Mayenga (mwalimu mkuu wa watu) ni fisadi...

Nostradamus

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2009
Messages
393
Likes
0
Points
0

Nostradamus

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2009
393 0 0
Kwa wale waliobahatika kusoma gazeti la Tanzania Daima la jana tarehe 13/01/2010 nadhani mtakuwa mlibahatika kusoma makala ya Mwalimu mkuu wa watu bwana Mayega yenye kichwa cha habari 'RAISI WANGU HEBU KWANZA TUWEKANE SAWA'

Sio nia yangu kuichambua ile makala wala kumjibu huyu kiumbe anayejiita mwalimu wa watu,bali siwezi vilevile kukaa kimya ninapoona waandishi wanapoelemewa na hisia za kisiasa kiasi cha kupofushwa macho yao na kuharibiwa bongo zao kiasi cha kushindwa hata kufikiri.Lakini zaidi ni kwamba naielewa jamii ya Kitanzania ilivyo na uvivu wa kuchambua mambo kiasi cha kudanganyika kirahisi na makala za waandishi wa habari na hivyo nahisi nikiwa kama mzalendo wa kweli nina jukumu la kuinusuru hii jamii yangu kutoka kwenye pingu za unafiki wa baadhi ya waandishi wetu.

Kuna mambo matatu katika makala ile ambayo ningependa wanajamii mliobahatika kuisoma tusaidiane kuyachambua.na mambo hayo ni kama yafuatayo:- matusi ya dhahiri dhidi ya raisi aliye madarakani,utetezi wa wazi dhidi ya raisi mstaafu MKAPA na mwisho ni uchochezi wa wazi na kushabikia machafuko.

Nikianza na matusi dhidi ya Raisi Kikwete, nadhani katika watu ambao hawatendewi haki na kupewa heshima yao katika nchi hii,basi ni raisi wetu mteule.Huenda amezidisha uungwana au labda ni mwanademokrasia aliyepitiliza,au huenda ni hulka yake ya uvumilivu na subira ndio inasababisha watu kama Mayega washindwe kuonyesha japo heshima kidogo kwa kiongozi wa nchi.Hebu ngoja nimnukuu huyu mwalimu mkuu wa watu katika moja ya kauli zake

"
Urais wa kisasa umejaa ufahari na mbwembwe za kimwambao ambazo kwa watu wengi hasa wa bara huziona kama ishara ya udhaifu, usultani na wakati mwingine ulofa tu.

Hebu ona na hii

"
Mtakuja kumpata rais wa kumaliza miaka mitano bila kumwona ameshika kitabu. Anatumia elimu yake ya zamani. Kutwa kiguu na njia analoleta halionekani sanasana michezo na mizaha mingi!

haya ni matusi ya dhahiri dhidi ya raisi ambaye ni sisi wenyewe tuliyemchagua tena baadhi ya watumishi wa mungu wakatuaminisha kuwa huyu ni chaguo la mungu.Na kwa ujumla haya ni matusi dhidi ya raia wa tanzania waliotumia haki yao ya kikatiba kumchagua KIKWETE kuwa raisi . Nina hakika Mayega hana haki ya kutukana raia wa Tanzania kwa kiwango hicho.hubu tuyaache hayo...
Swala la pili ni utetezi wa wazi dhidi ya Raisi mstaafu Mkapa, hebu ona hii

"
Nyerere alimfahamu Benjamin William Mkapa vizuri kuliko sisi. Anayetwambia leo kuwa Mkapa amechafuka huja ameuona ukosi wa shati lake. Jasho limtokalo mtu huchafua nguo zake. Utaufananishaje uchafu huu na ule ulioko kwenye ‘dampo

Hebu ona na hii


"Uamuzi wa Mkapa wa kuifanyia nchi hii ‘Overhall’ badala ya kuungaunga vipande alivyovikuta kuliifanya nchi yetu mpaka 2000 ikawa imerudisha heshima yake iliyokuwa imepotea katika mtazamo wa mataifa ya dunia. Katika miaka kumi ya uongozi wa Mkapa wananchi wa kawaida hawakuwahi kukumbana na mabadiliko yaliyowaongezea machungu ya maisha. Maisha yaliendelea kuwa yaleyale"

