Maziwa Ya Ngombe Arusha/Moshi

bbenedict

Member
Joined
Jun 30, 2013
Posts
91
Reaction score
7
Habari Zenu Wakuu,mm Ni Mama Anaemiliki Ngombe Zaidi Ya 1000 Nje Ya Mji Huko Monduli.
Natafuta Tenda Ya Kuwauzia Watu Maziwa Ya Jumla Kwa Bei Nafuu Kabisa Ilimradi Uwe Na Usafiri Wa Kufuata Mwenyewe.
Nina Uwezo Wa Kutengeneza Lita 300 Hadi 500 Kwa Siku.
Watu Wanaoishi Mji Wa Mto Wa Mbuu Pia Mnakaribishwa.Maziwa Ni Fresh Na Hayachanganyiwi Maji.
0756597108 Ndo Namba Yangu.Karibuni
 
bbenedict hongera kwa ufugaji wa ng'ombe wa maziwa.

Napenda kukupa ushauri mzuri juu ya ufugaji wa ng'ombe. Idadi ya ng'ombe ulio nao ni wengi sana, sijui kuwalisha inakuwaje kipindi cha kiangazi. Ukipiga mahesabu, ng'ombe wa maziwa ulio nao 1000 ukigawa kwa lita 500 za maziwa, utapata kuwa kila ng'ombe anazalisha lita 2 tu za maziwa kwa siku. Hiki ni kiwango kidogo sana, inaelekea ng'ombe wako ni wa asili ya kimasai. Ushauri wangu kwako punguza idadi ya mifugo kwa kuuza nusu ya ng'ombe wako. Ukiuza ng'ombe 500 kwa shilingi 500,000/= utapata mtaji wa shilingi 250,000,000/= ambazo zinatosha kununua mtambo mdogo wa kufungasha maziwa kwenye mifuko.

Uza tena ng'ombe 100 x 500,000/= utapata shilingi 50,000,000/= nenda Kenya kwenye mashamba makubwa ya ng'ombe wa kisasa ya Kabete nunua ng'ombe 25 wa maziwa kwa shilingi 2,000,000/= ambao wana uwezo wa kutoa maziwa hadi lita 20 kwa siku kwa ng'ombe mmoja. Baada ya muda ng'ombe hawa wakianza kuzalina utakuwa na kundi kubwa la ng'ombe bora wa maziwa, ambao watakupatia kiwango kikubwa cha maziwa.

Kwa maziwa uliyo nayo sasa hivi tembelea viwanda hivi mjini Arusha na Kilimanjaro vinavyo nunua maziwa kwa wingi.

  1. TDL New Northern Creamaries - Arusha
  2. International Dairy Product - Arusha
  3. Arusha Dairy Company - Arusha
  4. Nronga Women - Kilimanjaro
  5. West Kilimanjaro - Kilimanjaro
  6. Mboreni Women - Kilimanjaro
  7. Marukeni - Kilimanjaro
  8. Ng'uni Women - Kilimanjaro na
  9. Kalali Women - Kilimanjaro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…