MAXCOM wanastahili kupewa tenda Uwanja wa Taifa?

MAXCOM wanastahili kupewa tenda Uwanja wa Taifa?

JoeMan

Member
Joined
Oct 19, 2017
Posts
23
Reaction score
15
Ni ukweli kwamba MAXCOM ni moja kati ya kampuni zilizoleta mabadiliko makubwa nchini katika sekta ya fedha, kwa kurahisisha miamala na kuisogeza zaidi kwa jamii kupitia huduma kama vile MAX MALIPO.

Ni bahati mbaya kwamba kwa makusudi au kwa kutofahamu, uongozi wa kampuni hii umeruhusu kirahisi kabisa heshima hiyo waliyojijengea kuporomoka mbele ya macho ya jamii…

MAXCOM ndio wenye jukumu la kukusanya fedha kwenye vituo vya UDART (mwendokasi). Wiki iliyopita, uongozi wa MAXCOM ulifumbia macho mgomo uliofanywa na ‘cashiers’ wao wanaotoa huduma kwenye vituo vya mwendokasi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa abiria wa maeneo ya Ubungo, Fire, DIT na Kisutu ikiwa ni pamoja na kufungwa kwa kituo cha Kibo kwa siku mbili!

Mgomo huo lazima utakuwa umewaingiza hasara UDART (hata kama hawajasema hadharani) na wananchi kwa ujumla, ingawa lawama huelekezwa UDART!

Sasa ninajiuliza, hawa wakipewa tenda ya kuuza tiketi Uwanja wa Taifa kisha ‘cashiers’ wakagoma kutatokea nini siku hiyo? Je, MAXCOM wanastahili kuaminika na kupewa miradi mikubwa ya kutoa huduma za kukusanya fedha kama vile Uwanja wa Taifa, usafiri wa reli au hata kuendelea kutoa huduma za mwendokasi?

Iwapo uongozi wa MAXCOM haujatoa onyo wala adhabu kwa waliogoma wiki iliyopita, ni wazi kuwa uongozi huo ulihusika au uliuandaa mgomo huo…

Nawasilisha…
 
shida ya uongozi wa maxcom nadhani ni hii, wakiandaa vikao vya mawakala wao wanakuja watu wa chini sana ki utendaji na ambao kabla ya kikao wanasema mwanzo kabisa wanataka kusikia wanachopenda wao, ukiongea kero yao wanakukatisha, kwa hiyo wenye kampuni pengine wanajua wako vizuri
 
Back
Top Bottom