Hiyo haitoshi, malizia na hii ndio utakapojua nchi yetu ina mamluki

"Rais Mkapa alikuwa na makazi ya kudumu sehemu kuu tatu. Yeye alikuwa ameendelea kidogo, Lupaso alikozaliwa, Ukweni Moshi na Lushoto makazi mapya. Alipoenda likizo tulisema rais ameenda likizo kwao. Hakuwahi kuwa mtalii wa kutembelea vivutio vyetu vya kitalii na kufanya mapumziko yake katika hizo hoteli ghali kwa fedha ya walipa kodi wake maskini kwa kisingizio kuwa rais yuko mapumzikoni"

IPTL, AIR TANZANIA, NBC, MEREMETA, DEEP GREEN, EPA, KIWIRA COAL MINE, MIGODI YA TANZANITE, NYUMBA ZA SERIKALI, MSURURU WA VIWANDA, MISITU NA MALIASILI ZOTE ZILIZOVUNWA BILA TIJA. haya yote bwana Mayega hayaoni. Siasa zimemtia upofu huyu mzee.

Kweli hata shetani ana watetezi wake...hivi leo kuna mtu mwenye akili timamu anayethubutu kusimama na kumtetea Mkapa dhidi ya matendo aliyoyafanya dhidi ya watanzania???? huo ni ujasiri wa kifisadi..

Udhaifu wote tunaouona leo, misingi yake ilijengwa na Mkapa,akaipalilia na sasa tunachoshuhudia ni mavuno ya kazi ya Mkapa.

Sina dhamira ya kumtetea Kikwete kwani hata hivyo sio chaguo langu, ila hofu yangu ni hawa waandishi ambaoa ncha za kalamu zao zinatema wino wa sumu.Sumu ya kupotosha,kukana ukweli na kukweza maovu na mwisho wa siku kalamu zao zitatema wino wa kushawishi umwagaji damu......DAMU ZA WATANZANIA

kuhusu uchochezi nitajadili separately.

thanks
 

Marigwe

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Messages
226
Likes
4
Points
33

Marigwe

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2009
226 4 33
Mkumbushe na ufisadi mwingine wa TANESCO wakati NETGROUP SOLUTION walipolazimishwa kwa waendeshaji wa TANESCO kwa mtutu wa bunduki ili kukidhi deal iliyosukwa na shemeji yake BWM wa BOT ambaye ndiye aliewaleta na wakalipwa mabilioni ya dollars mpaka mshirika wake Enock Maganga akaugua figo shauri ya kuwa chapombe pale TAZARA. Jamani mnawasahau NETGROUP SOLUTION? Hivi ukweli menejimenti ya akina Luhanga ilikuwa na tatizo gani.
 

M-mbabe

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2009
Messages
6,294
Likes
6,028
Points
280

M-mbabe

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2009
6,294 6,028 280
haya ni matusi ya dhahiri dhidi ya raisi ambaye ni sisi wenyewe tuliyemchagua tena baadhi ya watumishi wa mungu wakatuaminisha kuwa huyu ni chaguo la mungu.Na kwa ujumla haya ni matusi dhidi ya raia wa tanzania waliotumia haki yao ya kikatiba kumchagua KIKWETE kuwa raisi
Whilst I agree kwamba una uhuru wa kutoa mawazo yako, kwa upande mwingine sikubaliani na wewe kuwa eti raisi huyu "tulimchagua sisi wenyewe". Sikubali kwa sababu mimi binafsi sikumchagua yeye.
To be frank, Mayega labda anaweza akaonekana amezidisha kidogo kwa mtizamo wa baadhi ya watu wachache kama wewe, lakini issue iko pale pale kwamba raisi huyu hawezi ku-make decision mpaka kwanza asome upepo unakwendaje - a typical populist! Na kwenye contribution yako naona umeandika "chaguo la mungu" - inaelekea huyu kweli ni chagu la mungu lakini si la Mungu yule ambaye sisi tunamwamini na kwa heshima kubwa jina lake linaanzia na capital "M". Mimi siamini kabisa kuwa eti raisi hafanyi maamuzi eti tu kwa sababu ni mvumilivu, mwanademokrasia, n.k bali ni kwa vile anaogopa kufanya maamuzi ambayo anahisi yataudhi watu halafu yakam-cost popularity!
 

Forum statistics

Threads 1,191,647
Members 451,726
Posts 27,716,446