Mazishi ya Kaweesi (Assistant IGP-Uganda) Live UBC now

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
44,158
82,245
Kamanda Kaweesi aliyepigwa risasi juzi Uganda anazikwa leo- UBC live now!. Misa inaendelea sasa. Kila mmoja ameguswa na anahuzunika. KUMBE KUFA KUNAHUZUNISHA!! Tunawapa pole sana wafiwa na askari polisi wote Tanzania na duniani kwa ujumla.

Wakati wa kifo huwa ni muda wa kutafakari matendo yetu. Wapendwa polisi wetu tafakali matendo yenu mnapofanya kazi zenu. Ukiacha waalifu ambao mna haki ya kuwashughulika ndani ya mipaka ya kazi yenu na sheria, upande wa mnavyo watreat wapinzania si sawa!

Jitafakari kazi zenu! Naona Uganda umati mkubwa wa watu wanamsalia marehemu. Nimefikiri mbali sana hapa kwetu mnavyowapiga waandamanaji, wanafunzi juzi etc, mfano juzi Arusha mahakamani, was there a need to do that? Jitafakari!
 
Umeongea ukweli sana mleta maada. Katika Africa polisi wamekuwa adui wa wananchi badala ya kuwa rafiki! Matendo ya polisi wetu yanahuzunisha na kuumiza. Ndo maana kama huna moyo wa ubinadamu hawa watu unaweza hata kuwanyima maji ya kunywa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom