwenye kiti kwa muda mrefu bila kuufanyisha kazi

mwili na ikifika weekend unashinda unatazama Tv full speed bila kujishughulisha na manual work.

Pia ukitoka ofisi unaingia kwenye gari hadi nyumbani kama unaishi maisha ya aina hii lazima ufanye mazoezi otherwise unaweza kuharibu afya yako, kitaalamu mazoezi mara mbili kwa wiki muhimu.

Kufanya mazoezi husaidia
kupunguza uzito, kuondoa nyama zembe mwilini, kupunguza mafuta (fat), kubalance blood pressure, pia kisukari.

Kufanya mazoezi (siyo magumu)hukuwezesha wakati wa kulala kuweza kufumba macho haraka na kuingia nchi ya ahadi ya usingizi haraka.
Mazoezi huongeza mental skills.


Ukiwa na afya yenye mgogoro maana yake hata mambo ya sita ka sita yataleta mgogoro hivyo basi fanya mazoezi ili uwe na afya njema na ukiwa na afaya njema maana yake better sex life.

Mwanamke ambaye misuli ya kegel imejikaza anakuwa na wakati mzuri linapokuja suala la sex kuliko Yule ambaye misuli

imelegea na huweza kuwa na misuli iliyokaza kama hufanyi mazoezi, unataka kushinda bahati nasibu wakati hukucheza, thubutu!


Na mwanaume ambaye anafanya mazoezi ni hivyo hivyo atampeperusha kipepeo hadi anapotakiwa kufika.

Kama upo nchi za magharibi summer hiyo inakuja, huna sababu ya kujitetea eti baridi ooh snow nyingi..... nk hukosi sababu!

Na sisi tulio tropics wengi shughuli zetu ni zoezi tosha, ila fanya mazoezi kwa ajili ya kuweka sawa ubongo pia kujiweka social na wengine.

 

sky_haf

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2012
Messages
222
Points
0

sky_haf

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2012
222 0
ahsanteni wakuu,
ili kupata afya njema...kuna uwezekano wa kufanya zoezi aina moja tu, au ni lazima ufanye zaid ya moja.
Mf. Kukimbia tu usifanye jengne...au kuruka tu usifanye jengne???
 

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined
Sep 1, 2011
Messages
3,232
Points
1,195

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined Sep 1, 2011
3,232 1,195
UMHIMU WA MAZOEZI KWA AFYA BORA


Moja ya mahitaji matano (5) mhimu ili kuishi baada ya oksijeni, maji, chumvi, na potasiamu; ni Mazoezi. Mazoezi ni mhimu kwa ajili ya afya zaidi ya kuwa na maumbile ya kuvutia (sex body), burudani au kitu kingine chochote.


Watu wengi hufuatilia kuhusu chakula tu, hata kama utakula vizuri vipi bila mazoezi mlo haujakamilika, kwa hiyo mazoezi ni mhimu kwa yeyote kama ilivyo kwa maji au chakula.


Zifuatazo ni moja ya sababu mhimu za kufanya mazoezi kwa afya bora na maisha marefu bila maumivu:
1. Mazozi yanasaidia kutanua mifumo ya mishipa ya damu ndani ya tishu za mishipa na hivyo kuzuia shinikizo la juu la damu (hypertension).
2. Mazoezi yanatengeneza mishipa mingi, hivyo kuzuia mishipa kutumika kama chanzo cha nishati.
3. Mazoezi yanasisimua kazi za vimeng'enya (enzymes) katika kuchoma mafuta ili kuzarisha nguvu kama mahitaji ya kudumu ya shughuri za mishipa.


Unapofanya mazoezi, unabadili chanzo cha nguvu kwa matumizi ya mishipa toka kutumia nguvu itokanayo na sukari na kutumia nguvu inayotokana na mafuta inayojihifadhi yenyewe kwenye mishipa hivyo kuepukana na unene na uzito kupita kiasi.
4. Mazoezi yanafanya uunguzwaji wa mishipa kama nguvu ya ziada toka kwenye asidi amino ambazo pengine zingefikia usawa wa kuwa sumu. Asidi amino zinapokuwa zaidi ya usawa wake wa kawaida kama matokeo ya kutofanya mazoezi, baadhi ya asidi amino zinaweza sababisha uharibifu mkubwa na kuzimaliza baadhi ya asidi amino mhimu. Baadhi ya hizi asidi amino mhimu zilizomalizwa, zinahitajika daima na ubongo ili kuzarisha transmita nyurolojia zake, ndiyo maana mazoezi huongeza akili.
5. Mishipa bila mazoezi inapotea, matokeo yake sehemu ya akiba ya madini ya zinki na vitamini B6 pia inapotea. kufikia kiwango fulani cha upotevu huo, kutapelekea matatizo ya akili na kuvurugika kwa saikolojia.
6. Mazoezi yanapunguza damu yenye sukari kwa wenye kisukari na hivyo kupunguza mahitaji yao ya insulini na matumizi ya dawa.
7. Mazoezi yanalilazimisha Ini kuzarisha sukari toka mafuta ambayo linayahifadhi au toka mafuta yaliyomo katika mzunguko wa damu.
8. Mazoezi yanasababisha urahisi wa kukunjana kwa makutano ya mifupa (joints).
9. Mishipa ya miguu inafanya kazi kama moyo wa pili!, Inapokunjana na kulegea wakati tunatembea, miguu inahimili nguvu ya mvutano. Inaisukuma kwenda mfumo wa vena damu iliyokuwa imepelekwa miguuni. Sababu ya shinikizo lake na mwelekeo mmoja wa plagi, damu ya miguuni kwenye vena inasukumwa juu dhidi ya nguvu ya mvutano kutokana na kukunjana kwa mara kwa mara kwa mishipa ya miguu. Hivi ndivyo mishipa ya miguu ifanyavyo kazi kama moyo wa pili katika mfumo wa vena mwilini. Hii ndiyo thamani ya mazoezi ambayo watu wengi hawaijui.
10. Mazoezi yanaimarisha mifupa ya mwili na hivyo kuzuia ugonjwa wa mifupa (osteoporosis).
11. Mazoezi yanaongeza uzarishaji wa homoni zote mhimu na hivyo kukuongezea uwezo wa kushiriki tendo la ndoa (positive sex libido).


Unapotembea kwa miguu bila kusimama mwendo wa lisaa limoja, unakuwa umeiamusha kemikali inayounguza mafuta mwilini (lipase) kuchoma mafuta kwa masaa 12, hivyo kama mtu atatembea lisaa limoja asubuhi na lingine jioni, atakuwa ameiamusha kemikali hiyo kufanya kazi kwa masaa 24, na kwa faida ya ziada kemikali hiyo huzisafisha pia taka za helemu (cholesterol) kwenye damu.


Hivi ndivyo ilivyo rahisi kupunguza uzito na unene bila nguvu wala gharama yeyote!. Anza leo, tembea saa moja kutoka kituo A mpaka kituo B bila kupumzika asubuhi na jioni, baada ya wiki mbili pima tena uzito wako kuona namna ulivyofanikiwa kwa muda huo na muda gani uwekeze tena kumaliza tatizo hili linalosumbuwa watu wengi kote duniani.


Mazoezi yafuatayo ni mazuri sababu ya thamani yake ya baadaye na hayasababishi maumivu kwenye maungio, nayo ni; kutembea, kuogelea, baiskeli, tenisi, gofu, kukwea, kudansi na kadharika.

Nyumbani | maajabuyamaji.net
 

Forum statistics

Threads 1,392,964
Members 528,761
Posts 34,123,656
Top