Mazda kwanini hazipendwi Tanzania ilhali bei yake ipo chini?

Vipo kuhusu hizi gari za kutoka Singapore? Zina sifa gani kwa wale waliowahi kutumia jamani tupeni uzoefu wenu
 
Oil za kubumba ni nyingi sana sokoni. Huwezi jua yani unaweza nunua oil kumbe chenga tu.
Ni muhimu pia kutambua oil ipi uweke kwenye gari na sio kila oil unatakiwa uweke. Hata izi synthetic niliwahi kusoma sehemu sio nzuri kwa magari ya zamani au yaliotembea sanaaa, wana recommend kutumia oil za kawaida.

Mimi naona ni uaminifu wa muuzaji, mana anaweza akakuletea Total ikawa total disaster nayo, kashachakachua china na kuibandika jina tu.
 
Daaah. Nilikuwa napenda sana hizi gari za singapore zimekaa luxury sana. Anyway acha nibadili muelekeo
Singapore hawana strict control measures kama Japan.

Ila Singapore wana magari mazuri (Europe Standards).

Singapore wanaweza kukuletea gari bovu ukaingia gharama za kulitengeneza. Na kinachooneshwa kwenye picha sio utakacholetewa.
 
Singapore hawana strict control measures kama Japan.

Ila Singapore wana magari mazuri (Europe Standards).

Singapore wanaweza kukuletea gari bovu ukaingia gharama za kulitengeneza. Na kinachooneshwa kwenye picha sio utakacholetewa.
Shukrani mkuu. Maana nilikuwa nayapenda sana haya magari ya kutoka kwa singasinga
 
Mkuu ina taarifa za hii gari japo kwa uchache tu? Na mm nahitaji kuliagiza hiili mwaka huu. Tupeane dondoo za hili gari mkuu kama unazijua baadhi ya sifa zake. Na je vipi kuhusu zinazotoka singapore. Zinahimili mikiki ya mazingira yetu ya kibongo?

Ni gari nzuri sana kwa ujumla wake, ubora wake wa engine na mifumo mingine na wanaoiendesha kila siku wanajua zinavyotulia barabarani na ni SUV inayoendesheka kama gari ndogo. Ina engine kama aina tatu nazozijua, 2.2 Diesel, 2.0 petrol na 2.5 Petrol. Kunaweza kuwa na engine nyingine lakini hizo ndo nazijua. Wameupdate design kuanzia mwaka 2017 ambazo mpaka kufika TZ na kuendesha inaweza kugharimu kuanzia mil 63 hivi. Za nyuma ya hapo zinaweza kagharimu kama mil 35-40 (lakini ni model nzuri sana).
Kwa kifupi kama unazipenda nunua, kwangu mimi naiweka hii mbele ya rav 4.
Muhimu ni kuwa hizi gari ni mjapan hivyo si lazima uagize Singapore
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom