Mazingaombwe ya Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania!

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,181
1,579
Kama si mazingaombwe ni nini basi?

Mwaka 1992 wanasiasa hawa-hawa walikubali kupokea demokrasia ya vyama vingi ilihali wanatambua fika kuwa hakuna tume huru ya uchaguzi.

Mwaka 1995 bila tume hiyo!
Mwaka 2000 bila tume hiyo!
Mwaka 2005 bila tume hiyo!
Mwaka 2010 bila tume hiyo!
Mwaka 2015 bila tume hiyo!
Mwaka 2020 bila tume hiyo!

Na kila mwaka wa uchaguzi watu hawa wamekuwa wakilalamika kuibiwa kura ingawa tena uchaguzi ukiisha hawachukui hatua zozote za kudai tume guru!
Daima wao husubiri wakati uchaguzi wenyewe na kutuambia sisi laia tulinde kura zetu!

Sasa basi bila tume huru ya uchaguzi, Mungu akipenda nifike mwaka 2020, mimi, nimeamua nitairinda kura yangu nyumbani na si vituoni kama awali.
Nimechoka na mazingaombwe ya tume huru ya uchaguzi Tanzania.
 
Nijuavyo mimi NEC na ZEC zote ni Tume Huru za Uchaguzi.

Kama lengo ni kuonyesha NEC au ZEC sio huru, ungetusaidia sana kwa kuonyesha ili tume iwe huru, inapaswa iweje kisha kuonyesha jinsi NEC na ZEC jinsi ambavyo sio huru.

Mimi kwa maoni yangu, NEC na ZEC zote ni tume huru, ila kufuatia kushiriki kikamilifu katika chaguzi 5 tangu 1995, nimegundua tatizo ni the playing field kwenye the game of politics is not level. Nyingi ya chaguzi zetu ni kugombea kisu huku kuna mmoja ameshika kwenye mpini na mwingine kwenye makali.

Fuatilia hoja kwenye hii mijadala.
TV Program Alert: Msidanywe na Wanasiasa Kuhusu Uchaguzi Mkuu: Ulikuwa Huru na wa Haki!. Shuhudia!

TV Prog. Alert: Tume ya Uchaguzi, NEC, Yajibu Hoja za JF Kuhusu Uchaguzi Huru na Wa Haki!

Paskali
 
Nikutafuta Sababu tu
Nchini Kenya Waliunda tume huru
vipi ilikuwaje
mbona walishindwa na wakaenda kupinga matokeo .
Upinzani wa Tanzania kuingia Ikulu Bado sana
upinzani huu wa Mbowe na Kubenea!!
Hawa wanafiki wanao kula Matapishi yao
waingie ikulu!!
Upinzani hauna Sera hauna Hoja zaidi ya Matukio,
Itakuwa laana kwa mungu hawa kuingia ikulu
labda upinzani kizazi kijacho
 
Nijuavyo mimi NEC na ZEC zote ni Tume Huru za Uchaguzi.

Kama lengo ni kuonyesha NEC au ZEC sio huru, ungetusaidia sana kwa kuonyesha ili tume iwe huru, inapaswa iweje kisha kuonyesha jinsi NEC na ZEC jinsi ambavyo sio huru.

Mimi kwa maoni yangu, NEC na ZEC zote ni tume huru, ila kufuatia kushiriki kikamilifu katika chaguzi 5 tangu 1995, nimegundua tatizo ni the playing field kwenye the game of politics is not level. Nyingi ya chaguzi zetu ni kugombea kisu huku kuna mmoja ameshika kwenye mpini na mwingine kwenye makali.

Fuatilia hoja kwenye hii mijadala.
TV Program Alert: Msidanywe na Wanasiasa Kuhusu Uchaguzi Mkuu: Ulikuwa Huru na wa Haki!. Shuhudia!

TV Prog. Alert: Tume ya Uchaguzi, NEC, Yajibu Hoja za JF Kuhusu Uchaguzi Huru na Wa Haki!

