Maziwa ya mama huanza kutoka Lini baada ya Kujifungua? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maziwa ya mama huanza kutoka Lini baada ya Kujifungua?

Discussion in 'JF Doctor' started by ZionTZ, Jun 12, 2012.

 1. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2012
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Siku chache baada ya kujifungua mwili wako utaanza kutoa maziwa ya awali(colostrum).Kwa baaadhi ya wanawake maziwa haya huwa mazito na kuwa na rangi ya njano, Kwa wengine ni mepesi na huwa ya maji maji.Maziwa haya ya awali hulinda mwili. Mfano huzuia bacteria na huimarisha kinga ya mwili, hivyo ni muhimu sana kwa mwanao tofauti na maziwa mengine ambayo si ya mama.Maziwa haya hutiririka taratibu na hii humsaidia mwanao kujifunza jinsi ya kunyonya huku akipumua na kumeza maziwa.
  [​IMG]Baadaya siku 3 hadi 4 za kunyonyesha, matiti yako yatazidi kuwa magumu kadri maziwa ya awali yanavyozidi kubadilika na kuwa maziwa ya kawaida.Maziwa hayo yatabadilika ndani ya siku 10 hadi 14 za mwanzo na kuwa maziwa kamili.
  Katika kipindi hiki kiwango cha maziwa kitaongezeka ili kukidhi mahitaji ya mwanao.Kiwango cha maziwa hutegemeana na jinsi unavyochochewa kwa jinsi unavyonyonyesha.Hii inamaanisha kwamba mwanao anaponyonya maziwa mengi, mwili pia hutoa maziwa mengi zaidi.
  Wanawake waliojifungua kwa njia ya operesheni, inaweza kuchukua muda mrefu maziwa yao kuongezeka. Wakati mwingine bila sababu yoyote inaweza kuchukua siku chache maziwa kuanza kutoka. Hili ni jambo a kawaida kabisa na hutokea pasipo sababu yoyote lakini hakikisha unamwambia daktari kuhusiana na suala hili.Ingawa watoto hawatahitaji chochote zaidi ya maziwa ya awali(colostrums) siku chache baada ya kuzaliwa daktari aatakushauri kuhakikisha kwamba mtoto anapata maziwa ya kutosha ikiwa na pamoja na kumuweka motto katika matiti yako kila baada ya masaa mawili hadi matatu.
  Endapo maziwa hayajatoka siku tatu baada ya kujifungua unaweza kuongea na daktari wako kuhusu kumpa maziwa mengine kwa muda (hadi hapo maziwa yatakapotoka) ili mwanao apate lishe ya kutosha na asipoteze uzito bila sababu.
  Usiogope endapo mwanao atapungua uzito siku za mwanzoni.Watoto wengi hupungua uzito hadi kwa asilimia 7% siku chache baada ya kuzaliwa.

  [h=2]Ni wakati gani naweza anza Kunyonyesha?[/h] Ikiwezekana jaribu kuanza kunyonyesha saa moja baada ya kujifungua.Watoto wengi huanza kunyonya hata bia kufundishwa.Baada ya kuamka na kuchangamka motto mchanga utumia muda mwingi kulala kwa kiwango cha angalau masaa 24 hivi.Hivyo itakuwa vigumu zaidi kumuona akitaka kunyonya saa chache baada ya kuzaliwa.
  Hata kama mtoto wako hataki kunyonya ukianza mapema kumnyonyesha itakusaidia wewe na mwanao kujizoeza katika suala zima la kunyonyesha
  Inaweza kuchukua muda kwa mwanao kujua kunyonya vizuri.Lakini mwanao anatakiwa kunyonya akiwa amepanua mdomo na kuingiza sehemu nyeusi ya titi mdomoni(asiingize chuchu peke yake mdomoni).Endapo mwanao atasinzia wakati ananyonya jaribu kumuamusha kwa kumtekenya miguuni au kumvua nguo.Pia unaweza kumpigia kelele na kumvalisha nepi akiwa ananyonya.
  Ili kusaidia kuzoea haraka jaribu kunyonyesha kila baada ya masaa matatu hata wakati wa usiku.Katika hospitali nyingi unaweza kuomba ubaki na mwanao chumbani.Kwa akina mama wanaotaka kupumzika siku chache baada ya kujifungua, mwanao anaweza kulala na wauguzi wakati wa usiku na kuwaomba wakuletee mwanao kipindi cha kumnyonyesha.

  [h=2]Je naweza kumnyonyesha mwanangu kwa kutumia chupa?[/h] Kama uko tayari kumnyonyesha mwanao hakuna haja ya kutumia chupa vinginevyo kuwe na sababu ya lazima sana kufanya hivyo.Mwanzoni ni muhimu kumzoesha mwanao kunyonya bila kutumia chupa.Baadhi ya wataalamu wanasema kwamba ukianza kutumia chupa mapema zaidi-kabla hajazoea kunyonya titi-anaweza kushindwa kunyonya na anaweza kupendelea chupa kuliko kunyonya titi.Hata hivyo watoto wengine huweza kunyonya kwa kutumia njia zote mbili.

  [h=2]Je nitajuaje kama mwanangu anataka kunyonya?[/h] Ingawa baadhi ya akina mama wanadhani kwamba kulia ni dalili ya njaa, kulia ni dalili ya baadae sana.Unatakiwa kujaribu kumnyonyesha kabla mwanao hajapata njaa kali kiasi cha kukata tamaa na kuwa vigumu kumtuliza.
  Dalili zinazoonyesha kwamba watoto wana njaa ni pamoja na;

  • Kugeuza kichwa huku na huko
  • kuachama
  • kuweka mikono mdomoni
  • Kukunja mdomo kama anayetaka kunyonya
  • kujinyoosha
  • kujisogeza karibu na matiti mama

  Imeandaliwa na Dr.Raymond Bandio(MD).

  kwa maelezo zaidi na kuuliza maswali na kujibiwa kitaalam tembelea Wanetu.com :: Elimu kuhusu Ujauzito na Uzazi, Malezi na makuzi ya watoto, Afya ya watoto, Saikoljia, Tabia na Haki za Watoto
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Asante kwa somo zuri.
  Kwa nyongeza tu, kama maziwa ya mama yanachelewa kutoka unaweza kunywa uji, mtori mwepesi ama chai yenye pilipili manga. It works like magic.

  Kama mama amezaa kwa operation, maziwa yaweza kuchelewa kutoka hadi hapo atakapoanza kula.
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  na mnyonyeshe mtoto maziwa ya mama tu kwa miezi 6 bila kumpa vyakula vingine.
   
 4. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kongosho my dear kungwi hiyo ya miezi 6 kwa sasa ni ngumu kutokana na hali ya maisha, but at most miezi mitatu inatosha, then anza kumkamulia kwa mashine ya kushinda nayo mchana ikiwezekana mengi ili yakute utakaporudi, au changanya na ya ng'ombe. ni best by far kuliko ya kopo!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nawashukuru wana JF kwa masomo mbalimbali yanayotolewa na wataalamu wetu humu ndani likiwemo somo la leo. Nina swali. Kama mwanamke amejifungua halafu maziwa hayatoki Je kwa mtoto aliyezaliwa ambaye ana siku moja je haiwezi kumletea shida mtoto? Maana hata mama yake akijaribu kumnyonyesha bado hayatoki. Msaada tafadhali
   
 6. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nanukuu: "Endapo maziwa hayajatoka siku tatu baada ya kujifungua unaweza kuongea na daktari wako kuhusu kumpa maziwa mengine kwa muda (hadi hapo maziwa yatakapotoka) ili mwanao apate lishe ya kutosha na asipoteze uzito bila sababu.
  Usiogope endapo mwanao atapungua uzito siku za mwanzoni.Watoto wengi hupungua uzito hadi kwa asilimia 7% siku chache baada ya kuzaliwa." Mwisho wa kunukuu.

  Je mtoto anaweza kuvumilia siku zote tatu bila kunyonya? au kuna njia mbadala?
   
 7. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu cacico, ni kwa miezi sita ndiyo ifaapo kumpatia chakula kingine(pamoja na maziwa ya mama)...wengi hufanya hivyo "kimakosa" hasa kutokana na kutingwa na shughuli ..lakini maziwa pekee kama chakula kwa mtoto(EBF) inapaswa kuwa miezi sita unless ana matatizo ya kiafya na hivyo kuzingatia hilo kupunguza muda wa kumnyonyesha mtoto.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. M

  Mzee Mwalubadu Senior Member

  #8
  Aug 6, 2015
  Joined: Jun 25, 2015
  Messages: 179
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakuu heshima sana,

  Kama inavyojieleza, mtoto wa mdogo wangu anashindwa kunyonya kutokana na mamake kushindwa kutoa maziwa.

  Amezaliwa juzi na hajawahi kunyonya, ikabidi walazimishe kukamua yakatoka kidogo. Ndo wakagundua si kwamba mtoto hataki kunyonya isipokuwa maziwa ya mama hayatoki so anashindwa kuyavuta titi likiwa mdomoni.

  Hivi sasa daktari amewaambia wampe maziwa ya unga ya lactogen ambapo binafsi sipendi vyakula vya viwandani kwa watoto.

  Tafadhari mwenye ushauri zaidi anisaidie.
   
 9. l

  limi Senior Member

  #9
  Aug 6, 2015
  Joined: Jun 8, 2013
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ampe tu hayo aliyoshauriwa na daktari for da tym being mpaka mama atakapoanza kutoa maziwa.....
   
 10. n

  ndimgayashida Member

  #10
  Aug 6, 2015
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mpeni huyo mama uji wenye pilipili manga lakin pia muomben Mungu amfanyie wepesi
   
 11. M

  Mzee Mwalubadu Senior Member

  #11
  Aug 6, 2015
  Joined: Jun 25, 2015
  Messages: 179
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Thanking you Mkuu.
   
 12. M

  Mzee Mwalubadu Senior Member

  #12
  Aug 6, 2015
  Joined: Jun 25, 2015
  Messages: 179
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Shukrani sana
   
 13. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2015
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,548
  Likes Received: 1,307
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni kawaida kwa wadada ambao ndio Mtoto wa kwanza. Ila anywe uji wenye pilipili manga kwa wingi maziwa yatatoka ni suala LA muda tu. Lakini Mtoto Lazima ale ashibe ndio maana anatakiwa kupewa lactogen
   
 14. n

  ndimgayashida Member

  #14
  Aug 6, 2015
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Atakua sawa tu msijali...bila kusahau huyo mama ale vtu vya maji maji sana...vimiminika namaanisha...ninamuweka kwnye maombi pia...Mungu atamsaidia msijali
   
Loading...