Mazembe yazidi kuibomoa Simba

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
ABINGWA wa Afrika, TP Mazembe wameendelea kuisambaratisha Simba baada ya kumnasa Mbwana Samata kwa Shs 150m, sasa wamemgeukia kiungo wa klabu hiyo Patrick Ochan anayetarajia kuondoka wiki ijayo kwenda DR Congo kwa majaribio.

Hata hivyo habari zilizopatika jana kutoka Lumbushashi zimeeleza kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Uganda tayari ameshaanza majaribio na Mazembe.

Makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyanga 'Kaburu' alisema baada ya tajili wa TP Mazembe, Moize Katumbi kumsajili, Samatta sasa wanamtaka Ochan wiki ijayo atakuwa kwenye majaribio huko.

Alisema wao kama Simba hawana tatizo kama Ochan akifaulu majaribio yake watakaa kwenye meza na Mazembe kujadiliana kuhusu bei ya mchezaji huyo.

''Kweli tumepata taarifa kutoka kwa Mazembe na mchezaji mwenyewe kuwa anatakiwa kwenda kwenye majaribio hivyo kwa kuwa mchezaji huyo yupo likizo tunafanya utaratibu iliaweze kwenda huko kwani sisi kama viongozi hatuna pingamizi lolote'' alisema Kaburu.

Alisema kwa upande wao bado wanazidi kuwa karibisha watu wanaowataka wachezaji wao kwani wanajua wachezaji hao mpira ndio maisha yaona kama wanapata sehemu nzuri zaidi ya Simba awana budi kuwaruhusu kwenda kutafuta maisha.

Alisema kuhusu suala la usajili katika timu yao mpya ya msimu ujao bado wanaendelea nayo japo kamati inatakiwa ipewe muda wa kutosha kuakikisha wanatafuta wachezaji wazuri na wenye kushindana.

"Suala la Samata kwao limemalizika hivyo mchezaji huyo sasa anatakiwa wiki ijayo kwenda TP Mazembe na kusaini mkataba wake na kuangalia ni suala lake la mshahara.

Simba tayari imeshawauza nyota wake kadhaa sehemu mbalimbali duniani kama kiungo Henry Joseph (Kongsvinger, Norway), Danny Mrwanda (DT Long An, Vietnam) na Haruna Moshi (Gefle IF, Sweden).

Mazembe yazidi kuibomoa Simba
 
Sidhani kama kuchukua wachezaji ni kuibomoa timu, tusiwe kama timu za Misri ambazo wachezaji wake wengi wanacheza ligi za ndani tu. Acheni watanzania wakalete fedha nchi za wengine waje wazitumie humu nchini tukuze uchumi wa nchi!
 
Khee kuna mchezaji wa Simba anacheza Vietnam???? mmhh huyu anacheza mpira au anafanya mazoezi ya kivita..Vietnam hawa sijawahi kuwasikia kwenye soka mie
 
Yah ni sahihi tu kuuza wachezaji hasa kwenye timu yenye mafanikio kama TP Mazembe, ila Simba wanakazi ya ziada kukuza vipaji zaidi ili kuziba nafasi zinazoachwa wazi na hao wakali wanaondoka!
 
ni kweli zamani walikua na timu za watoto sijui ziliishia wapi maana zilikua zinakuza vipaji pia kitu kingine hizi timu kama hivi zinaingiza pesa ila utashangaa hakuna maendeleo yoyote!mfano kip[indi cha uongozi wa kina kaduguda!walikua wanapiga mawe sijui hata yalikua yanakwenda wapi!
Yah ni sahihi tu kuuza wachezaji hasa kwenye timu yenye mafanikio kama TP Mazembe, ila Simba wanakazi ya ziada kukuza vipaji zaidi ili kuziba nafasi zinazoachwa wazi na hao wakali wanaondoka!
 
Na Saleh Ally GPL
MABINGWA wa Afrika, TP Mazembe ya DR Congo imekubali kutoa kitita cha Sh milioni 273 kwa Simba ili iwachukue wachezaji wawili tu.

Mazembe imekubali kutoa dola 100,000 kwa Mbwana Samatta (pichani juu) na dola 80,000 ili imnase Patrick Ochan (pichani chini) hivyo kufanya imwage Msimbazi jumla ya dola 180,000 (Sh milioni 273).

Kwa upande wa Samatta kila kitu kimekamilika na Simba imekubali kuchukua dola 100,000 huku ikisubiri TP Mazembe imalizane na Ochan ambaye yupo Lubumbashi kwa ajili ya makubaliano.

Pamoja na kuilipa Simba kitita hicho, Mazembe imeonyesha jeuri ya fedha kwa kukubali kutoa dola 50,000 (Sh milioni 75) kwa Samatta.

Makubaliano ya Samatta yamefikiwa Ijumaa iliyopita katika hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam lakini kumekuwa na mvutano katika suala la mkataba huo uwe wa miaka mingapi.


“Mazembe inataka kuingia mkataba wa miaka mitano kitu ambacho hata kwa sheria za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) si sahihi.
Lakini ukiachana na hivyo, wanataka Simba isiwe na haki tena na Samatta. Hii si sawa pia kwa kuwa akiuzwa huko mbele hatutafaidika,” kilisema chanzo.

Kuhusu suala la Ochan, inaelezwa kuwa Mganda huyo naye anataka kulipwa dola 50,000 kama zilizotolewa kwa Samatta wakati timu hiyo imekubali kutoa dola 25,000 (Sh milioni 37,000).

Akizungumzia suala hilo, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ alielezea kwa ufupi tu.

“Suala la Samatta tumemalizana, ingawa kuna vipengele kadhaa tunamalizia vizuri na tayari tumetoa ruhusa, ila yeye anakwenda Lubumbashi wiki ijayo kusaini mkataba. Kuhusu Ochan, yupo huko huko sasa tunasubiri wamalizane naye maana tumewapa ruhusa ya kuzungumza naye,” alisema Kaburu.

Kutokana na fedha hizo, maana yake Simba ina nafasi ya kufanya usajili wa uhakika kama wahusika watatuliza akili.
 
Safi sana Msimbazi...........watoeni vijana wakapige kabumbu nje

Big up kwa Mbwana na Ochan....hope you succeed.....

Mkuu Ivuga unaona vijana wanachanuka mkuu..........
 
It is time and chance for them to shine in these CAF CL matches ili wapate fursa ya kuonekana Ulaya...

Fixtures of the First 1/8th Finals round the 15th Orange CAF Champions League, "CL 2011"


79 Enyimba FC v Ittihad
Reference to article 5 para 15 of the regulations of CAF Champions League, only one match will be played due to the actual circumstances in Libya. It was decided that this match will take place on 6th, 7th, 8th May 2011.
81 Grupo Desportivo Interclube v Moloudia Club d'Alger
82 Moloudia Club d'Alger v Grupo Desportivo Interclube

83 E.S.T. v ASC Les Jaraafs
84 ASC Les Jaraafs v E.S.T.

85 Raja Club Athlétic v Asec Mimosas
Reference to article 5 para 15 of the regulations of CAF Champions League, only one match will be played due to the actual circumstances in Cote d'Ivoire. It was decided that this match will take place on 6th, 7th, 8th May 2011.

87 El Hilal v Club Africain
88 Club Africain v El Hilal

89 Widad de Casablanca v TP Mazembe
90 TP Mazembe v Widad de Casablanca

91 Coton Sport de Garoua v E.S. De Setif
92 E.S. De Setif v Coton Sport de Garoua

93 Zesco United v Al Ahly
94 Al Ahly v Zesco United

DATES : 1st leg 22, 23, 24 April 2011
2nd leg 06, 07, 08 May 2011
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom