Mazishi ya Inkosikasi "MADIBA" ........!!!

kisugujira

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
773
195
WanaJF,

Leo ni siku ya kuuweka mwili wa mtu wa watu, simba wa Afrika mwenye huruma hata kwa adui zake mzee Nelson Mandela katika nyumba ya milele. ITV kupitia BBC World News wanaonyesha matukio yote yanayoendelea huko Kunu katika kijiji alichozaliwa shujaa huyu. Watu ni wengi sana kutoka sehemu mbalimbali!

Mtu huyu hakutaka makuu kama rafiki yake kipenzi Nyerere kwani barabara inayokwenda nyumbani kwake si ya lami kama ilivyokuwa ya kwenda Butiama kabla ya kifo cha Nyerere!

Nenda Mandela nenda, kamwambie Nyerere ule ufa na ubaguzi aliokuwa anaukemea, sasa hivi ni mkubwa mno! Mmomonyoko wa maadili katika utumishi wa umma ni mkubwa sana!
 

Swat

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,199
2,000
Naangalia ETV ya South Africa live. Hatimaye yule mfasili Magumashi wa lugha ya walemavu wa kusikia ameondolewa na badala yake yupo mdada mmoja. Yule magumashi nadhani alikua ni mvuta bangi mahili ndio maana alikua anaona nyota,mwezi na malaika vinamjia!
 

kisugujira

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
773
195
Naangalia ETV ya South Africa live. Hatimaye yule mfasili Magumashi wa lugha ya walemavu wa kusikia ameondolewa na badala yake yupo mdada mmoja. Yule magumashi nadhani alikua ni mvuta bangi mahili ndio maana alikua anaona nyota,mwezi na malaika vinamjia!

Si unajua tena kuna watu wanatumia nyota za wenzao kupata umaarufu! Madiba alikuwa nyota na atakuwa nyota hata siku zijazo!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom