Mazda kwanini hazipendwi Tanzania ilhali bei yake ipo chini?

Wanasema ukinunua gari tofauti na Toyota hapa Bongo land ni sawa na kununua chupi, hilo linakuwa lako mpaka lichake.. maana hakuna wa kulinunua tena.
Ni kweli kabisa...
Ila ukiangalia kiuhalisia tumeambukizana mawazo ya kimasikini sana.

Unaweza kukuta mtu kwa mfano amependa sana Mazda ya aina flani na pesa anayo, basi atatokea B mtu mmoja na mawazo yake na kumwambia hili haliuziki basi jamaa anajikuta ameangukia mikononi mwa IST.

Kila mtu ana utaratibu wake...kwa upande wangu huwa ninnunua kitu ambacho moyo wangu unaridhika, nikikaa ndani naridhika, napata feeling....pia ninakuwa na mpango kuwa nitamiliki gari flani kwa miaka kadhaa. Huo muda ukifika hata nikiuza laki 8, sina hasara.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika pita pita zangu kwenye mitandao ya kuuza magari huko duniani, nimegundua ukiachana na Toyota na Magari ya ulaya bei zake sio rafiki kwetu dunia ya tatu

Nimegundua Mazda wana brand nzuri za Magari very economical and very reasonable price,

Mfano Mazda Cx-5 ya mwaka 2012 bonge la SUV mwonekano mzuri kuliko hata rav 4 au harrrier au kulger hadi unalo mkononi milion 22 kibongobongo nimelifuatilia kwa forum ya users wamelipendekeza fuel economy coz town trip km 12 per lita na lita 7 kwa km 100 high way.

Je, kwanini w hatupendi brand kama hizi ila tunachagua Toyota unakuta gari la miaka 20 iliyopita bei juu.

Wataalamu, Mazda zinashida gani kwa upande wa spears na maintainanceView attachment 1419166
Hivi kwanini Makonda alisema IST ni gari za kuhongwa ?
 
Ni kweli kabisa...
Ila ukiangalia kiuhalisia tumeambukizana mawazo ya kimasikini sana....

Unaweza kukuta mtu kwa mfano amependa sana Mazda ya aina flani na pesa anayo, basi atatokea B mtu mmoja na mawazo yake na kumwambia hili haliuziki.....basi jamaa anajikuta ameangukia mikononi mwa IST..
Upo sahihi kabisa, ila kwangu mimi siwezi kaa na gari kwa miaka miwili kwahiyo nanunua gari ninalolipenda ila nazingatia sana uwezekano wa kupata mteja kwa urahisi pindi nikitaka kuliuza.

Kwa mfano, mwaka juzi ndugu yangu alinunua Audi A4 lakini kashindwa kumpata mteja wa kuinunua na ana nia ya kubadilisha gari wakati mimi niliyekuwa na Rav 4 nimeuza na kununua gari nyingine kwa haraka.
 
Issue bei zake sio reasonable inakuwaje gari la miaka ya 90 huko technogia ya zamani lianuzwa bei mbaya kulinganisha na aina nyingine ya magari
Kwa sababu gari za toyota ni reliable. Izo za miaka ya 90 ni reliable kuliko BMW/Merc za miaka ya karibuni.
Zina low cost of maintainance. Izo brand kama BMW na MERC, AUDI na wenzao, gari zao zina depreciate kwa haraka sana. Unaweza kupata 2002 BMW 7 series kwa $1500 (bei ya gari tu) ambayo ni flagship model yenye features ambazo Markx, Camry na Crown haziingii ndani, unajua kwanini? Kwa sababu sio reliable, zinaharibika mara moja, service cost ni ghali, spare zake ni ghali ila ukija kwa toyota ni story nyengine.

Bei za magari mengine ndio sio reasonable, ila toyota, kwa kitu ambacho unadumu nacho miaka 20-30 zipo reasonable.
 
Issue bei zake sio reasonable inakuwaje gari la miaka ya 90 huko technogia ya zamani lianuzwa bei mbaya kulinganisha na aina nyingine ya magari

Hio Inaweza kuchangiwa na mambo mkuu,lkn mojawapo ni miaka ya 90's ndipo ilikua booming period kwa japanese cars na walikua na mapesa mengi sana waka-invest sana kwny R&D(Research and Development) so gari zao zilikua na Top notch tech na reliabilty ikawa hapo ndio nyumbani ndio maana mpk leo bado ziko expensive.

Miaka ya hivi karibuni Competition imekua kali sana na hata pesa wanayoinvest kwny R&D sio nyingi kama zamani lkn badi wanajitahidi sana.
 
Ni kweli kabisa...
Ila ukiangalia kiuhalisia tumeambukizana mawazo ya kimasikini sana....

Unaweza kukuta mtu kwa mfano amependa sana Mazda ya aina flani na pesa anayo, basi atatokea B mtu mmoja na mawazo yake na kumwambia hili haliuziki.....basi jamaa anajikuta ameangukia mikononi mwa IST....

Kila mtu ana utaratibu wake...kwa upande wangu huwa ninnunua kitu ambacho moyo wangu unaridhika, nikikaa ndani naridhika, napata feeling....pia ninakuwa na mpango kuwa nitamiliki gari flani kwa miaka kadhaa...huo muda ukifika hata nikiuza laki 8, sina hasara.



Sent using Jamii Forums mobile app

Nilinunua Mazda Tribute last year, ila dah! Kila mtu ananishangaa, wengine wananiuliza hiyo Rav 4 au? Ila nadhani itakuja kuwa na shida kama nitataka kuiuza.
Suala la Spare, wapo dealers kadhaa mjini Dar.


Alexander The Great
 
Kwasababu wananunua spare feki au second grade.

Spare original za Toyota hazina utofauti na Nissan au BMW.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa upande wa Nissan spea feki zimeshaanza kuenea na zinauzwa bei ya kawaida......

Hapa watu wawe makini....wengi wanapigwa feki kwa bei ya genuine wakiamini Nissan hazina spea feki...
I am talking this through personal experience...

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom