Maximo anataka abembelezwe ama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maximo anataka abembelezwe ama?

Discussion in 'Sports' started by Mfumwa, Jan 14, 2009.

 1. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Maximo mbioni kuikimbia Tanzania
  Michael Momburi,Kampala

  KOCHA wa Kilimanjaro Stars, Marcio Maximo huenda akajiunga na moja ya klabu za Ligi Kuu ya Afrika Kusini au China.

  Mbrazil huyo ambaye mkataba wake unamalizika Julai, hajaonyesha nia ya kutaka kuongeza na ameishauri serikali na Shirikisho la soka la Tanzania limpe tenda msaidizi wake, Marcus Tinocco.

  Kocha huyo akizungumza mjini hapa jana alisema kwamba amezungumza na klabu mbili za Ligi Kuu za nje, lakini akaziambia zisubiri kwanza mkataba wake umalizike.

  "Nimezungumza na klabu moja ya China na nyingine ya Afrika Kusini wote wananihitaji, lakini nimewaambia wasubiri kwanza nimalize mkataba wangu nikabidhi majukumu niliyopewa,"alisema Maximo.

  "Kila mmoja alikuwa akitaka nivunje mkataba huku halafu niende nikakataa kwa vile niliwaambia tatizo sifedha.

  "Lazima uangalie na utu na ulipoanzia, umefikia wapi. Nikishamaliza mkataba wangu ndio nimewaambia nitakaa nao tuongee vizuri,"alisema kocha huyo na kugoma katu katu kutaja jina la klabu hizo kwa madai kuwa ni siri.

  Kocha huyo alisema kwamba bado hajafikiria kubadilisha mawazo ya kuondoka Tanzania.

  Maximo alisema kwamba ameanzisha msingi mzuri ambao anahitaji mtu mwenye mtazamo mwingine kuuendeleza.

  Tangu akabidhiwa Stars miaka miwili iliyopita, Maximo amecheza mechi 39 akiwa ameshinda 17, sare 13 na kupoteza tisa.

  Source: Mwananchi Read News
   
 2. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Hapo ni danganya toto tu hakuna lolote anataka tumopne hot cake ili serikali imuongezee mkataba mwingine mnono. Mimi nadhani amesaidia sana kukuza soka letu na tulipofikia na kwa usaidizi wa karibu wa serikari we can move on with or without him.
   
Loading...