Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,036
- 3,929
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ufafanuzi juu ya utoaji wa huduma ya Ticketi za kielektroniki kwenye Mradi wa mabasi ya mwendo kasi.
Kampuni ya Maxcom Africa PLC ni mmoja kati ya wabia wanaoshiriki katika utoaji huduma katika Mradi wa uendeshaji wa Mabasi ya mwendo kasi Jijini Dar es Salaam, Kazi ambayo ilianza mnamo tarehe 16 Mei 2016 pindi tu Mradi huu ulipozinduliwa katika awamu ya Kipindi cha mpito (Interim period).
Kuanzia tarehe 13 Aprili 2018 kumekua na hali ya sintofahamu katika vituo vya Mwendo kasi, na kumekuwapo na uuzwaji wa tiketi za karatasi (za vishungi) ambazo hazitolewi kwenye mfumo wa Tiketi za Kielektroniki ulioidhinishwa na wasimamizi wa mradi huu (DART Agency), na pia kumekuwapo na nyakati ambazo abiria wanasafirishwa bila kulipa nauli.
Tunaomba ifahamike kwamba haya yanayoendelea yanaratibiwa na kampuni ya UDA-RT ambayo mbia wake mkubwa ni Simon Group ambao wanamiliki mabasi haya ya Mwendokasi. Maxcom Africa PLC waliingia mkataba kutoa huduma ya tiketi za kielektroniki katika mradi huu wa Mwendokasi chini ya kampuni ya UDA-RT kutokana na maagizo yaliyotolewa na serikali.
Kutokana na Mkataba huo Maxcom Africa PLC tuliweka Mifumo, Rasilimali watu, teknolojia na wasimamizi katika mradi huu. Ila katika hali isiyo ya kawaida tangu mradi huu umeanza Kampuni ya UDA-RT imeshindwa kuilipa kampuni ya Maxcom Africa PLC gharama za uendeshaji, uwekezaji na hata stahiki za wafanyakazi (ikiwamo michango ya hifadhi za jamii na tiba) hivyo mnamo Februari 2017 kampuni ya Maxcom Africa PLC tuliamua kufungua kesi ya madai katika Mahakama kuu ya Tanzania, Kesi ambayo mpaka sasa inaendelea kusikilizwa.
Kwa zaidi ya Miaka 2 sasa UDA-RT wamekua wakikwepa kulipa stahiki hizi za wafanyakazi, japo Maxcom imeendelea kutoa huduma iii kulinda heshima ya Mradi na nchi yetu.Kampuni ya Maxcom Africa PLC ni mmoja kati ya wabia wanaoshiriki katika utoaji huduma katika Mradi wa uendeshaji wa Mabasi ya mwendo kasi Jijini Dar es Salaam, Kazi ambayo ilianza mnamo tarehe 16 Mei 2016 pindi tu Mradi huu ulipozinduliwa katika awamu ya Kipindi cha mpito (Interim period).
Kuanzia tarehe 13 Aprili 2018 kumekua na hali ya sintofahamu katika vituo vya Mwendo kasi, na kumekuwapo na uuzwaji wa tiketi za karatasi (za vishungi) ambazo hazitolewi kwenye mfumo wa Tiketi za Kielektroniki ulioidhinishwa na wasimamizi wa mradi huu (DART Agency), na pia kumekuwapo na nyakati ambazo abiria wanasafirishwa bila kulipa nauli.
Tunaomba ifahamike kwamba haya yanayoendelea yanaratibiwa na kampuni ya UDA-RT ambayo mbia wake mkubwa ni Simon Group ambao wanamiliki mabasi haya ya Mwendokasi. Maxcom Africa PLC waliingia mkataba kutoa huduma ya tiketi za kielektroniki katika mradi huu wa Mwendokasi chini ya kampuni ya UDA-RT kutokana na maagizo yaliyotolewa na serikali.
Kutokana na Mkataba huo Maxcom Africa PLC tuliweka Mifumo, Rasilimali watu, teknolojia na wasimamizi katika mradi huu. Ila katika hali isiyo ya kawaida tangu mradi huu umeanza Kampuni ya UDA-RT imeshindwa kuilipa kampuni ya Maxcom Africa PLC gharama za uendeshaji, uwekezaji na hata stahiki za wafanyakazi (ikiwamo michango ya hifadhi za jamii na tiba) hivyo mnamo Februari 2017 kampuni ya Maxcom Africa PLC tuliamua kufungua kesi ya madai katika Mahakama kuu ya Tanzania, Kesi ambayo mpaka sasa inaendelea kusikilizwa.
Mnamo tarehe 13 Aprili 2018 UDA-RT walitangaza kuiondoa kampuni ya Maxcom Africa kwenye mradi na kuipa kazi kampuni ya TTCL corporation bila kufuata taratibu zozote za kimkataba, bila kutoa notisi na bila kurasimishana makabidhiano ya mradi.
Hivi karibuni UDA-RT wametumia nguvu kuwatisha na kuwatoa wafanyakazi waliokuwa wanatoa huduma ya tiketi za kielektroniki katika vituo vya Mwendokasi, bila kufuata taratibu zilizoainishwa kwenye mikataba ya ajira, hii ikiwa ni pamoja na kuwalazimisha wafanyakazi wa Maxcom Africa PLC kuvunja Mikataba yao ya ajira na kampuni ya Maxcom Africa PLC na kusaini mikataba mipya na kampuni ya UDA-RT iii waweze kuendelea kufanya kazi.
Sisi kama Maxcom Africa PLC tunaamini haya yanayofanywa na UDA-RT ambaye mbia wake mkubwa ni Simon Group hayana nia njema kwa taifa hili, hayana nia njema kwenye mradi huu wa usafiri wa Mwendokasi, na pia hayana nia njema kwenye maendeleo ya Nchi yetu.Ni Dhahiri haya yanaweka doa katika mradi huu na yanaweza kuleta mazingira ya ufisadi na dhuluma hasa ikizingatiwa kesi ya Madai ipo Mahakamani.
Tunawaomba Watanzania na Umma uelewe kwamba huduma inayotolewa katika vituo vya mwendo kasi isiyohusisha tiketi za kielektroniki inatolewa na UDA-RT na sio Maxcom Africa PLC.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma
======Tiketi zinazotolewa na UDA-RT hizi hapa