Paskali

Mwenye Akili atakuelewa
 
Kama si mazingaombwe ni nini basi?

Mwaka 1992 wanasiasa hawa-hawa walikubali kupokea demokrasia ya vyama vingi ilihali wanatambua fika kuwa hakuna tume huru ya uchaguzi.

Mwaka 1995 bila tume hiyo!
Mwaka 2000 bila tume hiyo!
Mwaka 2005 bila tume hiyo!
Mwaka 2010 bila tume hiyo!
Mwaka 2015 bila tume hiyo!
Mwaka 2020 bila tume hiyo!

Na kila mwaka wa uchaguzi watu hawa wamekuwa wakilalamika kuibiwa kura ingawa tena uchaguzi ukiisha hawachukui hatua zozote za kudai tume guru!
Daima wao husubiri wakati uchaguzi wenyewe na kutuambia sisi laia tulinde kura zetu!

Sasa basi bila tume huru ya uchaguzi, Mungu akipenda nifike mwaka 2020, mimi, nimeamua nitairinda kura yangu nyumbani na si vituoni kama awali.
Nimechoka na mazingaombwe ya tume huru ya uchaguzi Tanzania.
Mkuu Wanasiasa wa upinzani nchini Hawajitambui na hawajui wanahitaji nini na nini wanatakiwa kufanya kupata matarajio yao. Hawa ni kuwavumilia tu sababu lengo lao kubwa ambalo ni FEDHA wanalitimiza kwa mafanikio makubwa ndio maana mavitu ya msingi HAYAWAHUSU ila huwa wanazungumzia kinafiki kuwapumbaza wafuasi wao.
 
Tatizo ni umasikini...watu wanakuwa waoga hasa vijijini...Majeshi nayo yanatumika sana kupelekea watu waichague CCM..media nazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kutuonyesha mavita na mauwaji kama ya Kimbali.CCM mkichoka kuongoza tuambieni....
 
Nijuavyo mimi NEC na ZEC zote ni Tume Huru za Uchaguzi.

Kama lengo ni kuonyesha NEC au ZEC sio huru, ungetusaidia sana kwa kuonyesha ili tume iwe huru, inapaswa iweje kisha kuonyesha jinsi NEC na ZEC jinsi ambavyo sio huru.

Mimi kwa maoni yangu, NEC na ZEC zote ni tume huru, ila kufuatia kushiriki kikamilifu katika chaguzi 5 tangu 1995, nimegundua tatizo ni the playing field kwenye the game of politics is not level. Nyingi ya chaguzi zetu ni kugombea kisu huku kuna mmoja ameshika kwenye mpini na mwingine kwenye makali.

Fuatilia hoja kwenye hii mijadala.
TV Program Alert: Msidanywe na Wanasiasa Kuhusu Uchaguzi Mkuu: Ulikuwa Huru na wa Haki!. Shuhudia!

TV Prog. Alert: Tume ya Uchaguzi, NEC, Yajibu Hoja za JF Kuhusu Uchaguzi Huru na Wa Haki!

Paskali
Mbona Luvuba wakati anakabidhi ripoti ya uchaguzi alizungumzia tume huru?
 
Mayalla,

huko ni kuendekeza njaa au nini?

Kwa mtu muelewa kama wewe; kuthubutu kuziita NEC na zec kuwa ni tume huru!!
Yaani haya ndiyo mazingaombwe yenyewe ninayoyazungumzia.

Labda nikuulize maswali kidogo.

1) Wenyeviti wa tume hizi ni wateule wa nani?
2) Nani ni mwakilishi wa vyama ndani NEC?
3) Kama zec ni tume huru kwanini ilifuta uchaguzi ilioona ccm inashindwa kwa kisingizio cha kuwa na mapungufu?

Upi sasa ni uchagizi usio na mapungufu tangia tuanze mfumo wa vyama vingi nchini, na mbona ccm ikishinda hatujawahi kuona matokeo yakifutwa kwa sababu ya mapungufu?

Kama si mazingaombwe ni nini basi?

Mwaka 1992 wanasiasa hawa-hawa walikubali kupokea demokrasia ya vyama vingi ilihali wanatambua fika kuwa hakuna tume huru ya uchaguzi.

Mwaka 1995 bila tume hiyo!
Mwaka 2000 bila tume hiyo!
Mwaka 2005 bila tume hiyo!
Mwaka 2010 bila tume hiyo!
Mwaka 2015 bila tume hiyo!
Mwaka 2020 bila tume hiyo!

Na kila mwaka wa uchaguzi watu hawa wamekuwa wakilalamika kuibiwa kura ingawa tena uchaguzi ukiisha hawachukui hatua zozote za kudai tume guru!
Daima wao husubiri wakati uchaguzi wenyewe na kutuambia sisi laia tulinde kura zetu!

Sasa basi bila tume huru ya uchaguzi, Mungu akipenda nifike mwaka 2020, mimi, nimeamua nitairinda kura yangu nyumbani na si vituoni kama awali.
Nimechoka na mazingaombwe ya tume huru ya uchaguzi Tanzania.
 
Nijuavyo mimi NEC na ZEC zote ni Tume Huru za Uchaguzi.

Kama lengo ni kuonyesha NEC au ZEC sio huru, ungetusaidia sana kwa kuonyesha ili tume iwe huru, inapaswa iweje kisha kuonyesha jinsi NEC na ZEC jinsi ambavyo sio huru.

Mimi kwa maoni yangu, NEC na ZEC zote ni tume huru, ila kufuatia kushiriki kikamilifu katika chaguzi 5 tangu 1995, nimegundua tatizo ni the playing field kwenye the game of politics is not level. Nyingi ya chaguzi zetu ni kugombea kisu huku kuna mmoja ameshika kwenye mpini na mwingine kwenye makali.

Fuatilia hoja kwenye hii mijadala.
TV Program Alert: Msidanywe na Wanasiasa Kuhusu Uchaguzi Mkuu: Ulikuwa Huru na wa Haki!. Shuhudia!

TV Prog. Alert: Tume ya Uchaguzi, NEC, Yajibu Hoja za JF Kuhusu Uchaguzi Huru na Wa Haki!

Paskali

Ukiangalia kijuu juu, NEC na ZEC ni huru lakini kiuhalisia siyo huru! Kutokana na mfumo wa kuendesha chaguzi ulivyo nchini, sio NEC (au ZEC) pekee wanaodhibiti na kuratibu mchakato mzima wa uchaguzi. Kwa mfano wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo ni wakurugenzi wa halmashauri/miji/majiji. Kinadharia, wakati wa mchakato wa uchaguzi hawa maofisa wanapashwa kupokea maelekezo kuhusiana na masuala ya uchaguzi kutoka NEC tu. Lakini kiuhalisia sivyo mambo yalivyo!

Tumeona na kushuhudia mara nyingi wagombea wa upinzani wa ubunge au udiwani wakishinda uchaguzi bila kuwepo kwa kasoro zozote lakini matokeo yakacheleweshwa kutangazwa bila sabaubu zozote. Hakika katika mazingira kama haya, sio tume inayotoa maelekezo ya kuchelewesha kutangaza matokeo; ni mamlaka nyingine! Uhuru wa tume uko wapi hapo?

Tumeona na kushuhudia vituko vikifanywa na jeshi la polisi na hata JWTZ wakati wa uchaguzi venye lengo la kutisha wapiga kura. Kwa mfano kuna mantiki gani ya kupitisha mitaani magari ya washawasha yanayopiga ving'ora vya kuashiria hali ya hatari siku ya kupiga kura? Ni nani anayeamua haya hafanyike na yafanyike maeneo gani? Hakika siyo tume. Na kwa taarifa yako haya magari hayapitishwi sehemu ambazo chama tawala kina uhakika wa kushinda. Uhuru wa tume uko wapi hapo?

Pia mwaka 2010 siku moja kabla ya uchaguzi mkuu aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ wakati huo, Gen. Shimbo, alitoa taarifa ya vitisho kwa wapiga kura kuhusiana na uchaguzi. Kwanza ni sheria ipi inayoipa JWTZ mamlaka ya kutoa matamko kuhusiana na mambo ya uchaguzi? Kwa vile hakika sio NEC iliyompa hayo maelekezo Gen. Shimbo, basi lazima ukubali kuwa kuna mamlaka nyinyine yenye nguvu zaidi ya tume inayodhibiti na kuratibu shughuli zinazohusiana ya uchaguzi kwa maslahi ya chama fulani kinachoshiriki uchaguzi. Uhuru wa tume uko wapi hapo?

Kadhalika, ukiangalia tu uteuzi wa maafisa wakuu wanaosimamia uchaguzi utaona kuwa tume si huru hata kidogo. Tuachane na mwenyekiti wa tume ambaye kisheria ni lazima awe jaji wa mahakama ya rufaa na ana mkataba maalum wa kazi. Tuje kwa mkurugenzi wa uchaguzi ambaye ndiye mtendaji mkuu wa tume. Huyu anateuliwa na rais (ikumbukwe rais kama mwanasiasa ana maslahi ya moja kwa moja na matokeo yoyote ya uchaguzi) na pia mkurugenzi anaweza "kutumbuliwa" wakati wowote (kama tuliyoona kwa aliyekuwa mkurugenzi wa uchaguzi miezi kadhaa kabla ya uchaguzi mkuu 2015). Uhuru wa tume uko wapi hapo?

Mwisho, tumeona hapa kuwa katika mazingira haya tume ya uchaguzi haiwezi kuwa huru hata kidogo. Na therefore, logically, tume isiyo huru haiwezi kusimamia uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika (free, fair and credible election). Lakini je, mchakato wa uchaguzi nchini, hususan uchaguzi wa urais, una uwazi kiasi gani? Eti kwa mfano, upinzani ulipewa full access ya ufumo wa computer uliotumika kujumlisha kura (vote tallying system) za urais mwaka 2015? Kama hawakupewa, ilikuwa ni kwa maslahi ya nani?
 
Uchaguzi huru ni ule ambao Tume inatakiwa kuwa na wafanyakazi wake mpaka ngazi za chini,hivi unamuweka Mkurugenzi wa Halmashauri/Mkuu wa Wilaya/Mkuu wa Mkoa hawa ndiyo wasimamizi na wateuzi wa wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata,Ubunge na Urais na utegmee Upinznai kushinda bila ugomvi itakuwa ndoto.

Unategeme Rais aliyesema anashangaa kuona Mkurugenzi anayelipwa na serikali kuachia Mgombea wa upinzani anashinda ni maajabu na hataki kusikia tena.

Unautegemea Uchaguzi kuwa huru wakati Jeshi la Polisi linatumia nguvu kubwa kwenye mikutano ya wapinzani,kupiga mabomu ya machozi,kuweka wapinzani ndani sababu tu wanataka kupiga kura chama wanachoona kinafaa.

Tumeona jinsi Lijuakali alivyoswekwa jela kisa kutaka kupiga kura kwenye halmsahuri yake na akaswekwa ndani na polisi,tumeliona kwenye uchaguzi wa Umeya Darisalama hasa pale Kinondoni.

Kama huu ndiyo Uchaguzi huru na Tume huru basi tusahahu maana ya Tume huru ya Uchaguzi.

Hivi Mengi alivyopopolewa mawe na wale wanachama wa Chama Cha Mauaji kuna kiongozi yeyote wa TUME aliyetoa angalizo kwa CCM??

Shemeji yangu mpendwa,usiendelee kutudanganya tumeshakuwa watu wazima hatuhitaji 'PIPI',labda Lumumba wanaweza kuukubali huu uongo.
 
Ukiangalia kijuu juu, NEC na ZEC ni huru lakini kiuhalisia siyo huru! Kutokana na mfumo wa kuendesha chaguzi ulivyo nchini, sio NEC (au ZEC) pekee wanaodhibiti na kuratibu mchakato mzima wa uchaguzi. Kwa mfano wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo ni wakurugenzi wa halmashauri/miji/majiji. Kinadharia, wakati wa mchakato wa uchaguzi hawa maofisa wanapashwa kupokea maelekezo kuhusiana na masuala ya uchaguzi kutoka NEC tu. Lakini kiuhalisia sivyo mambo yalivyo!

Tumeona na kushuhudia mara nyingi wagombea wa upinzani wa ubunge au udiwani wakishinda uchaguzi bila kuwepo kwa kasoro zozote lakini matokeo yakacheleweshwa kutangazwa bila sabaubu zozote. Hakika katika mazingira kama haya, sio tume inayotoa maelekezo ya kuchelewesha kutangaza matokeo; ni mamlaka nyingine! Uhuru wa tume uko wapi hapo?

Tumeona na kushuhudia vituko vikifanywa na jeshi la polisi na hata JWTZ wakati wa uchaguzi venye lengo la kutisha wapiga kura. Kwa mfano kuna mantiki gani ya kupitisha mitaani magari ya washawasha yanayopiga ving'ora vya kuashiria hali ya hatari siku ya kupiga kura? Ni nani anayeamua haya hafanyike na yafanyike maeneo gani? Hakika siyo tume. Na kwa taarifa yako haya magari hayapitishwi sehemu ambazo chama tawala kina uhakika wa kushinda. Uhuru wa tume uko wapi hapo?

Pia mwaka 2010 siku moja kabla ya uchaguzi mkuu aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ wakati huo, Gen. Shimbo, alitoa taarifa ya vitisho kwa wapiga kura kuhusiana na uchaguzi. Kwanza ni sheria ipi inayoipa JWTZ mamlaka ya kutoa matamko kuhusiana na mambo ya uchaguzi? Kwa vile hakika sio NEC iliyompa hayo maelekezo Gen. Shimbo, basi lazima ukubali kuwa kuna mamlaka nyinyine yenye nguvu zaidi ya tume inayodhibiti na kuratibu shughuli zinazohusiana ya uchaguzi kwa maslahi ya chama fulani kinachoshiriki uchaguzi. Uhuru wa tume uko wapi hapo?

Kadhalika, ukiangalia tu uteuzi wa maafisa wakuu wanaosimamia uchaguzi utaona kuwa tume si huru hata kidogo. Tuachane na mwenyekiti wa tume ambaye kisheria ni lazima awe jaji wa mahakama ya rufaa na ana mkataba maalum wa kazi. Tuje kwa mkurugenzi wa uchaguzi ambaye ndiye mtendaji mkuu wa tume. Huyu anateuliwa na rais (ikumbukwe rais kama mwanasiasa ana maslahi ya moja kwa moja na matokeo yoyote ya uchaguzi) na pia mkurugenzi anaweza "kutumbuliwa" wakati wowote (kama tuliyoona kwa aliyekuwa mkurugenzi wa uchaguzi miezi kadhaa kabla ya uchaguzi mkuu 2015). Uhuru wa tume uko wapi hapo?

Mwisho, tumeona hapa kuwa katika mazingira haya tume ya uchaguzi haiwezi kuwa huru hata kidogo. Na therefore, logically, tume isiyo huru haiwezi kusimamia uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika (free, fair and credible election). Lakini je, mchakato wa uchaguzi nchini, hususan uchaguzi wa urais, una uwazi kiasi gani? Eti kwa mfano, upinzani ulipewa full access ya ufumo wa computer uliotumika kujumlisha kura (vote tallying system) za urais mwaka 2015? Kama hawakupewa, ilikuwa ni kwa maslahi ya nani?

Uko sahihi kabisa.Unless tunapata Mwenyekiti huru,na Mkurugenzi huru asiye na Makando kando ya UNAZI.Leo Mkuu wa Majaeshi ni home boy tutarajie tume kuwa huru??

Wakurugenzi wote ni MAKADA wa CCM unataraji UCHAGUZI uwe huru??Pascall ana matatizo ya UKABILA pia atueleze vizuri anatetea nini??
 
Nijuavyo mimi NEC na ZEC zote ni Tume Huru za Uchaguzi.

Kama lengo ni kuonyesha NEC au ZEC sio huru, ungetusaidia sana kwa kuonyesha ili tume iwe huru, inapaswa iweje kisha kuonyesha jinsi NEC na ZEC jinsi ambavyo sio huru.

Mimi kwa maoni yangu, NEC na ZEC zote ni tume huru, ila kufuatia kushiriki kikamilifu katika chaguzi 5 tangu 1995, nimegundua tatizo ni the playing field kwenye the game of politics is not level. Nyingi ya chaguzi zetu ni kugombea kisu huku kuna mmoja ameshika kwenye mpini na mwingine kwenye makali.

Fuatilia hoja kwenye hii mijadala.
TV Program Alert: Msidanywe na Wanasiasa Kuhusu Uchaguzi Mkuu: Ulikuwa Huru na wa Haki!. Shuhudia!

TV Prog. Alert: Tume ya Uchaguzi, NEC, Yajibu Hoja za JF Kuhusu Uchaguzi Huru na Wa Haki!

Paskali
Huitaji kuwa na elimu kubwa kujua kuwa tume zetu sio huru labda kama umeamka Nazo kichwani. Unajua kwanini yule bwana wa nec aliteuliwa kuwa boss tiss?
 
Shemeji Tetty, ni ya kweli haya? .
Mimi nimegeuka mkabila?.
Paskali

Shemeji umenishangaza na comment zako ndiyo sababu nikaweka hiyo je na Pascal naye Ukabila unamsumbua??Maana ukweli wa Tume zetu unazijua,ukianzia na ya Mutungi na kumalizia na ya Kata.
 
Nijuavyo mimi NEC na ZEC zote ni Tume Huru za Uchaguzi.

Kama lengo ni kuonyesha NEC au ZEC sio huru, ungetusaidia sana kwa kuonyesha ili tume iwe huru, inapaswa iweje kisha kuonyesha jinsi NEC na ZEC jinsi ambavyo sio huru.

Mimi kwa maoni yangu, NEC na ZEC zote ni tume huru, ila kufuatia kushiriki kikamilifu katika chaguzi 5 tangu 1995, nimegundua tatizo ni the playing field kwenye the game of politics is not level. Nyingi ya chaguzi zetu ni kugombea kisu huku kuna mmoja ameshika kwenye mpini na mwingine kwenye makali.

Fuatilia hoja kwenye hii mijadala.
TV Program Alert: Msidanywe na Wanasiasa Kuhusu Uchaguzi Mkuu: Ulikuwa Huru na wa Haki!. Shuhudia!

TV Prog. Alert: Tume ya Uchaguzi, NEC, Yajibu Hoja za JF Kuhusu Uchaguzi Huru na Wa Haki!

Paskali
Anko P ule msemo wa kesi ya tumbili kuamuliwa na ngedere unamaana kubwa.

Tume haiwezi kuwa huru ilhali wale wanaoiongoza wana maslahi na upande mmoja.wengi wa watendaji wakuu wa tume kuanzia ngazi ya taifa wana maslahi direct ama indirect na CCM,system iliyomweka Jaji Lubuva kuwa mwenyekiti wa tume ndo hyohyo ilompa u AG na uwaziri huko nyuma unadhani anaweza kwenda against interest za hyo system.Yalofanyika Zanj kila mtu anayajua,Haihitaji kuwa na degree kuona sarakasi zilizopigwa na ZEC katika kufuta uchaguzi halali na kuurudia ili wapate outcome wanayoitaka.Unaposema kuwa playing field haikuwa level moja ya sababu ni mwamuzi kupendelea upande mmoja,hivyo hatuwezi kulaumu leveling field tukaacha kumlaumu mshika kipenga ambaye ndie aliongoza mechi.
 
Back
Top Bottom