Max Melo, mwana mapinduzi wa Tanzania?

Sep 29, 2016
34
125
MAX MELLO MWANA MAPINDUZI WA TANZANIA.?

Na; Noel C Shao

Katika historia ya dunia tuliwahi sikia historia za wana mapinduzi, mateso waliyo wahi yapata na njia zao katika kufichua uovu, Hasa wa tawala kandamizi duniani. Wanaharakati wengi ni wafuasi wa haki dhidi ya dhuluma, ni nuru katika uongo, unyanyasaji, uovu, ukandamizwaji, mateso na kila aina ya uonevu dhidi ya binadamu.

Wanaharakati ni wa kweli, hawako tayari kusema uongo kwa kusudi la kuficha ukweli. Ingawa ukweli siku zote una gharama zake kama kufungwa, kuteswa, kuumizwa, kuitiwa kizuizi na hata kuuwawa. Ndio maana kuna watu hujikuta wanaujua ukweli ila katika vifua vyao hawana mioyo ya ujasiri na ushujaa wa kusema ukweli.

Na mbaya zaidi matunda na jasho la wanaharakati huwa si kwa faida yao, wengi hufa wakiwa na umri mdogo na kuucha wengine wakifaidi kazi za jasho na damu zao. Mfano; Martin Luther aliuwawa akiwa na umri wa miaka 39, Enersto che Guevara nae aliuwawa na miaka 39, Thomas Noel Sankara aliuwawa na miaka 37 hiyo ni mifano michache ya jinsi gharama za mapambano zilivyo.

Dunia iko katika vipindi tofauti, maendeleo ya sayansi na technolojia yana kasi labda kuliko vitu vyote. Serikali nyingi duniani zilipendelea kutumia vyombo vya habari katika kueneza siasa, itikadi, sera na falsafa za nchi. Katika maendeleo haya changamoto kubwa ni jinsi serikali zilizo shika dola hazitaki kukoselewa, kukosoa serikali iliyopo madarakani ni “kosa” kama binadamu wengi wasivyo penda kukoselewa. Kwa muktadha huo vyombo vingi vya habari vikajikuta vinajiingiza katika mtego wa kusifia tu, na vile vingine vilivyo jaribu kukosoa hujikuta vikifungiwa au kutiwa zengwe.

Changamoto nyingine ya vyombo vya habari, ni habari nyingi “huchakakuliwa” kabla ya kurushwa au kuundikwa, hivyo kufifisha harkati za kuisema au kuikosoa serikali iliyopo madarakani.

Mathalani bado watu wanapenda kusema ukweli “naked truth” sasa dunia inashughudia kuibuka kwa kundi la wanamapinduzi wa kimitandao “cyber revolutinarities” hawa wapo tayari kufichua uovu wa serikali zisizo pendwa kukosolewa, kundi hili la wanaharkati nao hujikuta katika mateso yale yale ya wanaharakati wa mwanzo kama kuuwawa, kuitwa vizuizini mfano Julian Assange(niliwahi andika habari zake) ambaye kichwa chake kinahitajika pale marekani kwa nguvu zote. Edward snowden aliyekataa mshahara wa zaidi ya hela ya kitanzania ml.500 akaamua kufichua siri za serikali za marekani, huyu yupo katika makazi ya muda Russia siku akitoka tu, ahitajika pale marekani akajibu zaidi ya mashtaka matatu. Wote hawa wanaitwa ni magaidi wa kimtandao “cyber terrorist”

Sasa tureje katika mandhari ya Tanzania, tukutane na huyu mwanamapinduzi wa kitanzania Max Melo mwanzishaji wa Jamii Forum, njia walizo pitia wenzake ndizo anazo pitia yeye, tayari amewekwa rumande kwa kuamua kuficha siri za watumiaji wa Jamii Forum, huu si tu ni ujasiri bali kuheshimu terms and condition za kumiliki mtandao kuwa hutatoa siri (privacy)za wateja.

Ndio maana miaka ya nyuma kampuni ya “APPLE” iligoma kutoa taarifa za mteja wake ambaye tayari alikuwa ameshafariki, ili zitumike katika uchunguzi na FBI ambao walishindwa kuhack taarifa zake. Ila sidhani kama mmiliki wa apple alikamatwa.

Serikali inashindwa kuingilia hasa moja kwa moja “mitandao ya kijamii” hasa “server”. Katika mitandao ya kijamii huko hakuna “editing” serikali huvuliwa nguo, husemwa, hupewa makavu na hukoselewa moja kwa moja, ndio maana baada ya kutumia njia zote kupata taarifa za wateja wa JF hasa wanao ikosoa serikali sasa wanaanza kupambana na mmiliki.

Hata marekani walijaribu kupambana na mtandao wa “wikileaks” wakashindwa waliamua kupambana na Julian Assange, kama Tanzania inavyo pambana na MAX.

Ninacho kiona kwa kuwa tayari sheria ya huduma za habari imeshapitishwa, katika vyombo mbalimbali vya habari hakutakuwa na taarifa anuwai, hivyo itawapelekea watu kuingia katika mitandao kupata habari, ndio maana kuna upigwaji vita mitandao ya kijamii.

Mwanaharakati yoyote kama MAX hawezi kukubali kusema uongo, na anaamini “only revealed injustice can be answered” (uovu uliofichuliwa ndio unaweza kujibiwa). JF wamegoma kutoa taarifa za wateja wake ili waendelee kukosoa, kwani wanajua katika vyombo vingine, habari hupindishwa.

Kwanini serikali haipendi watu wajue kipi kinaendelea ndani, naamini ili binadamu aweze kufanya jambo lolote la werevu ni lazima ajue mambo yanayo endelea (for a man to do any thing intelligent he has to know what’s actually going on). Ila hapa kuna pingamizi mno, ndio maana sishangai kwanini mliliki wa “Tanzagiza” nae ni most wanted. Huyu yumo katika kundi la uanaharakati wa kimtandao “cyber activism”.

Mwisho huwa naugawa mwili wa binadamu katika sehemu kuu tatu, kwanza sehemu ya ubungo ambapo ndipo zilipo akili, ambazo zikiwa timamu hutoa zao bora la fikra, pili kinywa, ambacho hutoa maneno yanayo paswa kujaa hekima, maarifa na busara, pia kinywa kisicho ropoka hovyo. Tatu, sehemu ya kifua, hii ndio muhimu zaidi kwani ndiyo imebeba moyo ambao hutakiwa kuwa jasiri na moyo uliyojaa ushujaa, katika hili ndicho chanzo cha mabadiliko yoyote hasa ya kimapinduzi, na ujasiri ni heshima pekee katika mapambano ya kudai mapinduz. Kumbuka penye moyo wa uoga hakuna maendeleo wala mapinduzi..

[HASHTAG]#bringbackbeb[/HASHTAG]
[HASHTAG]#freemaxmello[/HASHTAG].

Noel C S..
 

jabulani

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
4,346
2,000
Melo akitoka lupango JF itakuwa maarufu mpaka itakuwa chanzo kikuu cha kupata habari tz.

Kiama kwa ccm.

Katika kuinyoosha nchi hapa mkulu amechemka, dunia itapata picha mbaya juu ya utawala wake.

Alituahidi tanzania ya viwanda kumbe moyoni anawaza tanzania ya utalii, ananunua misururu ya ndege isiyokuwa na tija.

Mtalii gani atatembelea nchi isiyokuwa na uhuru wa kutoa maoni.
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,776
2,000
Eti katiba naiweka pembeni, nataka kunyoosha nchi, yaani macho makavu kabisa bila hofu mtu anachezea katiba na sheria za nchi
 

Farudume

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
3,953
2,000
Mimi huwa naamini kabisa kwamba "mtu yeyote anayetembea katika haki haaibiki kamwe".
 

Kibo255

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
4,408
2,000
[HASHTAG]#freemaxencemelo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#TunamtakaBenAkiwaHai[/HASHTAG]
[HASHTAG]#JusticeForLema[/HASHTAG]
[HASHTAG]#usirudiekosa2020[/HASHTAG]
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom