kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
ABINGWA wa Afrika, TP Mazembe wameendelea kuisambaratisha Simba baada ya kumnasa Mbwana Samata kwa Shs 150m, sasa wamemgeukia kiungo wa klabu hiyo Patrick Ochan anayetarajia kuondoka wiki ijayo kwenda DR Congo kwa majaribio.
Hata hivyo habari zilizopatika jana kutoka Lumbushashi zimeeleza kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Uganda tayari ameshaanza majaribio na Mazembe.
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyanga 'Kaburu' alisema baada ya tajili wa TP Mazembe, Moize Katumbi kumsajili, Samatta sasa wanamtaka Ochan wiki ijayo atakuwa kwenye majaribio huko.
Alisema wao kama Simba hawana tatizo kama Ochan akifaulu majaribio yake watakaa kwenye meza na Mazembe kujadiliana kuhusu bei ya mchezaji huyo.
''Kweli tumepata taarifa kutoka kwa Mazembe na mchezaji mwenyewe kuwa anatakiwa kwenda kwenye majaribio hivyo kwa kuwa mchezaji huyo yupo likizo tunafanya utaratibu iliaweze kwenda huko kwani sisi kama viongozi hatuna pingamizi lolote'' alisema Kaburu.
Alisema kwa upande wao bado wanazidi kuwa karibisha watu wanaowataka wachezaji wao kwani wanajua wachezaji hao mpira ndio maisha yaona kama wanapata sehemu nzuri zaidi ya Simba awana budi kuwaruhusu kwenda kutafuta maisha.
Alisema kuhusu suala la usajili katika timu yao mpya ya msimu ujao bado wanaendelea nayo japo kamati inatakiwa ipewe muda wa kutosha kuakikisha wanatafuta wachezaji wazuri na wenye kushindana.
"Suala la Samata kwao limemalizika hivyo mchezaji huyo sasa anatakiwa wiki ijayo kwenda TP Mazembe na kusaini mkataba wake na kuangalia ni suala lake la mshahara.
Simba tayari imeshawauza nyota wake kadhaa sehemu mbalimbali duniani kama kiungo Henry Joseph (Kongsvinger, Norway), Danny Mrwanda (DT Long An, Vietnam) na Haruna Moshi (Gefle IF, Sweden).
Mazembe yazidi kuibomoa Simba